Ronal Reagan
JF-Expert Member
- Nov 4, 2010
- 5,298
- 3,060
Narudia tena kuwa mimi sina shaka kabisa na uelewa wako kwenye madini na pia ni jambo jema sana kama tungekuwa na smelter yetu hapa nchini. Pia ingekuwa bora zaidi ungekuja na supporting details za kuonyesha kuwa economically is vaible kuwa na smelter yetu inayotosha kiwango cha uzalishaji wa migodi yetu kwa mfano inahitaji vitu hivi na hivi.
Kuwashutumu TMAA kwa utafiti wao wa kusema kuwa ili smelter kuwa commercially viable kwa nchini kwetu "Tanzania" lazima iwe na capacity ya 150,000 tons per year bila keleta utafiti wako uliotimia si sawa. Tukumbuka unapofanya visiability study inahusu eneo husika na si kufananisha na Sichuan or Inyati kama graph inavyoonyesha. Ili kufanya idea kuwa business enterprise unatakiwa kuangalia kwa umakini mazingira ya ndani na nje ya eneo husika.
Hili jambo linahitaji umakini mkubwa sababu si project ndogo sababu pia tayari tuna project nyingi tu hapa nchini zimebadilika na kuwa "white elephant" sababu ya kukosa in depth investigation of the idea and whether its viable to be converted into a profitable business enterprise.
Inafika wakati lazima tutambue tofauti ya wants na needs, na hivyo kwenye approach zetu lazima tuwe impartial tusifanye mambo kwa mizuka na kukurupuka. Naheshimu sana munkali wa Raisi wetu kuwa na Tanzania yenye smelter yake lakini pia tuwe wawazi ya kuwa 'do we real need it now' tena kwa gharama za serikali? Mimi naamini kama tungetengeneza mazingira rafiki nchini nahakika Acacia Mining au wadau wao wangeweza kununua na kujenga smelter yao hapa hapa nchini bila hata sisi kutumia gharama zetu.
Lakini haya mazingira rafiki imekuwa wimbo kwa miaka 56 sasa na hata vile vizuri vichache tulivyoachiwa na mkoloni tumeshaviharibu. "We wants what we do not need" na mfano rahisi tazama scholars wetu wengi sasa wamekimbilia siasa na kuacha vyuo vyetu na elimu inaanguka mbadala na kuviendeleza kwa kutumia weledi wao na kuvifanya kuwa research institutions. Hiyo yote ni sababu wamesoma wasichokiitaji na sasa wanahitaji wasicho kisomea (siasa) ndiyo matokeo yake inchi iko shaghala baghala.
Excellent and well-balanced presentation EWGM.
Somehow kuna watu wanadhani humu kuwa ni wajibu wa mwekezajij kujenga smelters. Na kwamba ikijengwa basi ndio one-stop solution for all mining problems, sio kweli.