Julius Mtatiro
Member
- Jun 20, 2009
- 45
- 225
mkuu mtatiro,ukweli ni kwamba nchi yetu inapitia mabadiliko,na sis vijana ndo engine ya mabadiliko haya,bahati nzuri kipindi upo chuoni nami nilikuwepo!kuna hoja ya kwamba upo cuf kama ajira,kwani kam,a ni mwana harakati wa kweli ungetizama uelekeo sahii!umeijibu kiujanjaujanja!kwamba we ni mjariamali,we umetaja mali zako!kabla ujakubali hicho cheo!unakiri kwamba cuf ulijipeleka,unakiri kwaba at the time unajiunga cuf,chadema ilikuwa vibrant!sasa kwa hili hukubaliani nami kuwa uliona hajira unayotafuta cuf ni muafaka zaid kwani kwingine kuna ugumu kidogo,walaji ni wengi?na kwa nini kama si ajira mbona hujaonyesha ni kiasi gani unapata kutokana na unaibu katibu mkuu!then tukachambua na kujua ukweli?
Julius umejibu vema sana tena kisomi.Hongera kwa hilo.Nina swali moja kwako.Kwanini wakati wa kampeni Igunga Cuf iliungana na ccm kuishambulia chadema ktk kila mkutano wenu? Ilifika mahali bila aibu Hamad Rashid akauambia mkutano Chadema ni chama cha wachaga.Huoni hilo linawafanya muonekane CCM B? Nijibu Julius.
Julius!Mpiganaji,
ukweli ni kuwa katika kampeni za Igunga CHADEMA ndio walichukua muda mwingi kuishambulia CUF na kumbuka hata kuna wakati walikuwa na operesheni kuzunguka nchi wakiishambia CUF. Sielewi hii aidia kuwa CUF walikuwa wanaishambulia CHADEMA ilitokea wapi. Igunga kazi kubwa ya CHADEMA ilikuwa ni kuishambulia CUF kuwa CUF ni CCM B, ni mke wa CCM, CUF imeolewa na CCM , siyo chama cha upinzani, CUF ni chama cha Zanzibar n.k. Nijuavyo mie CHADEMA ndio walichukua muda mwingi kuishambulia CUF na huku vijana wao wa vyuo vikuu waliokuwa katika kila kijiji wakiendelea na kampeni kali dhidi ya CUF, lengo ilikuwa ni kuhakikisha kuwa CUF haiungwi mkono na wananchi na kuwapa wananchi mtizamo kuwa CUF ni CCM tu, na katika hili walifanikiwa sana.
Julius!Ndugu yangu Luka,
Idea yako ni nzuri, lakini utambue kuwa sikufika chuo kikuu kutafuna fedha za walipa kodi ili baada ya hapo niwe mshabiki wa vyama vya siasa. Siku zote nimejifunza umuhimu wa kufanyia kila jambo utafiti. Sielewi Idea ya kugeuza wadhifa wa chama cha siasa kuwa ajira, sielewi hii kaka. Wakati napewa wadhifa wa ukurugenzi CUF, mkurugenzi alikuwa anapewa posho ya shs 280,000/- hii ina maana kuwa kwa CUF hatuajiri mtu, kila mtu anajitolea na kuna mikataba ya kujitolea. Kabla sijawa naibu katibu mkuu aliyekuwepo(mhe. Bashange) alijitolea kwa mwaka mzima na baadaye akakiomba chama akapumzike ajenge maisha ya familia yake ambayo ilianza kuyumba kiuchumi. Katika CUF naibu katibu mkuu huna access na pesa, pesa wanasimamia kurugenzi ya fedha tu. Wewe naibu katibu mkuu unakagua nini wamelipa na kama imekuwa sahihi baada ya makubaliano ya vikao. Kwa hiyo hakuna loophole ya kula hela ndani ya CUF na ndiyo maana hadi leo CUF ina rekodi nzuri ya masuala ya pesa, so siku rafiki yangu ukipewa unaibu ukadhani utakula pesa za CUF umeula wa chuya.
Jambo lingine ni kuwa, baada ya kumaliza chuo ningeweza kupata ajira nzuri katika makampuni kadhaa kama ningetaka, lakini niliona nikienda kufanya kazi ofisini sitakuwa na muda wa kufanya advocacy na kuifikia jamii pana zaidi, niliona malengo yangu ya kuelimisha wananchi wengi na kuwatetea yatapotea.
Mwisho napenda kukujulisha kuwa Naibu Katibu Mkuu wa CUF kwa viwango vya sasa anapokea POSHO ya tzs 525,000 kwa mwezi. Kwa hiyo unaposema nilijiunga CUF ili kupata ajira that mean 525,000/- kwangu ndiyo fadhila. Hapa nilipo nina digrii moja, nina advanced diploma moja na ninasoma shahada ya pili.
Huyu kijana alikuwa hapendi shule, alikuwa mwendesha migomo mkuu akiwa UDSM. Nilikuwa kila mara migomo ikitokea UD lazima aonekane na alikuwa anavaa tu nguo moja! Tshirt ya Arsenal!!
Mkuu Julius Mtatiro, kwanza hongera kwa kuja humu Crystal clear. Pili asante sana kwa majibu yako ambayo yanazidi kuthibitisha wewe sio tuu ni kichwa, bali pia ni jembe kweli la kuchapa kazi kwenye medani za siasa.
Enzi zile mimi nikiwa mwanahabari, baada ya Mrema kuhama CCM, nilimuuliza maswali kama haya naye alitoa majibu mazuri kama yako kuhusiana na hoja za kuhama chama. Kilichofuatia sote tunakijua.
Nakuaminia wewe ni wewe hivyo post zako nazichukulia kama msahafu wa msimamo wako kisiasa na nitazitumia kama rejea from time to time kukuthibitishia CUF is a wrong party for you huku bara.
Umethibitisha SUK inafanya vyema Zanzibar kwa kupandisha bei ya zao la Karafuu toka 5,000 kwa kilo mpaka 15,000, this is fine, kitu ambacho hukusema ni kuwa wana CUF wote walioingia SUK, wamekula kiapo cha kutekeleza ilani ya uchaguzi ya CCM!.
Nafasi ya Maalim Seif kama Makamo wa kwanza wa rais ni purely ceremonial with no executive powers na mwenye mamlaka ni makamo wa pili!.
Pamoja na yote uliyosema na kwa uwazi uliopitiliza hata mipaka, fact zinabaki kuwe wewe Julius Mtatiro ni mpiganaji wa kweli uliokuweko kwenye waste party, the sooner you realize, the better!. Other wise time will tell.
I wish you all the best hapo ulipo.
Pasco (wa jf).

Pasco kwa maoni yako unafikiri angeenda chama gani?
Brother Wabe,Pasco kwa maoni yako unafikiri angeenda chama gani?
Mpiganaji,