COVID 19 iliyotufanya tuwahudumie wapendwa wetu kama wanyama, unapitisha chakula chini ya mlango kukwepa maambukizo. Tunamshukuru Mungu

Resilience

JF-Expert Member
Jan 4, 2023
891
4,142
Tunapotafakari mwaka 2023 yatubidu kumshukuru Mungu kwamba tuliishi kama binadamu. Kuna kipindi hapo miaka ya nyuma tulikatazwa kuwazika wapendwa wetu, kuwahudumia na hata kuongea nao.

Tulikatazwa kwenda kijijini desemba kwa madai kwamba tunapeleka magonjwa, wazee wetu wakawa na hofu kubwa juu ya nafasi yetu kuwaambukiza covid 19.

Mwaka huu tumeishi kama binadamu na ndugu mmoja. Tuzidi kumwomba Mungu madhila ya 2019 to 2021 yasijirudie tena. Unampa ndugu yako huduma kwa kumrushia dawa au chakula mlangoni? It was terrible.

Tukawazika ndugu zetu usiku kwa usiku bila kupewa nafasi yakuwaaga.....wema wa Mungu ni mkubwa kwamba tupo hai na tunaishi kibinadamu.
 
Acha Kbs, Ule Mlipuko Wa Mwaka Wa Kwanza....Wagonjwa walipata Tabu Sana....
Imagine Kambi ya Wagonjwa inajengwa Porini,hakuna Maji Wala Umeme.

Akumbukwe JPM....Alipambana kuondoa hofu.!
 
Back
Top Bottom