Dola milioni 300, siku 90, sentano kipande haijalipwa! acacia inakula hasara, has no capacity to pay! Tumedanganywa?

Pascal Mayalla

Platinum Member
Sep 22, 2008
50,468
113,583
Wanabodi,

Hili ni bandiko la swali, kuwa ile ahadi ya Tanzania kulipwa kishika uchumba cha Dola Milioni 300 na Acacia, kuonyesha nia njema, sasa tunakwenda Siku 90, ambayo ni miezi mitatu tangu tumeahidiwa, hakuna hata Sentano Kipande Iliyolipwalipwa huku taarifa za mahesabu ya Acacia zikionyesha Inakula Hasara, na Fedha walizo nazo, inaonyesha wazi kuwa hawana uwezo wa kulipa hata hicho tuu kishika uchumba, sembuse mahari!. Taarifa hizo zinaonyesha Acacia has No Capacity to Pay!, Swali ni Jee Tanzania Tumedanganywa?, au tuendelee kusubiria kwa matumaini Noah zetu?!.

Niliwahi kushauri humu kuwa bila Watanzania kupata elimu ya ni nini kinachoendelea ndani ya sekta ya gesi na madini yetu, hakuna jinsi, tutaendelea kuibiwa tuu na kudanganywa kama Watoto wadogo!.
Mkapa na Kikwete Walidanganywa na Wakadanganyika!, Magufuli Anadanganywa!, Jee Atadanganyika?.

Maendeleo ya kweli TZ Yataletwa na Elimu na Ukweli. Tusidanganye, Tusidanganywe, Tusidanganyike!

Gesi asili: Is it "day light robbery?!" Watanzania tunaibiwa mchana kweupe!

Tunakwenda siku 90 tangu tulipoahidiwa kishika uchumba cha dola milioni 300, lakini mpaka leo ni miezi 3 hakuna taarifa yoyote ya kulipwa hata senti tano kipande, unless kama tumelipwa kwa siri, lakini kwa mujibu wa press release ya Acacia iliyotoka kwenye website yao, inaonyesha kwenye robo ya mwisho ya mwaka jana, Acacia wanapa hasara kama inavyosome hapa.
Press Release Item
Fourth Quarter Production Report for the three months ended 31 December 2017

15 Jan 2018

Based on IFRS and expressed in US Dollars (US$)

Acacia Mining plc (“ACA’’) reports fourth quarter production results
"We are pleased to report fourth quarter production of 148,477 ounces driven by strong operational performance at Buzwagi, whilst we successfully transitioned Bulyanhulu into a reduced operational state.” said Peter Geleta, Interim CEO of Acacia. “Disciplined cost management, combined with the operational performance, led to Q4 2017 all-in sustaining costs (“AISC”) of US$779 per ounce, which helped to significantly reduce the cash outflow in the quarter despite the cost of transitioning Bulyanhulu to reduced operations. At the end of the quarter, as previously announced, we also agreed to sell a non-core royalty for US$45 million which will increase the strength of our balance sheet. Our focus remains on delivering optimal performance in the current operating environment and delivering value for all of our stakeholders. We are also continuing to support efforts towards achieving a negotiated resolution with the Tanzanian Government. We look forward to providing guidance for the year in our preliminary results in February."

Highlights
  • Q4 2017 gold production was slightly ahead of expectations at 148,477 ounces, although 30% lower than Q4 2016 which was a direct result of Bulyanhulu transitioning to reduced operations
  • Gold sales of 147,636 ounces were in line with production with all gold produced being in doré form
  • Preliminary Q4 2017 AISC1 of US$779 per ounce sold, 18% lower than Q4 2016 and preliminary cash costs1 of US$581 per ounce sold, 14% lower than Q4 2016
    • Q4 2017 preliminary AISC1, assuming sales ounces equalled Q4 production, would have been approximately US$764 per ounce
  • 2017 gold production of 767,883 ounces, 7% lower than 2016 as a result of lower production mainly from Bulyanhulu, but ahead of revised full year guidance of 750,000 ounces
  • Full year sales of 592,861 ounces, 27% lower than 2016, driven by the impact of the concentrate export ban
  • Preliminary 2017 AISC1 of US$875 per ounce sold, 9% lower than 2016 and below full year guidance range
    • 2017 preliminary AISC1, assuming sales ounces equalled full year production, would have been approximately US$798 per ounce
  • Cash balance was US$81 million at 31 December 2017 (net cash position of US$10 million), a decrease of US$15 million during the quarter as a result of the cost of transitioning Bulyanhulu to reduced operations
  • Sale of non-core royalty in December for US$45 million with proceeds due to be received in January 2018
Hasara hizo ni kama ifuatavyo,
  1. Wamezalisha 148,477 ounces za dhahabu. Uzalishaji umeshuka kwa asilimia 30% kutokana na kuzuiwa kwa makinikia ya mgodi wao wa Bulyanhulu.
  2. Bei ya dhahabu ni US$779 per ounce sold, ambayo ni pungufu ya asilimia 18% ukilinganisha na mwaka uliopita.
  3. Cash costs1 ni US$581 kwa kila ounce sold, ambayo ni pungufu ya asilimia 14% ukilinganisha na mwaka jana.
  4. Uzalishaji wa jumla kwa mwaka 2017 gold production of 767,883 ounces, ambao ni asilimia 7% pungufu ya mwaka uliotangulia.
  5. Mauzo ya mwaka mzima ni 592,861 ounces, za dhahabu ambayo ni pungufu ya asilimia 27% kwa mwaka uliotangulia.
  6. Financial position yao kwa sasa wana cash ya US$81 million at 31 December 2017 (net cash position of US$10 million), wamepata hasara ya US$15 million kwenye robo ya mwisho peke yake!. NB hawakueleza hasara ya jumla ya mwaka mzima!.
  7. Ili kujinusuru kiuchumi, mwezi December, wamelazimika kuuza baadhi ya non-core royalty ambapo wataingiza US$45 million mwezi huu wa January.
What does that mean?.
Taarifa hii inaonyesha hawa Acacia, hawana the capacity sio tuu ya kutulipa lile deni tunalowadai, bali hawana hata uwezo wa kulipa hata robo tuu ya kile kishika uchumba cha dola milioni 300 tulichoahidiwa!, unless kama Fedha hizo zitatolewa na mzazi wale, Barrick, nimemtembelea baba mtu, kuiona taarifa yake ya Fedha Barrick Gold Corporation - Barrick to Report Fourth Quarter 2017 Results on February 14 and Will Hold 2018 Investor Day Webcast on February 22, nikaambiwa itatoka siku ya Valentine, February 14.

Kwa kawaida mtu unapokwenda kuoa, unakwenda na kishika uchumba chako kabisa!, ukibisha tuu hodi na kufunguliwa, unakabidhi kishika uchumba kuonyesha nia ya kuposa. Kishika uchumba huwa hakina ahadi, unakuja nacho upfront, ukiishakubaliwa, ndipo unapangiwa mahari, na hii ndio yenye ahadi, utalipa lini, tena unaweza kukopeshwa mchumba, mahari ukalipia taratibu hadi ukamaliza!.

Sisi Watanzania, baada tuu ya kuhadithiwa ahadi ya kishika uchumba, tukaanza kushangilia, na mpaka leo hata hayo mahari hayajapangwa tukisubiri kishika uchumba chetu kilipwe!. Kama tulivyotangaziwa kishika uchumba hiki kwa mbwembwe, pia tuwe tunapewa update ya ni nini kinachoendelea, mimi kwa upande wako bado naamini niko right kuwa Watanzania tunadanganywa, tunaibiwa, na tutaendelea kudanganywa na kuibiwa, hadi tuwe na elimu ya kujua kilichomo ndani ya makinikia!.

Hizi hasara ni taarifa kuwa kutokana na kuzuiawa kwa makinikia, Acacia na Barrick wanapata hasara, hivyo ili watulipe hata hicho tuu kishika uchumba cha dola milioni 300 tulichoahidiwa, lazima kwanza makinikia yaruhusiwe kuondoka, na tukiruhusu tuu!, tumeliwa!, tutaendelea kuibiwa hadi tuelimike!.

Swali linabaki, kwenye hii issue ya makinikia, jee Tanzania tunajua kweli tunataka nini na tutapata nini kama sijasikia mpango wowote wa uchenjuaji wa makinikia?.

Paskali.
Rejea
Priorities Zetu Nini?. Dola Milioni 300 Zinatosha Kununua Smelter, Jee Tununue Au Tuzitumie Kwa Mahitaji Muhimu Zaidi?
Kuzuia Mchanga wa Dhahabu, Magufuli Anastahili Pongezi. Tusiishie Kwenye Madini Tuu na Gesi Jee?!.
Maendeleo ya kweli TZ Yataletwa na Elimu na Ukweli. Tusidanganye, Tusidanganywe, Tusidanganyike!
https://www.jamiiforums.com/threads...uchumba-cha-dola-milioni-300.1340383/page-8si
Madini Report Betting: Wanaotuibia Madini Yetu, "They Can Go To Hell" or Tuwasamehe Kama EPA?..
Makinikia: Je, Vyombo Vya Habari Vifukue Makaburi ya Chanzo, Au Kushangalia Tuu Matokeo?.Jicho Letu.
Sensationalism kwenye Professional Presentations inakubalika? Ni swali tu...
A Compromised Possibility: Iweje Ripoti ya Kamati ya 2 iibukie Acacia-London kabla ya kwa Magufuli?
Hivi Hawa Acacia Wana Adabu Kweli?, Baba Akiishasema Kitu, Mtoto Anatakiwa Kunyamaza. Bora Wafungashe Tuu, Waondoke?
Zita Act Retro-Respectively? Tutavunja Mikataba Yote Iliyopo?, Can we Stand?, Do we Have The Guts?.
Mkapa na Kikwete Walidanganywa na Wakadanganyika!, Magufuli Anadanganywa!, Jee Atadanganyika?
Wataalamu Hawa Wachunguzwe!,Jee Kuna Posibility Walihongwa Kutoa Ripoti Kuwa "Tanzania Hatuwezi?!".
Kumbe Tunapaswa Kumiliki,16% Stake ya Migodi Yote!, Jee ni Kweli Tunamiliki?, Are We Open & Fair Kwa Investors?.
 
Nakumbuka siku moja tukiwa ziarani na mkwere nchi fulani bwana mmoja aliuliza "hivi tukiamua kuachana na ununuzi wa madini ya Afrika mtayatumia kufanya nini?"

Swali hili linaungana na kauli yako kuhusu umuhimu wa elimu kwa watu wetu nchi hii inahitaji sana elimu.

Si madini tuuu tuna resources nyingi bado hazijatusaidia.

Pole zake bwana Ngosha anatakiwa apewe elimu shibishi ya the " corporate world"
 
Mzee Baba, Paskali ingekuwa vyema ukaandika barua ikulu, tena barua ya wazi kumkumbusha Mkuu kuhusu wadeni wetu Acacia, na nakala imfikie Paramagamba.
Hilo swali lako sisi hatutaweza kulijibu.

Tukasubiri Noah, Noah zikageuka Balimi, sasa Balimi zenyewe ndo hatahatupewi ili mbao zilegee.

Hii ndio TZ ya vi-wonder
Na TZ ndio Poliwood kwenyewe
 
Nakumbuka siku moja tukiwa ziarani na mkwere nchi fulani bwana mmoja aliuliza "hivi tukiamua kuachana na ununuzi wa madini ya Afrika mtayatumia kufanya nini?"

Swali hili linaungana na kauli yako kuhusu umuhimu wa elimu kwa watu wetu nchi hii inahitaji sana elimu.

Si madini tuuu tuna resources nyingi bado hazijatusaidia.

Pole zake bwana Ngosha anatakiwa apewe elimu shibishi ya the " corporate world"
Ungekuwa na elimu ya coporate world usingeshindwa kujua kinachoendelea...
 
Rais hapaswi kulaumiwa kwenye hili na anahitaji kutiwa moyo na watanzania wote bila kuingiza itakadi za vyama. Kwa hakika amepambana lakini kuna sehemu tunakwama, hasa kwenye utaalamu wa mambo haya ya madini na mikataba mibovu ambayo inasimamiwa kimataifa na ilishaingiwa huko nyuma.

Naamini Kinu cha uchenjuaji makinikia kitakua suluhisho la huu wizi wa mchana, rais aendelee kubana hayo mkontena haiwekani muuza korosho ajiendeshe kwa kuuza maganda ya korosho badala ya korosho yenyewe. Tumeibiwa sana.
 
Yale makontena bado tunayashikilia kwani?
Na wale watu wa Acacia kutoma Canada bado wanaendelea na mazungumzo au walisharudi kwao? Kimya kweli naona
Yani nikifikiria zile Noah zetu...naumia sana roho. Maana nilisharenew leseni na kuuza kale ka starlet kangu. Ntatembea kwa miguu hadi lini?

Maana mkuu kabisa alituambia "wanaume wamekubali kutulipa"...

Maskini nchi yangu...... aliyeiloga Mungu amlaani
 
Yani nikifikiria zile Noah zetu...naumia sana roho. Maana nilisharenew leseni na kuuza kale is starlet kangu. Ntatembea kwa miguu hadi lini?

Maana mkuu kabisa alituambia "wanaume wamekubali kutulipa"...

Maskini nchi yangu...... aliyeiloga Mungu amlaani
Kwa hiyo Kwa taarifa hii ya Pasco ndio unaamini hatutalipwa?
Kweli naamini maneno ya Trump
 
Hakuna malipo nje ya mkataba,
Cha muhimu ni srikali kuweka wazi nikataba ijadiliwe kwa uwazi ili kuondoa au kupunguza mambo ya asilimia kumi. Botswana na Ghana waliweza kutikana na uwazi na uzakendo was mamlaka husika (parliament na rais)

Pia ni lazima wabunge na watz wore tuacge siasa za kubaguana kwa vyama Bali tufanye siasa za hoja kuhusu rasilimali zetu.

Haiwezekani wabunge wanazomeana kisa tu mcgango umetolewa na mpinzani
Hatustahili/tunastahili kulipwa kutokana na mikataba na si mazungumzo ya kupata public support
 
Hizi hasara ni taarifa kuwa kutokana na kuzuiawa kwa makinikia, Acacia na Barrick wanapata hasara, hivyo ili watulipe hata hicho tuu kishika uchumba cha dola milioni 300 tulichoahidiwa, lazima kwanza makinikia yaruhusiwe kuondoka, na tukiruhusu tuu!, tumeliwa!, tutaendelea kuibiwa hadi tuelimike!.
Sababu ya kutokulipwa hiyo hapo, umeitaja mwenyewe. Kama kuna nyingine muulize yeye moja kwa moja.
 
Paskali, hayo makorokocho yoote uliyoandika sijayaelewa/sitaki kuyaelewa.

Haimaanishi na yale tuliyoelezwa na kamati niliyaelewa, hasha!

Mlituambia kuwa yale Makinikia si kitu, ni vivumbi tu vya dhahabu...kamati ikasema TUNAPIGWA, mmapinga.....mkatoa makorokocho meeengi ya kupinga.

Leo, hao hao wanakuaminisha kuwa wanapata hasara kwakuwa VIVUMBI vimezuiwa, wewe unajitoa ufahamu kuwa unawaelewa sana?

SIEIJII alisema hao jamaa walikuwa wanajiendesha kwa hasara, sasa kama watu wanakaa miaka ishirini sehemu na kusema wanapata hasara tuuu na hawaondoki, leo wanakwambia ABC...unakuja hapa na kujiona wewe ndo ulioumba maandishi jinsi unavyoyaelewa.....

Mi sielewi chochote yani, FUKUZA tu....si wanapata hasara, waondoke......wasomi wetu hawa wanaochanganya maneno, wanachoweza ni kutuchanganyia lugha tu wakidhani ndio uerevu au kuendelea.....
 
Yani nikifikiria zile Noah zetu...naumia sana roho. Maana nilisharenew leseni na kuuza kale is starlet kangu. Ntatembea kwa miguu hadi lini?

Maana mkuu kabisa alituambia "wanaume wamekubali kutulipa"...

Maskini nchi yangu...... aliyeiloga Mungu amlaani
Yani ile habari ilinifurahisha sana ila ndo tukaishia kudanganywa
 
Back
Top Bottom