#COVID19 COVID-19 is historical in Tanzania: Why don't USA, UK, EU and others copy from Tanzania how to fight against the Corona Virus?

Inasikitisha sana kuona jinsi ugonjwa huu wa COVID 19 ulivyotuathiri hata kwenye fikra na mitazamo yetu!

Shukrani kwa wanasiasa wetu leo ghafla kila mtu amekuwa nguli na mtaalamu wa afya na tiba... ghafla wataalamu wa afya tiba hawasikilizwi tena ushauri wao unabezwa, ghafla kila anayeshauri kufuata kanuni za tiba anabezwa kuwa ametumwa na mabeberu kutudhoofisha kiuchumi!

Ugonjwa umeua ndugu zetu kwa wingi tu lakini bado tunajipa jeuri kwamba tuko salama... labda kwa sababu tumegoma kutangaza data tumejificha vichwa ardhini kama mbuni. Hatutaki kupima, hatutaki social distancing, hatutaki barakoa, hatutaki chanjo yote haya tunasema ni mbinu chafu za mebeberu tutumie tiba zetu za asili.... Lakini ukihoji tafiti za kuthibitisha kwamba kupiga nyungu au kunywa bupiji zinatibu corona hupati majibu! Ile dawa tuliyotuma ndege Madagascar kwenda kuichukua sijui nayo iliishia wapi! Lakini tuko mstari wa mbele kupiga kelele dawa za mabeberu na kuwabeza wanaoziongelea kwamba wametumwa!

Tumekuwa taifa la kusikiliza zaidi blah blah za wanasiasa zaidi kuliko kujielimisha, kila kitu tumegeuza kuwa siasa kila mtu amekimbilia huko.... ndio maana leo darasa la 7 anamdharau PHD kuwa hana mchango wowote kwa Taifa (only in Tanzania).

Marehemu Banza Stone aliwahi kuimba ikiwa unaona elimu ni ghali basi jaribu ujinga.... na sisi ndio tunakoelekea huko!
 
Mkuu Nguruvi3 , una matokeo ya mwaka mmoja mbele ya chanjo ambayo tangu ianze kutolewa haijafikisha mwaka!!!!?????? UNALIPWA NA NINI KUTETEA UBATILI KWA GHARAMA KUBWA HIVYO?
Hee unashangaa hilo, inategemea unatazama sayansi kwa mtazamo gani.
Watu wapo Mars 300 M Miles
Watu wanaweza ku predict nini kinatokea na kinatokea kama kilivyo !
Yaani wanapeleka chombo katika o gravity halafu Maili 300 chombo kinaji control! una doubt Sayansi

Halafu unashangaa mwaka 1 matokeo yanajulikanaje, wakati umeeeleza matokeo ya watu kupona baada ya kutumia nyasi a.k.a nyungu chini ya mwaka 1. Hii imekaaje ! kwamba 'sayansi' yako ni bora au! ha ha ha
Umepoteza integrity ya majadiliano, naomba nikuache kwa kukumbia hivi...
Integrity ya majadiliano inapotea tunapoanza kuamini mapambio! na nyasi bila kuwa na uwezo wa kuzieleza

Mlenge alijaribu kutuletea nyasi na nyungu za India, well, leo kimyaa maana huko wanakotengeneza nyungu sasa hivi drip ni kwenye miti , Oksijeni ni bidhaa adimu sana. Hali ni mbaya sana.
Hakuna sehemu nimekuhoji kwamba kwanini hujibu baadhi ya hoja, kama ipo nioneshe.
Soma bandiko lako hapo juu! Haya mambo ni magumu hayahitaji ufahamu wa bahati nasibu

Corona inashambulia system za mwili na hasa mapafu, si vita ya uchumi.
Virus hatibiwi kwa mapambio hayo tuyaache huko yaliko atakaye ayafuate.

Dunia inapiga chanjo, sisi tunatumia data za dunia kutafsiri kazi za dunia!
Hatuwezi kufanya gene sequencing lakini tunahoji waliofanya!

Chanjo ije kwa anayetaka, asiyetaka aende kwenye Mapambio ni haki yake

Mwalimu kauliza ile mitishamba ya Madagascar vipi?
 
Kwahiyo kwako huko ndio Kuhoji kwangu ati kwanini hunijibu hoja Fulani na fulani?
Usilazimishe hoja Mkuu, Haipendezi.
 
Mkuu Nguruvi3, JE KILA PREDICTION HUTIMIA KWA USAHIHI WAKE 100%?
Juzi chombo cha China kimeanguka kinyume na matarajio na matamanio yao, je haikuwa sayansi?

Unazoita nyasi ni organics ambazo nyingine zipo kila siku katika Milo yetu....

Kipi kisichowezekana kwako? Kwamba hakuna uwezekano wa uwepo wa Sayansi iliyo bora kushinda hiyo uipiganiayo, na huku bado isiweze kutafsiri mfupa wa goti unaungaje pasipo kuguswa mgonjwa ndani muda mfupi?

Imani yako juu ya sayansi haina tofauti na ulevi wa watu wa dini, hakuna watakacho kuambiwa wala kusikia.

Dawa ya Madagascar kama haijaletwa hadharani, basi tambua kuwa haijakidhi vigezo vya mamlaka husika, sawa na Chanjo leo.

Itoshe tu.
 
Halafu, namna yako ya kuhoji Vita ya Uchumi na Corona, kwangu naona inashusha hadhi ya jukwaa. Wewe si wa kujenga hoja kitoto hivyo...unalifanya kwa makusudi.

Kinachosemwa ni Uwezekano wa Virusi vya Corona kuwa vimetengenezwa kwa makusudi ya Ushindani wa kiuchumi wa mataifa makubwa, Nasi ni nyasi ziumiazo katika vita hiyo ya wenye nguvu kubwa kiuchumi.
(Nimefafanua hilo si kwa kufikiri wewe hujui, NO. Najua wazi unalijua vema, ila umekusudia kupotosha. Inachosha)
 
Mkuu Nguruvi3, JE KILA PREDICTION HUTIMIA KWA USAHIHI WAKE 100%?
Juzi chombo cha China kimeanguka kinyume na matarajio na matamanio yao, je haikuwa sayansi?
Hapana ! Sayansi inaeleza chombo cha China ilikuwa ni 'human error kutokana na miscalculation'
Vyombo vinavyokwenda katika space vina stage za detachment na hutokea kabla ya kuingia katika Orbit.

Kilichotokea kwa China ni kuwa detachment ili miss na kuingia katika orbit bila mpango na kurudi katika Earth bila mpangilio. NASA walikuwa tayari kukilipua kama kingalikuwa kinaelekea kwenye makazi ya watu.

Chombo hicho cha China kilikuwa katika mwendo wa 18,000 Miles/hr sawa na KM 29,000/hr.

Ni hivi kutoka New York hadi Dar ni KM 13,000 na chombo kingefika katika Dakika 30 .
Katika kasi hiyo bado wanasayansi walikuwa na hesabu za kukitungua. Think about that!

Wanasayansi wana uwezo wa ku isolate protein kutoka kitu usichokiona na hutakiona katika maisha yako kinachoitwa Virus. Wanajua coding n.k. leo una doubt Sayansi? Please
Unazoita nyasi ni organics ambazo nyingine zipo kila siku katika Milo yetu....
Kuna dawa za asili hazina doubts, na hizi tunazijua. Dawa zinatokana na miti lakini si kila mti ni dawa.

Nyungu ni nyasi tu tunazoambiwa tufukize.
Kila nyumba ina nyungu yake, hili linapinga logic wala halihitaji kukaa darsa lolote lile.

Nina uhakika hata Watu wa Mapambio wanauelewa ukweli huu.Miti ni dawa lakini si kila mti ni dawa.
Kipi kisichowezekana kwako? Kwamba hakuna uwezekano wa uwepo wa Sayansi iliyo bora kushinda hiyo uipiganiayo, na huku bado isiweze kutafsiri mfupa wa goti unaungaje pasipo kuguswa mgonjwa ndani muda mfupi?
Ipo na hiyo tunaihitaji, hata hivyo hadi itakapokuwepo hatuwezi kuamini tu kwasababu kuna mtu kasema jukwaani. Tunataka maelezo ya nini kinafanyika, inafanyike na kwanini.
Siyo tangazo la mtu mmoja tu ambaye kwa imani zake au hisia zake anahisi hivyo.
Dawa ya Madagascar kama haijaletwa hadharani, basi tambua kuwa haijakidhi vigezo vya mamlaka husika, sawa na Chanjo leo.

Itoshe tu.
Ya madagascar iliua sana hadi wakapiga magoti WHO.
Kwetu haikufanyiwa kazi ilikuwa sawa na Covidol na Mpiji tu.

Chanjo haijakidhi vigezo gani wakati kamati ndio imeundwa? hee ! unataka kusema chanjo imeshafanyiwa tathmini! Real!

Mwisho, kauli ya 'vita ya uchumi ' si yangu hivyo usinichukie. Kama kauli hiyo inashusha hadhi ya jukwaa hili, fikiria hadhi ya nchi ipoje? Maana tuliambiwa hadi mask zimewekewa vitu na watu wanaojua siri za nchi

Virus anakula mapafu halafu tunaambiwa ni vita ya uchumi! ndio maana ilikatazwa kusema Corona eti changamoto ya kupumua ! Nini kilifichwa? Hakuna takwimu lakini wenzetu mnasema '' Hali ni poa''
Tena unajinasibu bila aibu '' watu hawavai mask'.
 
Inasikitisha sana kuona jinsi ugonjwa huu wa COVID 19 ulivyotuathiri hata kwenye fikra na mitazamo yetu!

Shukrani kwa wanasiasa wetu leo ghafla kila mtu amekuwa nguli na mtaalamu wa afya na tiba... ghafla wataalamu wa afya tiba hawasikilizwi tena ushauri wao unabezwa, ghafla kila anayeshauri kufuata kanuni za tiba anabezwa kuwa ametumwa na mabeberu kutudhoofisha kiuchumi!
Wataalam walioshauri walipoteza kazi, tukaambiwa wanastaafu. Wakaletwa wapiga debe tukaambiwa watalaam
Ugonjwa umeua ndugu zetu kwa wingi tu lakini bado tunajipa jeuri kwamba tuko salama...
Huyu bwana tunayeongea naye kasema '' watu wapo Poa, kuna watu hawajawahi kuvaa barakoa''
Kwamba, anaamini kwa dhati hakuna tatizo licha ya misiba. Anaamini kusema kuna Corona ni kukosa uzalendo ! Kaaminishwa ni vita ya uchumi hii . Tena kaambiwa si Corona ni changamoto ya kupumua.
labda kwa sababu tumegoma kutangaza data tumejificha vichwa ardhini kama mbuni.
Bila data jibu lolote ni sahihi, kwamba kuna Corona au hakuna. Data ndizo zina prove kama hakuna hakuna proof
Hatutaki kupima, hatutaki social distancing, hatutaki barakoa, hatutaki chanjo yote haya tunasema ni mbinu chafu za mebeberu tutumie tiba zetu za asili.... Lakini ukihoji tafiti za kuthibitisha kwamba kupiga nyungu au kunywa bupiji zinatibu corona hupati majibu! Ile dawa tuliyotuma ndege Madagascar kwenda kuichukua sijui nayo iliishia wapi! Lakini tuko mstari wa mbele kupiga kelele dawa za mabeberu na kuwabeza wanaoziongelea kwamba wametumwa!
Hapa Jamvini waliaminisha India ndio wenyewe kwa nyungu. Leo hali ipoje? Dunia inakimbilia kuokoa hali
Nimewauliza mara nyingi sana iweje kila nyumba iwe na nyasi zake na nyungu yake. Hakuna jibu
Tumekuwa taifa la kusikiliza zaidi blah blah za wanasiasa zaidi kuliko kujielimisha, kila kitu tumegeuza kuwa siasa kila mtu amekimbilia huko.... ndio maana leo darasa la 7 anamdharau PHD kuwa hana mchango wowote kwa Taifa (only in Tanzania).
Ukizungumzia vaccine, social distancing and mask unaambiwa umetumwa na mabeberu.

Wao wakiumwa wanatumia ventilator na dawa za mabeberu.
Huko Airport kuna mashine kutoka kwa mabeberu.
Tumeanishwa matumizi ya akili ni ukosefu wa uzalendo!
 
Madagaacar hao wamekubali yaishe....
 
Nguruvi3, naona kama unazungukazunguka na hoja zilezile zisizo na misingi imara ya kutetea.

1. Hakuna Sayansi iliyo nje kabisa ya Human Errors. Hivyo madai yako ya kuwa una hakika wa usalama wa chanjo baada ya mwaka mmoja ni Uongo.

2. Hoja ya Vita ya Kiuchumi wewe binafsi unaelewa aliyetoa hakuwa na maana hiyo unayoing'ang'ania Leo. Umekula kiapo cha Upotoshaji.

3. Hakuna mtu amesema kila mti ni Dawa, huu ni upotoshaji mwingine. Kama unakubali zipo tiba asilia nje ya sayansi ya leo, kukataa Nyungu kisa imesemwa na mtu unayemchukia, hilo ni tatizo lako si nyungu. Nyungu zipo hata kabla haijasemwa na huyo mtu.

4. Nilishasema mwanzo kuwa, Mamlaka haijaidhinisha bado au haitaidhinisha kabisa Chanjo. Ukiona kimya ujue kwamba bado hawajapata vigezo vya kuiidhinisha chanjo. Umeshupaza shingo mno.

5. Punguza Chuki Mkuu, ukishindwa kabisa jaribu kuzificha.
 
Nguruvi3, naona kama unazungukazunguka na hoja zilezile zisizo na misingi iNi vizurimara ya kutetea.

1. Hakuna Sayansi iliyo nje kabisa ya Human Errors. Hivyo madai yako ya kuwa una hakika wa usalama wa chanjo baada ya mwaka mmoja ni Uongo.
Hakuna mahali nimesema nina uhakika. Nipo katika record nikisema sayansi ni WIP na chanjo ni sehemu yake
Hakuna mahali nimesema mwaka mmoja, nilichosema ni kuwa matokeo ya awali yanaonyesha kupunguza tatizo
Hakuna mahali nimethibitisha mwaka mmoja, nilichosema katika kipindi cha mwaka mmoja kilichoonekana ni abc
2. Hoja ya Vita ya Kiuchumi wewe binafsi unaelewa aliyetoa hakuwa na maana hiyo unayoing'ang'ania Leo. Umekula kiapo cha Upotoshaji.
Vita ya uchumi sikusema mimi! please uliza waliosema kama wana majibu. Ninachosema hapa ni kuwa vita ya uchumi gani na watu wasioweza kujenga vyoo hadi balozi wa Japan akabidhi matundu hayo?
Vita gani ya uchumi Virus wakitafuna mapafu? Kwamba kuna virus katika mask watu wasivae ni vita ya uchumi!!!
3. Hakuna mtu amesema kila mti ni Dawa, huu ni upotoshaji mwingine. Kama unakubali zipo tiba asilia nje ya sayansi ya leo, kukataa Nyungu kisa imesemwa na mtu unayemchukia, hilo ni tatizo lako si nyungu. Nyungu zipo hata kabla haijasemwa na huyo mtu.
Ninaamini kabisa katika dawa za asili. Wamasai ni mfano mzuri sana.
Ninachohoji kwenye nyungu ni variations. Hata wamasai wana miti specific kwa maradhi specific. Hawachukui magome ya miti tu kwasababu yapo porini. Hii ni tofauti na nyungu ambapo tunaambiwa watu wachemshe majani tu yanayopatikana uani. Hapa ndipo nasema miti ni dawa lakini si kila mti ni dawa.
Kama kuna miti ya nyungu isemwe, hatuwezi kuwa na majani ya mbuzi tukasema ni dawa
Huu ujinga tumeotoa wapi? Hawa wanaotufundisha huu ujinga wana roho za aina gani?
4. Nilishasema mwanzo kuwa, Mamlaka haijaidhinisha bado au haitaidhinisha kabisa Chanjo. Ukiona kimya ujue kwamba bado hawajapata vigezo vya kuiidhinisha chanjo. Umeshupaza shingo mno.
Mamlaka itaahidhinisha nini? Dawa zinafanyaiwa tathmini maabara si katika majukwaa ya siasa
Dawa zinafanyiwa tathmini kwa kutumia data. Hapa kwetu hakuna local data, tunazotumia ni za kimataifa
Tlizuia kukusanya data ili wapotoshaji kama wewe wasema '' Mambo Poa hakuna kuvaa barakoa''

Wataalam wetu wanatathmini nini bila kuwa na data? Je tuna tatizo au hapana? Huwezi kujibu hilo bila data
Nimekuuliza tunaweza kufanya sequencing hapa Tanzania?

Haya mambo si ya kukaa vikao, ni utaalam
5. Punguza Chuki Mkuu, ukishindwa kabisa jaribu kuzificha.
chuki kusema tubadilike na tuwe sehemu ya dunia!
 
Nilikuuliza je unajua matokeo ya chanjo baada ya mwaka mmoja, Ukajibu NDIO. Unaanzaje kukana sasa?

Kujua jambo ni kuwa na Hakika nalo, kuwa na ushahidi nalo. Wewe hapa umekiri kujua Matokeo ya Chanjo baada ya mwaka mmoja, wakati huna Ushahidi nalo. Hayo ni matapishi, ukimudu yarejeshe. Chutama uanze upya.

Usitufanye tujadili MATAMANIO yako zao la Mihemko yako.

Nikikuambia wewe ni Mpotoshaji, unadhani nimekutusi. NI WAPI UNAKOTOA HOJA ZA KUWA NYUNGU INAFANYWA KWA MAJANI YOYOTE TU? Wewe ni Mpotoshaji usiyeona aibu hata kidogo. Ati unaita majani ya hovyohovyo. Sad!

Hoja ya Vita ya Uchumi inakuvua nguo kwa werevu, heri Uchutame tu. Na bado naamini unajichetua makusudi katika hilo. Too low!

Fikra za kwamba Usipofanya wafanyavyo ni kutokuwa sehemu ya dunia, ni Utumwa. Pole sana.
 
Watanzania hawafi kama yanayotokea India, Je Serikali inaficha vifo? Naona kuna wengi wanaopenda kuona Watanzania wanapoteza maisha yao kisa tu ku-prove hoja zao. Hii dunia ina mambo mengi Watanzania wanatakiwa kuwa makini hata na majirani zetu tu. Alikuwepo JK Nyerere ambaye alishindwa kukubaliana na Majirani zetu wa Kenya hadi pale alipotokea Moringe na kutoa ushauri, lakini tunaona hivi sasa jinsi Serikali inavyowakumbatia kama wao ndio wakombozi. Tuipende nchi yetu na hakuna taifa lolote lile ulimwenguni linaloweza kuwawezesha Watanzania kutoka kwenye umasikini wakati ina kila kitu.
 
Sijui kama clip hii imeishaletwa humu. Najua itakwaza baadhi yetu ama kutokana na hoja ama na mtoa hoja.

Ni kweli, tuna tia aibu kuonyesha wazi kabisa kuwa kila tunachoshariwa ama letewa na hao jamaa wa kaskazini ni salama kwetu.

====
Corona amekuja na promotor mkali kweli kweli....! Ethics za kidaktari zinakanyagwa, madaktari wenye ujuzi juu ya mambo haya wananyamazishwa. Ushuhuda upon RT.com
Watanzania hawafi kama yanayotokea India, Je Serikali inaficha vifo? Naona kuna wengi wanaopenda kuona Watanzania wanapoteza maisha yao kisa tu ku-prove hoja zao. Hii dunia ina mambo mengi Watanzania wanatakiwa kuwa makini hata na majirani zetu tu. Alikuwepo JK Nyerere ambaye alishindwa kukubaliana na Majirani zetu wa Kenya hadi pale alipotokea Moringe na kutoa ushauri, lakini tunaona hivi sasa jinsi Serikali inavyowakumbatia kama wao ndio wakombozi. Tuipende nchi yetu na hakuna taifa lolote lile ulimwenguni linaloweza kuwawezesha Watanzania kutoka kwenye umasikini wakati ina kila kitu.
 
Millions of over-50s could be given THIRD Covid jab from September | Daily Mail Online

Third Covid vaccine for millions from September: 32m over-50s, key workers and Britons with underlying health conditions could be offered a booster Covid jab in as little as two months under fresh guidance to shield most vulnerable in winter​

Millions of Britons could be offered a third Covid vaccine from September, No10's top advisers say

Figures show immunity from the jabs lasts at least six months in the 'majority' of cases, sources say

But there are fears it could wane later in the year, leaving Britain open to spiralling hospitalisations and deaths.

1625125049401.png

No10's top scientists are considering a Covid 'booster' vaccination programme from September

1625125087931.png

1625125114915.png

1625125144174.png

Rasmi: Rais SAMIA atangaza wagonjwa wapya wa CORONA: hali ni mbaya huko. tumeamua watu wachanjwe. - YouTube
 
13 Reactions
Reply
Back
Top Bottom