Coronavirus: Tanzania bila lockdown tutakufa tuishe

Coronavirus: Tanzania bila lockdown tutakufa tuishe

cutelove

JF-Expert Member
Joined
Oct 3, 2017
Posts
3,586
Reaction score
8,389
Habari njema kwa majiji ya Roma, Madrid, New York, taarifa za leo zimeonyesha maambukizi na vifo kutokana na Covid 19 umepungua.

Na hii imetokana na lockdown katika majiji hayo pia na maeneo mbalimbali ya nchi hizo Italia, Spain na USA, hata kule Wuhan bila lockdown corona isingeisha.

Kuna kauli zinatumika na viongozi wa Tanzania kuwa hawawezi kutumia mbinu za mataifa yaliyoendelea kudhibiti Corona kwa kuwa Watanzania wengi ni masikini.

Na kauli hii inaungwa mkono na viongozi wa serikali, chama tawala na upinzani lakini.

Huko Uturuki Rais wa nchi hiyo alisema wananchi wachape kazi lakini kilichoripotiwa leo na madaktari wakinukuliwa na vyombo vya habari ni kuwa maambukizi katika taifa hilo yanaenda kwa kasi zaidi ilivyokuwa China, Italy, Spain na USA, yaani kiwango cha maambukizi huko Uturuki kinatisha.

Kule Brazil hivyo hivyo, tukija hapa Bongo unaambiwa lockdown haitawezekana, hebu tupeni mbinu mbadala ambayo mnafikiria kuwa inaweza kuzuia maambukizi, maana nahisi wiki mbili zijazo tutakuwa tunaongea lugha moja.

Kula USA mpaka chui ameambukizwa korona, huku kwetu mbwa, paka na ng'ombe wasipo ambukizwa tumuombe Mungu.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mkiifuta lockdown vichwani kwenu kama ndiyo njia pekee bora ya kupambana na Corona ndivyo mtatengeneza mwanya mzuri wa kuwaza ni njia gani bora ya kupambana nayo.

Kama utaendelea kuwaza lockdown, corona itapamba moto na mtakimbilia lockdown ambayo italeta matokeo hasi zaidi ya corona yenyewe.

Lockdown ni mzigo mkubwa kwa Tanzania; hakuna atakayeweza kuubeba; si serikali, si wahisani, si wananchi wake.
 
Hivi haya Mawazo waTz mnayatoa wapi?

Kama watu tu bila lockdown watu wanalala na njaa uje ufungie watu ndani kwa Uchumi upi?.. hayo magonjwa ndio yameanza leo.. mbona TB inatembea na wateule kila Mwaka, Malaria inakamua na neti zipo.. homa ya ini vilevile..

Tena takwimu za kutisha kabisa.. mbona hatujaskia nchi ikifungwa. Sio kila kitu Ni cha kuiga iga hovyo.. utaskia ooh wagonjwa wanaongezeka.. wewe kwenu Nani kaugua?

Cha msingi tufuate Maagizo ya Wataalamu huku shughuli za kiuchumi zinaendelea, unataka Watu waje kula kwenu?
 
wew dada kwani wiki mbili ziliyopia hali ilikuwaje?
na wiki mbili zijazo itakuwaje?

embu wacha basi mautani mama yangu!!!!!!!!
WHO wametupa wiki mbili kwa hiyo tujiandae, ila hata majirani zetu Kenya unaona mwenyewe, vifo vinaongezeka na maambukizi yanaenda kasi

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Halafu wewe dada jiheshimu na uache kueneza uwongo kwenye mitandao.

Unachokizungumzia juu ya uturuki kwamba maambukizi yako na Kasi kuliko USA mbona ni tofauti. USA kwa siku inarepot wagonjwa 15000+

Uturuki usiku huu ipo na 3000+

Punguza uvumi watanzania, wasikilizeni wanaowaongoza.
Screenshot_20200406-222633.png
 
Hivi haya Mawazo waTz mnayatoa wapi?
Kama watu tu bila lockdown watu wanalala na njaa uje ufungie watu ndani kwa Uchumi upi?.. hayo magonjwa ndo yameanza leo.. mbna TB inatembea na wateule kila Mwaka, Malaria inakamua na neti zipo.. homa ya ini vilevile.. Tena takwimu za kutisha kabisa.. mbna hatujaskia nchi ikifungwa. Sio kila kitu Ni cha kuiga iga hovyo.. utaskia ooh wagonjwa wanaongezeka.. we kwenu Nani kaugua? Cha msingi tufuate Maagizo ya Wataalamu huku shughuli za kiuchumi zinaendelea, unataka Watu waje kula kwenu?
asante ndugu yangu
 
Unataka Lockdown wakati uwezo wa kuweka hata backup ya chakula 5kg ndani hauna, wewe maliza kwanza rejesho la watu uliokopa kikoba halafu ndio uje kuandika huo ushubwadu wako JF, unadhani Lockdown ndio kama shughuli ya kumtoa mtoto 40 aka kibeseni??.

Lockdown ni mziki mwingine hautopata hata nafasi ya kwenda kudanga Sinza, nje wajeda wametanda hata mtoto akiumwa unaambiwa kaa ndani hamna kutoka na huko uswahili kwenu Chumba hapa choo Mbagala mbona mtajiharishia ndani mwezi mzima badala ya kufa kwa Corona mtakufa kwa njaa, UTI na kipindupindu.
 
Mkiifuta lockdown vichwani kwenu kama ndiyo njia pekee bora ya kupambana na Corona ndivyo mtatengeneza mwanya mzuri wa kuwaza ni njia gani bora ya kupambana nayo. Kama utaendelea kuwaza lockdown, corona itapamba moto na mtakimbilia lockdown ambayo italeta matokeo hasi zaidi ya corona yenyewe.
Lockdown ni mzigo mkubwa kwa Tanzania; hakuna atakayeweza kuubeba; si serikali, si wahisani, si wananchi wake.
Bila lockdown, jamani tuhurumiane, maambukizi yanaweza kuwa kwa binadamu na wananyama, mimi nawaza hakuna mbinu mbadala

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom