#COVID19 Yaliyonikuta baada ya kuchomwa chanjo ya COVID-19

Mlatino Zeshalo

JF-Expert Member
Sep 10, 2014
2,016
3,462
Habari zenu wana JF

Natumai mambo yanaenda vizuri ukizingatia leo ni siku ya mapumziko kwa wengi wetu.

Niende moja kwa moja kwenye mada, tar 16 mwez huu siku ya j3 nilifanya booking online kwaajili ya kupata chanjo ya covid 19. Nilitamani sana nipate hiyo chanjo siku ya ijumaa tar 20 mwez huu. Mipango yangu ilikuwa nikipata chanjo ijumaa, jmos niende home kusikilizia reaction ya chanjo mwilini ili ikizingua niwe karibu na ndugu.

Jana tar 20 nilijiandaa na mida ya saa 6 mchana nilikuwa nimeshafika kwenye kituo nilichofanyia booking kwaajili ya kupokea chanjo. Niliwapa ref number niliyopewa siku nimefanya booking. Baada ya hapo nilienda chumba cha sindano.

Kabla sijatoa shati, niliamua kumuuliza nurse kama hiyo chanjo inasababisha homa maana nilisikia kwa watu watatu tofauti kuwa ukichoma lazima homa ikuzingue. Nurse alijibu simple tu kuwa unaweza kupata homa kidogo tu na siyo wote wanaopata homa. Akanipa mfano ambao sikuutilia maanani sana kuwa yeye hakupata homa lakini wenzake walipata.

Basi nikatoa shati akanichoma sindano, baada ya kumaliza akaniambia nenda kapumzike pale kwenye bench. Nikajiuliza sana, kwanini nipumzike? Hiyo chanjo inakipi hasa cha kunifanya nikimaliza nipumzike, badae kuna jamaa mmoja alichoma baada ya mimi kumaliza, nae aliambiwa asisimame, akae kwani angeweza kudondoka.

Nilikaa pale mapumzikoni kama dakika 15, nikasepa getto. Ilikuwa mida ya saa nane mchana. Nikaandaa chakula nikala fresh. Jioni sikuwa na mpango wa kupika, ikabidi mida ya saa moja nikatafute chakula kwenye hotel flani, nilivaa jacket maana huku kwetu mvua ilinyesha mchana wakati nipo kwenye chanjo. Nilitoka kupata chakula cha jioni saa moja na dakika 45. Basi nikazama getto kufanya mambo mengine.

Usiku saa mbili nikampigia dogo simu (anaishi na aunty Dar) nikamweleza kuwa nimekamilisha zoezi la chanjo maana baada ya kufanya booking nilimwambia pia. Dogo akacheka sana akisema mziki wake utaujutia maana aunty aliumwa baada ya kuchomwa hiyo chanjo. Mimi sikujali, tukapiga story kidogo badae nikaanza kuhisi mwili unauma kwa mbali. Kadri muda ulivyozidi kwenda hali yangu pia ikaanza kuwa mbaya. Nikamcall tena dogo kumwambia kuwa hali yangu imechange, hapo ni saa nne usiku. Akanishauri nivumilie kesho nisepe home. Basi, kidume nikalala, saa sita na dakika 15 nikashtuka, nikapiga glass ya maji then nikalala. Hapo ilibidi nijihami tu kuwa na maji karibu labda yangesaidia chochote. Saa saba pia na dakika 28 nikaamka tena, nikanywa maji alaf nikaenda kukojoa, lakini muda huu hali ilikuwa mbaya sana maana nilianza kutetemeka sana. Ikabidi nivae full, huwa napenda kulala na boxer. Nikavaa soksi ndefu, pensi, tshirt na jacket. Nilipolala nikajifunika shuka na duvet kwa juu. Asee niliendelea kutetemeka hadi nikahisi hilo duvet halina maana. Wakati huo kichwa kinauma balaa, alafu mwili wote kuanzia miguuni hadi shingo vilikuwa hoi.

Nikajikaza huku nikisali maana nilijua asubuhibikifika ntaenda kulazwa. Ndani ninazo diclopa za maumivu lakini sikutaka kutumia maana sijui ingekuwaje. Nikalala hadi saa nane na nusu nikashtuka tena, nikanywa maji then nikauchapa. Saa tisa nikaamka tena hapo nilikuwa nahisi baridi imekata, nikavua soksi maana nilikuwa nahisi miguu imechemka sana, poa nikavua jacket.

Nikalala lakuni bado nilijifunika shuka na duvet. Asubuhi leo nimeshtuka saa tatu, nikaenda nje kuota jua kidogo then nikarudi ndani. Nikawa nahisi homa imepungua japo kichwa kinauma kwa mbali. Saa tano asubuhi nikachukua maji ya mvua, ya baridi sana nikaoga. Asee nilihisi raha sana maana mwili umwkuwa fit japo maumivu ya kichwa bado nayahisi.

Sijajua kwa wengine waliopata hii chanjo kama na wao wamepitia hii changamoto maana daah, usiku nimehangaika hadi kufikia muda nikajuta kuchomwa hiyo chanjo. Nimepatwa maswali mengi kichwani, kwamba, ni kweli hawa viongozi wamechoma hii chanjo? Mbona wao walikuwa fit tu, au wao afya zao ni bora zaidi?

Lakini namshukuru Mungu, maana naendelea vema japo kichwa ndio bado kinauma kwa mbali. Jioni ntaenda uwanjani nikajaribu kufanya mazoezi kidogo maana miguu usiku pia ilizingua sana hadi nikahisi nitaamka nikiwa nimepooza.
 
Miye nimechoma ila usiku wake nilisikia baridi sana nikajifunika duvet, asubuhi nikaamka shwari na niko poa.
Hongera, mimi duvet lilikuwa limezidiwa na baridi, pamoja na kuvaa jacket, nikatanguliza shuka na duvet juu. Hata safari ya home nimeipiga chini maana siwez panda bus na hii hali
 
HIyo ni ya papo kwa papo na ni kawaida kwa chanjo nyingi. Subiri kwanza kama utakuwa na uwezo wa kuzalisha. Subiri baada ya miaka 2 uone kama tabia yako itabaki kuwa kawaida na binadamu wengine. Zaidi ya yote subiri uzae watoto kama watakuwa ni biandamu wa kawaida. Kinga yako y amwili kuweza kupambana na magonjwa unayoweza kuyashinda leo bila kutibiwa kama mafua n.k. Lakini pia aina ya watoto utaozaa, na hasa wakiwa wakubwa , tathmin iuwezo wao katika mambo anuai kuanzia kichwa.

Kuna yasiyozungumziwa:-

Nyie kwa kuwa mmeamua kuwa panya wa maabara, muwe tu tayari kisaikolojia kwa lolote lile. Maabara kuna mengi!.
 
Habari zenu wana jf. Natumai mambo yanaenda vizuri ukizingatia leo ni siku ya mapumziko kwa wengi wetu.

Niende moja kwa moja kwenye mada, tar 16 mwez huu siku ya j3 nilifanya booking online kwaajili ya kupata chanjo ya covid 19. Nilitamani sana nipate hiyo chanjo siku ya ijumaa tar 20 mwez huu. Mipango yangu ilikuwa nikipata chanjo ijumaa, jmos niende home kusikilizia reaction ya chanjo mwilini ili ikizingua niwe karibu na ndugu.

Jana tar 20 nilijiandaa na mida ya saa 6 mchana nilikuwa nimeshafika kwenye kituo nilichofanyia booking kwaajili ya kupokea chanjo. Niliwapa ref number niliyopewa siku nimefanya booking. Baada ya hapo nilienda chumba cha sindano.

Kabla sijatoa shati, niliamua kumuuliza nurse kama hiyo chanjo inasababisha homa maana nilisikia kwa watu watatu tofauti kuwa ukichoma lazima homa ikuzingue. Nurse alijibu simple tu kuwa unaweza kupata homa kidogo tu na siyo wote wanaopata homa. Akanipa mfano ambao sikuutilia maanani sana kuwa yeye hakupata homa lakini wenzake walipata.

Basi nikatoa shati akanichoma sindano, baada ya kumaliza akaniambia nenda kapumzike pale kwenye bench. Nikajiuliza sana, kwanini nipumzike? Hiyo chanjo inakipi hasa cha kunifanya nikimaliza nipumzike, badae kuna jamaa mmoja alichoma baada ya mimi kumaliza, nae aliambiwa asisimame, akae kwani angeweza kudondoka.

Nilikaa pale mapumzikoni kama dakika 15, nikasepa getto. Ilikuwa mida ya saa nane mchana. Nikaandaa chakula nikala fresh. Jioni sikuwa na mpango wa kupika, ikabidi mida ya saa moja nikatafute chakula kwenye hotel flani, nilivaa jacket maana huku kwetu mvua ilinyesha mchana wakati nipo kwenye chanjo. Nilitoka kupata chakula cha jioni saa moja na dakika 45. Basi nikazama getto kufanya mambo mengine.

Usiku saa mbili nikampigia dogo simu(anaishi na aunty dar) nikamweleza kuwa nimekamilisha zoezi la chanjo maana baada ya kufanya booking nilimwambia pia. Dogo akacheka sana akisema mziki wake utaujutia maana aunty aliumwa baada ya kuchomwa hiyo chanjo. Mimi sikujali, tukapiga story kidogo badae nikaanza kuhisi mwili unauma kwa mbali. Kadri muda ulivyozidi kwenda hali yangu pia ikaanza kuwa mbaya. Nikamcall tena dogo kumwambia kuwa hali yangu imechange, hapo ni saa nne usiku. Akanishauri nivumilie kesho nisepe home. Basi, kidume nikalala, saa sita na dakika 15 nikashtuka, nikapiga glass ya maji then nikalala. Hapo ilibidi nijihami tu kuwa na maji karibu labda yangesaidia chochote. Saa saba pia na dakika 28 nikaamka tena, nikanywa maji alaf nikaenda kukojoa, lakini muda huu hali ilikuwa mbaya sana maana nilianza kutetemeka sana. Ikabidi nivae full, huwa napenda kulala na boxer. Nikavaa soksi ndefu, pensi, tshirt na jacket. Nilipolala nikajifunika shuka na duvet kwa juu. Asee niliendelea kutetemeka hadi nikahisi hilo duvet halina maana. Wakati huo kichwa kinauma balaa, alafu mwili wote kuanzia miguuni hadi shingo vilikuwa hoi.

Nikajikaza huku nikisali maana nilijua asubuhibikifika ntaenda kulazwa. Ndani ninazo diclopa za maumivu lakini sikutaka kutumia maana sijui ingekuwaje. Nikalala hadi saa nane na nusu nikashtuka tena, nikanywa maji then nikauchapa. Saa tisa nikaamka tena hapo nilikuwa nahisi baridi imekata, nikavua soksi maana nilikuwa nahisi miguu imechemka sana, poa nikavua jacket.

Nikalala lakuni bado nilijifunika shuka na duvet. Asubuhi leo nimeshtuka saa tatu, nikaenda nje kuota jua kidogo then nikarudi ndani. Nikawa nahisi homa imepungua japo kichwa kinauma kwa mbali. Saa tano asubuhi nikachukua maji ya mvua, ya baridi sana nikaoga. Asee nilihisi raha sana maana mwili umwkuwa fit japo maumivu ya kichwa bado nayahisi.

Sijajua kwa wengine waliopata hii chanjo kama na wao wamepitia hii changamoto maana daah, usiku nimehangaika hadi kufikia muda nikajuta kuchomwa hiyo chanjo. Nimepatwa maswali mengi kichwani, kwamba, ni kweli hawa viongozi wamechoma hii chanjo? Mbona wao walikuwa fit tu, au wao afya zao ni bora zaidi?

Lakini namshukuru Mungu, maana naendelea vema japo kichwa ndio bado kinauma kwa mbali. Jioni ntaenda uwanjani nikajaribu kufanya mazoezi kidogo maana miguu usiku pia ilizingua sana hadi nikahisi nitaamka nikiwa nimepooza.
Mimi tulienda wawili kuchoma mimi sikupata shida mwenzangu kichwaa kiliuma usiku kucha baridi kutetemeka na kutoka jasho ilikua jumatano ila leo ni mzima.
 
HIyo ni ya papo kwa papo na ni kawaida kwa chanjo nyingi. Subiri kwanza kama utakuwa na uwezo wa kuzalisha. Subiri baada ya miaka 2 uone kama tabia yako itabaki kuwa kawaida na binadamu wengine. Zaidi ya yote subiri uzae watoto kama watakuwa ni biandamu wa kawaida. Maan kuna uwezekano mkubwa waliochanjwa hii chanjo kuanza kuzaa:-
Hayo hata sijali sana. Hata nikiwa na tabia kama mbuzi maana tutakuwa wengi tu. Afu mimi nitakuwa mbuzi dume
 
Duh!
Mbona Mimi nimechoma tarehe 13 August na sijahisi chochote Cha ajabu zaodi ya kaganzi flani kwa mbaali kwenye bega pale nilipochomea sindano ambayo ilidumu kama siku tatu au nne tu ikapotea na mpaka sasahivi Niko fiti na hata siku niliyochoma hiyo chanjo kazi nzito za kutumia nguvu nilikuwa nafanya Kama kawaida.
Anyway Kama ni kweli Basi pole Sana na hongera kwa uamuzi wa kupata chanjo.
 
Asante
 
Kwani hao viongozi unataka nao mkuu wakiumwa homa na kutetemeka usiku kwenye maduveti yao pia wakwambie?

Chanjo zote duniani huwa hivi. Ni lazima mwili u react ukichoma chanjo. Umewahi kuchoma chanjo gani ingine ukiwa mkubwa? Umewahi choma ya hepatitis? Yellow fever? Ya mafua? Na zote tu huwa hivyo. Na ungekuwa mzazi utakumbuka kuwa watoto wachanga wakichomaga chanjo za aina mbali mbali huwa zinawaletea homa siku chache za kufuatia na huwa wanalia sana tu
 
HIyo ni ya papo kwa papo na ni kawaida kwa chanjo nyingi. Subiri kwanza kama utakuwa na uwezo wa kuzalisha. Subiri baada ya miaka 2 uone kama tabia yako itabaki kuwa kawaida na binadamu wengine. Zaidi ya yote subiri uzae watoto kama watakuwa ni biandamu wa kawaida. Maan kuna uwezekano mkubwa waliochanjwa hii chanjo kuanza kuzaa:-
🤡🤡🤡
 
Wote mkilala nd mna umwa itabidi nichome usiku afu nione kama taumwa mchana
 
HIyo ni ya papo kwa papo na ni kawaida kwa chanjo nyingi. Subiri kwanza kama utakuwa na uwezo wa kuzalisha. Subiri baada ya miaka 2 uone kama tabia yako itabaki kuwa kawaida na binadamu wengine. Zaidi ya yote subiri uzae watoto kama watakuwa ni biandamu wa kawaida. Maan kuna uwezekano mkubwa waliochanjwa hii chanjo kuanza kuzaa:-
Mapimbi na misukule ya Gwaji boy bado mpoo kumbe?
 
Ho
Hongera, mimi duvet lilikuwa limezidiwa na baridi, pamoja na kuvaa jacket, nikatanguliza shuka na duvet juu. Hata safari ya home nimeipiga chini maana siwez panda bus na hii hali
Hongera kwa kupata chanjo na pole kwa hayo maudhi madogomadogo
 
Hongera, mimi duvet lilikuwa limezidiwa na baridi, pamoja na kuvaa jacket, nikatanguliza shuka na duvet juu. Hata safari ya home nimeipiga chini maana siwez panda bus na hii hali
Pole.miye tulienda na Bi mkubwa lkn yeye hakupa wala kujisikia chochote.Ila miye baridi aise km vile nimepita mafinga alafu basi liwe na kitundu inanavyopenya.
 
Back
Top Bottom