Sawa kabisa, ila mie tena na tena narudia, kila idara, taasisi, shirika, wizara, bodi, wizara zinazo hawa wasomi, wana masters kibao, maprofesa, wana ma phd mawili mawili mpaka 3, lakini mbona kusoma mikataba wanashindwa, mbona kujuwa wafanyakazi hewa issue, mbona kujuwa kuna ufisadi hapa au pale ni kazi kwao, kila kitu kwao haiwezekani lakini ni hodari wa kuongea na kutoa ma bombastic ya kisomi radioni au kwenye TV, wanaishi maisha ya anasa sana, makubwa ya gharama, nyumba za kifahari, mashamba ya hekari za ajabu, hata kuwakodishia mahawara majumba kama sio kuwajengea, na hapo ndipo tunapojuwa kweli hatuna wasomi bali wezi tu, mafisadi wanaojali matumbo yao na kuishia kupiga domo na porojo, INATOSHA...