Mwalimu
JF-Expert Member
- Aug 21, 2008
- 1,581
- 1,069
Inasikitisha sana kuona jinsi ugonjwa huu wa COVID 19 ulivyotuathiri hata kwenye fikra na mitazamo yetu!
Shukrani kwa wanasiasa wetu leo ghafla kila mtu amekuwa nguli na mtaalamu wa afya na tiba... ghafla wataalamu wa afya tiba hawasikilizwi tena ushauri wao unabezwa, ghafla kila anayeshauri kufuata kanuni za tiba anabezwa kuwa ametumwa na mabeberu kutudhoofisha kiuchumi!
Ugonjwa umeua ndugu zetu kwa wingi tu lakini bado tunajipa jeuri kwamba tuko salama... labda kwa sababu tumegoma kutangaza data tumejificha vichwa ardhini kama mbuni. Hatutaki kupima, hatutaki social distancing, hatutaki barakoa, hatutaki chanjo yote haya tunasema ni mbinu chafu za mebeberu tutumie tiba zetu za asili.... Lakini ukihoji tafiti za kuthibitisha kwamba kupiga nyungu au kunywa bupiji zinatibu corona hupati majibu! Ile dawa tuliyotuma ndege Madagascar kwenda kuichukua sijui nayo iliishia wapi! Lakini tuko mstari wa mbele kupiga kelele dawa za mabeberu na kuwabeza wanaoziongelea kwamba wametumwa!
Tumekuwa taifa la kusikiliza zaidi blah blah za wanasiasa zaidi kuliko kujielimisha, kila kitu tumegeuza kuwa siasa kila mtu amekimbilia huko.... ndio maana leo darasa la 7 anamdharau PHD kuwa hana mchango wowote kwa Taifa (only in Tanzania).
Marehemu Banza Stone aliwahi kuimba ikiwa unaona elimu ni ghali basi jaribu ujinga.... na sisi ndio tunakoelekea huko!