Coronavirus: Tanzania bila lockdown tutakufa tuishe

Coronavirus: Tanzania bila lockdown tutakufa tuishe

Habari njema kwa majiji ya Roma, Madrid, New York, taarifa za leo zimeonyesha maambukizi na vifo kutokana na Covid 19 umepungua.

Na hii imetokana na lockdown katika majiji hayo pia na maeneo mbalimbali ya nchi hizo Italia, Spain na USA, hata kule Wuhan bila lockdown corona isingeisha.

Kuna kauli zinatumika na viongozi wa Tanzania kuwa hawawezi kutumia mbinu za mataifa yaliyoendelea kudhibiti Corona kwa kuwa Watanzania wengi ni masikini.

Na kauli hii inaungwa mkono na viongozi wa serikali, chama tawala na upinzani lakini.

Huko Uturuki Rais wa nchi hiyo alisema wananchi wachape kazi lakini kilichoripotiwa leo na madaktari wakinukuliwa na vyombo vya habari ni kuwa maambukizi katika taifa hilo yanaenda kwa kasi zaidi ilivyokuwa China, Italy, Spain na USA, yaani kiwango cha maambukizi huko Uturuki kinatisha.

Kule Brazil hivyo hivyo, tukija hapa Bongo unaambiwa lockdown haitawezekana, hebu tupeni mbinu mbadala ambayo mnafikiria kuwa inaweza kuzuia maambukizi, maana nahisi wiki mbili zijazo tutakuwa tunaongea lugha moja.

Kula USA mpaka chui ameambukizwa korona, huku kwetu mbwa, paka na ng'ombe wasipo ambukizwa tumuombe Mungu.

Sent using Jamii Forums mobile app
Screenshot_20200405-022845.png
 
Rebeca 83, Wewe unayo hela ya kununua chakula, unajua ni watu wangapi hawana pesa ya kununua chakula hata kwa siku mbili? Unataka tuanze kuvamiwa majumbani watu kuja kuiba chakula? Unadhani utakuwa salama ukiwa na chakula ndani na majority hawana? Haya mambo ni ya wenye akili tu. Kinachotakiwa kufanyika ni partial lock down na sio full lockdown. Wazuie safari kutoka mkoa kwenda mkoa na kutoka wilaya kwenda wilaya

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Corona sio gonjwa kubwa kama tunavyolichukulia.

Yaani kwenye watu 200
wanaokufa 8
Wanaopona 150
wanaokuwa mahututi 42.
Cha mtoto.
Narudia tena Cha mtoto.

Tena kwenye hao 8
Wazee 6
Vijana lakini waliokuwa na matatizo yao hapo kabla 2.

Sasa kwanini tunaogofya sana.


Mwenye kupiga anyooshe kidole juu.
 
  • Thanks
Reactions: UCD
Rebeca 83,
Unaposema atoke tu anapokwenda kununua mahitaji ya muhimu una maana huyo mtu atakuwa anapesa ametunza hapo nyumbani kwake? Hivi wewe dada unajua kuwa kuna watu lazima watoke wakahemee ndiyo wapate pesa za matumizi? Wewe inaonekana kama siyo kula kulala basi unakazi ambayo inakulipa bila kufanyakazi. Fikiria maisha ya Kiafrika acha kufikiria maisha ya kizungu ambapo anaweza akakaa home lakini bado akaendelea kufanyabiashara na kusupply bidhaa zake through mtandao ambapo hapa TZ haiwezekani. Think out of the box!!
 
Watanzania walio wengi karibia 70% hawana uwezo hata wa kusave 10kg tu ya sembe,washazoea watoke ndio wale.

Hebu fikiria wamachinga,wauza mboga za majani,wauza kahawa,Shoes shiner,vibarua kwa wahindi,walinzi,madereva wa daladala,mama ntilie,madogo wanaoshinda barabarani wakiuza pipi na maji ,wakina mama mtaani wanaouza maandazi,vitumbua nk watakuwa na hali gani ukiwaambia nchi inaenda total lockdown.

Sijajua umekulia wapi lkn kwa sisi tulikulia kwenye life ya kawaida tunajua,kuna watu wengi leo wanaishi kwa HISANI YA MIKOPO YA KIDUKA CHA MANGI,kila siku jina lake halikauki KWENYE DAFTARI LA MANGI.Anamka asubuhi hela hana anaenda kwa Mangi na kumwambie awapatie nyumbani kilo moja ya Maharage na Kilo Moja ya unga akirudi kwenye mihangaiko atalipa,lkn vilevile anaweza akaenda akirudi hana kitu akienda kwa MANGI anaunga deni.Acheni kabisa kuna watu wana hali mbaya,MANAKE UNAWEZA UKAZUIA CIRONA lkn MWISHO WA SIKU UKAWAUA WATU WENGI KWA NJAA zaidi ya hata hiyo Corona.

India,Kenya,South Africa hii Total Lockdown yao ishafeli,watu India sasa wanapigana na polisi,wewe pata picha India watu karibia 1bilion kula yao ya shida alafu uwaweke total lockdown,sasa kuna maeneo India raia wanapigana na polisi na sio kama wanapenda bali NJAA ,MSIFANYE MASIHALA NA NJAA.

Cha msingi tufuate ushauri wa Daktari na wataalamu wetu,tufanye vitu kutokana na uwezo wetu na si kuiga na tusilete siasa ktk hili swala.
 
  • Nzuri
Reactions: UCD
lockdown sio kwamba kila mtu atabaki ndani,ila kupunguza maambukizi wale ambao is necessary kutoka kama wauguzi then itabidi watoke,kuna kundi la watu tutawapoteza ili kulinda WENGI ..hii ndio kanuni behind lockdown, again lockdown ni kipindi tuu..ambacho serikali husika kabla ya kuimpose wanaweigh the risks and everything....vyote vinakua calculated..either tupoteze watu 1000 kwa njaa ama tupoteze 10,000 kwa corona. Nyie mnaosema sijui mahitaji inabidi mfanye kazi..mtashindia uji pale utakapoona familia yako inapukutika kama majani. New York ma Mogul yamejaaaaaaaaaaaa….naona mna underestimate corona eeh..
Wewe kwa vile una uwezo wa kukaa ndani na kupata Chakula ndio maana unashadadia lockdown ili wenzio wafe kwa njaa. Mi nasema lockdown isiwepo Kwa sababu ninadhani ni zaidi ya watanzania milioni ishirini wanategemea mlo wa siku kwa kutoka nje. Siwezi kubali wote hawa wafe. Heri Corona isambae tubaki na natural selection, the weak will perish and the strong will survive. Who will survive and who will die, this belongs to The Almighty GOD. Sasa kwa vile wewe una uwezo basi unataka watu wafungiwe ili wafe wewe usalimike, to me that's big no, kila maamuzi unayofanya wafikirie na wengine. You need to view things at different angles and see things from humanity point of view

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Tanzania na nchi nyingi za Africa hata tukiweka lockdown ya miaka saba, kama ni kufa tutakufa tu, tumshukuru Mungu anatulinda sana kwa kweli na ndiye atatutetea

Sent using Jamii Forums mobile app
 
  • Thanks
Reactions: UCD
Stephen Chelu,
Wewe ndio unaweka emotions, mimi siishi New York, sijui kwa nini umeling’ania neno njaa... hii inaonyesha unataka tusijadili objectively..anyway lockdown unaweza kusave 7000 na wengine 3,000 kufa, sasa wewe unaepinga lockdown ndio uje na ‘ executable viable plan’ itakayisave MASS?!?
 
Hakika mkuu, watu wasijifanyevwanajali sana katika hili. Kama wao matajiri wanaona lockdown ni suluhisho wajifungie ndani na sisi masikini tusioweza kumudu wacha tutoke tukafe na corona na baada ya hapo wataishi maisha mazuri kwa kuwa tanzania haitakuwa na masikini tena hivyo itapaa kiuchumi. Mbona ni rahisi tu.
Kweli kabisa mkuu

Sent using Jamii Forums mobile app
 
No mkuu,watoe kodi kwa wanaouza mazao..

Sijui kama hata tuna staticians..na kama wapo je hawako influenced na serikali..(kutokua na bias),

Otherwise tungejua rate ya wanaoumwa sasa hivi na baada ya kuweka kipindi maalumu cha lockdown..may be 8 weeks, then tuna evaluate kama lockdown imesaidia kupunguza maambukizi bila athari nyingine..baada ya hapo ndio tutajua kama tuendeleee na lockdown...ama sivyo
😂😂😂😂😂😂
Tupige lockfown ya wiki nane halafu tufikiri kama tuendelee ama la! Kirahisi hivyo.
This shit ain't a video game that anything you want can happen with just a press of a button.
 
Hapana, Serikali CCM isiweke Lockdown yoyote .


watu watakufa nanjaa...Serikali sidhan km wanaweza kutoa fungu Ku support maisha ya watu.
 
Tunapenda last minute rush na kulaumiana dakika za mwisho... Tunita zima moto...

Nisingependa tufikie kwenye total lockdown...


Cc: mahondaw
 
Wewe kwa vile una uwezo wa kukaa ndani na kupata Chakula ndio maana unashadadia lockdown ili wenzio wafe kwa njaa. Ni nasema lockdown isiwepo Kwa sababu ni zaidi ya watanzania milioni ishirini wanategemea mlo wa siku kwa kutoka nje. Siwezi kubali wote hawa wafe. Heri Corona isambae tubaki na natural selection, the weak will perish and the strong will survive. Who will survive and who will die, this belongs to The Almighty GOD. Sasa kwa vile una uwezo basi unataka watu wafungiwe ili wafe wewe usalimike, to me that's big no, kila maamuzi unayofanya wafikirie na wengine. You need to view things at different angles and see things from humanitarian point of view

Sent using Jamii Forums mobile app

Nimewaeleza pale juu, unapima wangapi watakufa na njaa na wangapi watakufa kwa corona , Kisha unamake decisions!!? Mmeng’ania njaa mbona kabla hata corona haijaja kuna watu walikua wanalala na njaa,

Kama una support natural selection na unajua some people will die kwenye corona no matter what kwa nini sasa unapinga lockdown??? Au wewe kifo cha corona kinakutisha zaidi kuliko kifo cha njaa??
 
Wewe ndio unaweka emotions, mimi siishi New York, sijui kwa nini umeling’ania neno njaa... hii inaonyesha unataka tusijadili objectively..anyway lockdown unaweza kusave 7000 na wengine 3,000 kufa, sasa wewe unaepinga lockdown ndio uje na ‘ executable viable plan’ itakayisave MASS?!?
Ni hivi.
1. Watu waendelee kufuata ushauri wa wataalamu wa afya kuhusu taratibu za usafi.
2. Kufunga safari za mkoa mmoja kwenda mkoa mwingine, ni mizigo pekee iruhusiwe kuvuka mipaka ya mikoa.
3. Tuache kanuni ya asili ifanye kazi, corona ije watakaoondoka wawasalimie huko na watakao baki wafute machozi na wakomae kiume kuendelea na maisha.

Wewe kama unaona lockdown ni suluhisho jifungie wewe na familia yako.
 
Back
Top Bottom