Copy and paste toka kwa mtatiroJ

Kapyungu A

JF-Expert Member
Jul 8, 2015
3,499
3,161
Ndugu zangu Watanzania Mimi ALPHAYO
NDANGALASI, Leo Tar.27/12/2015 nilikuwa
safarini tokea Dodoma kwenda Dar.kwa basi la
CHAMPION. kuna abiria mwenzangu kwa bahati
Mbaya wakati anashuka njiani kati ya Dom na
Moro kashuka na Begi ndogo ambalo si lake.
Ambalo ndani yake kulikuwa vitu vyangu
vikiwemo vyeti hivi:
Cheti cha shahada ya kwanza (udsm.)
Cheti cha Advance level (same sec. school)
Cheti cha o-level ( Mlimba sec. School)
Cheti cha kuzaliwa
Cheti cha mafunzo ya udereva na leseni.
Cheti cha membership of Graduate Engineer
(ERB)
Cheti cha membership of institute of Engineers
TZ
Na vyeti vya membership CCT na USCF vyote vya
chuo kikuu cha Dar es salama
Naomba msaada wenu Wa kusambaza ujumbe
huu ktk magroup mengine ili nipate vyeti
vyangu. Nitashukuru sana kwa msaada wenu.
Mawasiliano.
0766-306-289
0653-380-398
0788-022-087
 
Pole Sana Ndugu
Naamini Aliyeshuka Na Hilo Begi Atakuwa Mstaarabu Baada Ya Muda Yaani Atakapofungua Na Kuona Siyo Lake Atakutafuta
 
Ukiamua kutembea na documents muhimu Kama hizo inabidi uzihifadhi ndani ya hand luggage,ambayo itakuwa na wewe muda wote safarini.
 
Pole Sana Ndugu
Naamini Aliyeshuka Na Hilo Begi Atakuwa Mstaarabu Baada Ya Muda Yaani Atakapofungua Na Kuona Siyo Lake Atakutafuta

Mimi naona hujaeleweka vizuri unatoa taarifa ya kupoteza/kuibiwa au kubadilishiwa begi? Sasa kama ni kubadilishiwa begi baada ya mwenzio kuona linafanana na la kwake wewe uliondoka na begi lake? Kama ndivyo atalipataje mbona hujaeleza la kwake lilikuwa na vitu gani ili apate moyo wa kukupigia simu? Na wewe mpaka kutembea na original documents zote hizo ulitoka kwenye interview ambako sharti lilikuwa kuviona vyeti halisi?Unaelewa ugumu wa wizara ya elimu kukupatia vyeti vingine? Vyeti muhimu kama hivyo usingeweka kwenye begi mkuu vinhifadhiwa kwenye mkoba wa mkononi. Nakuombea mafanikio ila punguza kauzembe kidogo.
 
Back
Top Bottom