Ikawa hivi....
"Huyo First Lady1 ni nani kwani".. mtu kaulizwa
"Ah.. ni mwanachama mmoja wa huko JF".. akajibiwa
"Mbona watu wanawachombeza sana na kuwafanya couple" mtu anandelea kudadisi
"Ah wanatania tu si unajua tena mambo ya mtandao". Anajibiwa kama kwa kupuuzia
"Umewahi kuwasiliana naye" mtu haachii anaendelea. Hapa inabidi utafute jibu zuri.
"Hapana.." kama kwa kigugumizi.
"Unamtaka eh.. kama unamtaka si useme tu" kwa sauti ya juu mtu wa watu anaanza kupandisha.
"Jamani hunny! mbona una wivu hata kwa avatar" anaambiwa kama kwa kukofokewa.
"Yaani, unanifanya miye sijui.. naona jinsi watu wanavyokuchombezea.. na wengine sijui kina Pearl, Queenkami, na nani wote ungekuwa na uwezo ungewabeba wewe.. mwanaharamu mkubwa. Kama hunitaki nipe talaka yangu nirudi kwetu. Huwezi kuninyanyasa mimi na sijui kina nani hao"..
Mara jambo likazua jambo ngumi teke. Kaanza kulia.. kakimbia chumbani anaanza kufungasha.. nasimama mbali naangalia monitor kurasa zinavyozidi kujaa...