Hakuna lockdown, Basi tuonyesheni mipango

Ramark

JF-Expert Member
May 19, 2015
1,989
1,440
Wana jamvi

Nilitamani niandike haya maoni yangu mapema wiki hii ya kwanza ya paska lakini nashukuru Leo nimeandika.

Maambukizi yanaendelea kupaa kwa kasi tofauti na mtazamo WA awali licha ya waziri Ummy kueleza maambukizi ya ndani yameanza lkn hakutuonyesha mipango madhubuti.

Pia waziri Mkuu alipoongea ikulu ya DDM bado hakuonyesha mbinu wezeshi na nyongeza ktk kukabiliana na hali hii.

Lockdown kwa dunia yote ilionekana na njia madhubuti ya kukabiliana na maambukizi ya ndani lkn hapa kwetu si madhubuti.

Wengi tulifikiri na kuomba lockdown kama sehemu ya kujisalimisha kuwa hatutaki kuugua. Pia zuio LA kutotoka ndani nalo tuliona linafaa lkn serikali na bunge haionyeshi kujali mawazo ya umma.

Lockdown na curfew ni njia madhubuti hasa kwenye nchi zenye mifumo mibovu ya kiafya.

Kama hatuitaji kufunga mipaka ya miji na majiji vilevile zuio LA kutotoka nje kwa kigezo cha umaskini WA Tanzania, biashara na mazoea ya umma basi serikali tuonyesheni mipango.

Tunataka kuona mipango madhubuti ya nyongeza ktk kukabiliana na maradhi ya corona ya 2019 tofauti na hizi zinazoendelea; tunaomba haya kwa kuwa hamtaki kutufungia ndani na mipaka kwani hamtaki inawezekana kugawa chakula, kutoa posho, kutikisa biashara na uchumi ili kuhifadhi mwenendo WA mapato ya umma.

Hapo awali tuliwahi kumsikia wazir Mpango akiwaelekeza BOT kufanya tathimini ya uchumi na corona lkn hatujapata majibu.

Bunge linaendelea lkn hatujasikia msimamo WA bunge au wabunge wakitaka mipango ya kukabiliana na corona katika afya na uchumi WA watu na Taifa. Bajeti zinaendelea lkn si bunge Walioitaka wizara au wazir kurevise budget yao kutokana na mtikiso WA uchumi uliopo duniani kwani fedha za misaada na ruzuku zinaweza kupungua au kutowepo hivyo ofisi za umma zingeanza kupunguza matumizi na kuelekeza fedha hizo kwenye kuimarisha uchumi na miradi ya maendeleo au binge linakwenda kupitisha bajeti ambayo mwakani tunalaumiana kwa utekelezaji wake? Si muda wa viongozi wetu kuwa realistic?

Tunatamani tuone mipango ya kuimarisha kwelikweli kipato na uchumi WA sekta binafsi kwani tunaamini wameathirika. Marekani wameshapitisha bajeti hiyo na sisi hatuoni haja hiyo kwani tunabenki kuu, mfuko WA hazina na sheria ya fedha za dharura na katiba inaruhusu.

Wanajf wengi walishatoa na wanaendelea kutoa mapendekezo yao ni vema mkuu wa nchi na wa kila muhimili kuonyesha mahitaji ya kuinusuru nchi yetu kwani tunajua roho zetu si muhimu kuliko uchumi wetu na siasa yetu.

Naomba niishie hapo

Karibuni, tuendelee
 
Kuna thread humu ndani nilliona mchana ikimdhihaki Rais kuwa "Asante Magufuli kwa kutuvusha kwenye Corona"! Aliyeandika ni Mwana CCM au ni MTU mwenye mrengo huo! Nilisiikitika sana maana gonjwa linazidi na kuna Wapuuzi wanamdhihaki Rais wakidhani wanamsifia.

Kwa hali ilivyo, nawasihi nyote ndugu zangu, tusimame kwa pamoja, watakaokufa sio wana CCM au CHADEMA! Ni Watanzania, ni ndugu zetu, kwanini tusiungane? Kwanini tusiheshimu mawazo ya hao tunaowaita Wapinzani waliotumwa na Mabeberu?

Inaumiza na inakera sana Mwenyezi Mungu atusaidie. Tumeshachelewa kuchukua hatua na tunafanya utani, tutakwisha! Wala hatutishani. Afya zenyewe mgogoro kisha tunaleta siasa. Narudia, kama hatutakuwa serious, tutakwisha.
 
Mipango ni kutoka na kwenda kuchapa kazi huku bank zikifanya kazi hadi saa mbili usiku ili serikali ikusanye Kodi Hii serikali niya pesa Kama inaongozwa na mchaga vile
 
Hili ndilo swali Bora la mwezi huu!!!!
Kati ya maswali magumu ambayo serikali hii inatakiwa kujibu ni hili.....

Asante Sana mtoa mada
 
Niliwahi mwambia mdogo wangu wakike miaka ya nyuma, gauni halijakupendeza, akanuna na kutoka hivyo hivyo, kufika alikokuwa anaenda mashoga zake wakamuuliza vipi shosti hukutokea home nini? akawauliza kwann? wakamjibu mbona upo normal sana hujadamshi. Akaelewa kuwa ni kweli hakuwa amependeza, aliporudi akaniambia. Nikanyamaza.

Siku nyingine akanifuata na mchoro wa gauni anataka akashone, nikamwambia huu umekaa kibibi sasa, ngoja nikutafutie mshono online, hakungoja, huyooo kwa fundi, baada ya wiki akarudi na gauni lake, kulivaa, mama akamwambia loooooooo yaani kitenge kizuri umeenda kukiharibu mwanangu, ndo umeshona kituko gani hicho. Akaniangalia, nikafumba macho.

Kuanzia siku hiyo, akawa akija na jambo lake, mi naunga mkono hoja tu, mpaka akajua kuwa bro hana time tena na mimi, akaamua kujishusha na kuacha ujuaji, ikawa akiomba ushauri kama yupo sahihi namwambia, kama kabugi namwambia na anachukua ushauri.

So tuendelee kujikinga wenyewe mpaka hapo watakapoona kuwa sisi nasi watu sio mifugo.
 
Marekani imewashinda wanawaza kuachia watu wafanye kazi.

Sasa Tz mtakuwa mnaokota watu barabarani waliokufa kwa njaa na vipigo vya polisi.

Sent using Jamii Forums mobile app
Uhispania wanarejea kazini, vilevile Italy na marekani baada ya muda.
Fuatilia hatua wanazozichukua.

China hata Korea waliofanya Jana (Leo) uchaguzi ukiangalia watu wanavyofanya kazi
Hakuna kunawa kwa maji tiririka Bali disposable gloves, barakoa, suits za kuzuia maambukizi, 1metre ya ukweli, 2 metres ya ukweli kwa walioko karantini pamoja na GPS je sisi tuko vipi sasa?

Kanisani, misikitini, masoko, kazini, wanahabari (mic) kila mtu kila mahali bila kuisanitazer na hata ukiisanitaZer inafasi ndani zinazotunza mate ambayo yanaweza kuvutwa na pua, vituo na magari ya umma pia binafsi, uhuduma za umma n.k bado yako mengi yaliyo loose
 
Niliwahi mwambia mdogo wangu wakike miaka ya nyuma, gauni halijakupendeza, akanuna na kutoka hivyo hivyo, kufika alikokuwa anaenda mashoga zake wakamuuliza vipi shosti hukutokea home nini? akawauliza kwann? wakamjibu mbona upo normal sana hujadamshi. Akaelewa kuwa ni kweli hakuwa amependeza, aliporudi akaniambia. Nikanyamaza.

Siku nyingine akanifuata na mchoro wa gauni anataka akashone, nikamwambia huu umekaa kibibi sasa, ngoja nikutafutie mshono online, hakungoja, huyooo kwa fundi, baada ya wiki akarudi na gauni lake, kulivaa, mama akamwambia loooooooo yaani kitenge kizuri umeenda kukiharibu mwanangu, ndo umeshona kituko gani hicho. Akaniangalia, nikafumba macho.

Kuanzia siku hiyo, akawa akija na jambo lake, mi naunga mkono hoja tu, mpaka akajua kuwa bro hana time tena na mimi, akaamua kujishusha na kuacha ujuaji, ikawa akiomba ushauri kama yupo sahihi namwambia, kama kabugi namwambia na anachukua ushauri.

So tuendelee kujikinga wenyewe mpaka hapo watakapoona kuwa sisi nasi watu sio mifugo.
Hawawez omba ushauri isipokuwa kulazimisha Nguvu ya umma isikike.
Wachambue maoni ya wapinzani, umma na ya kwao KISHA walete mipango.
Si lazima waige
 
Nashauri viongozi wauambie umma wote pamoja na kunawa mikono na kutokuwa na misongamano
Wote tuvae mask muda wote

Na zigawiwe kwa wingi

Mana lockdown yaonekana ni impossible watu watakufa njaa

Mask na gloves
 
Makanisa pia mnaweza weka mipango bila kusubiri matamko ya watawala

Kanisa katoliki hivi karibuni wameweka masharti ya kusherekea madhehebu ya misa na sakrament zake ni vema kutazama je, kuna haja ya mamia kuwa kanisani kila jumapili?

Si vema kuendelea kusubiri serikali itoe tamko, nanyi toeni maamuzi kwa waamini wenu.
Mabenchi bado yamejazana, wanakwaya wanaendelea kupumuliana kwa kigezo cha kufundishana mazoezi achilia uimbaji kanisani. Ni vema litoke tamko kuwa watoto hapana, wazee hapana, wajawazito hapana, kwaya zisimame kwa sasa, awepo mmoja anayeongoza nyimbo then waumini kuitikia au kuimba mwenyewe.
Mic inaambukiza hivyo kutumia wengi haifai hivyo tofaut na mapadri ambao ni familia wengine ni mmoja tu aruhusiwe kusoma masomo, na matangazo.
Mita moja izingatiwe kweli ikiwezekana benchi moja livukwe kila baada ya kukaa benchi husika, wahudumu hasa dar kila kanisa wanunuliwe suits za kuzuia maambukizi na kupima joto la mwili.
Ministrant wapumzishwe kwa sasa au atumike mmoja( chetezo kinaweza punguzwa kwa sasa)

Sadaka, masunduku yawe wazi lkn watu wavae barakoa wote wanaoingia kanisani kasoro makundi yaliyopumzishwa.
 
Wana jamvi

Nilitamani niandike haya maoni yangu mapema wiki hii ya kwanza ya paska lakini nashukuru Leo nimeandika.

Maambukizi yanaendelea kupaa kwa kasi tofauti na mtazamo WA awali licha ya waziri Ummy kueleza maambukizi ya ndani yameanza lkn hakutuonyesha mipango madhubuti.

Pia waziri Mkuu alipoongea ikulu ya DDM bado hakuonyesha mbinu wezeshi na nyongeza ktk kukabiliana na hali hii.

Lockdown kwa dunia yote ilionekana na njia madhubuti ya kukabiliana na maambukizi ya ndani lkn hapa kwetu si madhubuti.

Wengi tulifikiri na kuomba lockdown kama sehemu ya kujisalimisha kuwa hatutaki kuugua. Pia zuio LA kutotoka ndani nalo tuliona linafaa lkn serikali na bunge haionyeshi kujali mawazo ya umma.

Lockdown na curfew ni njia madhubuti hasa kwenye nchi zenye mifumo mibovu ya kiafya.

Kama hatuitaji kufunga mipaka ya miji na majiji vilevile zuio LA kutotoka nje kwa kigezo cha umaskini WA Tanzania, biashara na mazoea ya umma basi serikali tuonyesheni mipango.

Tunataka kuona mipango madhubuti ya nyongeza ktk kukabiliana na maradhi ya corona ya 2019 tofauti na hizi zinazoendelea; tunaomba haya kwa kuwa hamtaki kutufungia ndani na mipaka kwani hamtaki inawezekana kugawa chakula, kutoa posho, kutikisa biashara na uchumi ili kuhifadhi mwenendo WA mapato ya umma.

Hapo awali tuliwahi kumsikia wazir Mpango akiwaelekeza BOT kufanya tathimini ya uchumi na corona lkn hatujapata majibu.

Bunge linaendelea lkn hatujasikia msimamo WA bunge au wabunge wakitaka mipango ya kukabiliana na corona katika afya na uchumi WA watu na Taifa. Bajeti zinaendelea lkn si bunge Walioitaka wizara au wazir kurevise budget yao kutokana na mtikiso WA uchumi uliopo duniani kwani fedha za misaada na ruzuku zinaweza kupungua au kutowepo hivyo ofisi za umma zingeanza kupunguza matumizi na kuelekeza fedha hizo kwenye kuimarisha uchumi na miradi ya maendeleo au binge linakwenda kupitisha bajeti ambayo mwakani tunalaumiana kwa utekelezaji wake? Si muda wa viongozi wetu kuwa realistic?

Tunatamani tuone mipango ya kuimarisha kwelikweli kipato na uchumi WA sekta binafsi kwani tunaamini wameathirika. Marekani wameshapitisha bajeti hiyo na sisi hatuoni haja hiyo kwani tunabenki kuu, mfuko WA hazina na sheria ya fedha za dharura na katiba inaruhusu.

Wanajf wengi walishatoa na wanaendelea kutoa mapendekezo yao ni vema mkuu wa nchi na wa kila muhimili kuonyesha mahitaji ya kuinusuru nchi yetu kwani tunajua roho zetu si muhimu kuliko uchumi wetu na siasa yetu.

Naomba niishie hapo

Karibuni, tuendelee

This is stupid

Toa mawazo waziri mkuu afanye nini zaidi ya kinachofanyika sasa
 
Back
Top Bottom