Comrade Julius Mtatiro

Na wanashindwa kufika tamati kwani lengo lao kubwa la kuiondoa ccm ni la kipuuzi, nadhani wangekuwa na lengo zuri la kimaendeleo ni wazi wangekuwa wamefanikiwa.
 
Hii sheria MBOVU iliyowekwa juu vyama vya siasa ndio inayowagharimu CUF Zanzibar "kuwa chama cha siasa lazima kiwe cha Muungano."

Tokea lini watanganyika wakawa watu ambao wanajiamini na kusimamia Yale wanayoyaamini!!!???

90% ya watanganyika wanaumwa na UGONJWA WA BORA TUMBO!! Ugonjwa ambao dakika moja unamtoa mtu katika msimamo aliousimamia kwa zaidi ya Miaka 10!!! Dokta MIHOGO, ALI KESSY, PROPESA PUMBA, MWAKWEMBE, SHOVJI, N. KASAKA, HIZO TAMBWE, N. k

Hao hapo ni mifano hai kati ya mingi sana dhidi ya Wafoji vyeti wa KITANGANYIKA ambao kwao TUMBO ndio limeshika akili zao zote.

Nikija kwako ndugu "NJAA KIKWAO MHESHIMIWA" kuwaona CHADEMA ndio wapinzani wakweli na kuwadharau CUF waliopoteza wanachama wao na wengine kuwa wakimbizi katika kupigania nchi hii IPATE KATIBA MPYA, TUME HURU ZA UCHAGUZI leo unawaona sio wapinzani wakweli!!!!!!!!!! Hili bwana NJAA kwa kweli ni ajabu Sana!!! Bwana NJAA (PASCAL MAYALLA) nakuomba unipe ushahidi ambao utaionyesha jamii kuwa CHADEMA PEKEE ndio wapinzani wakweli katika INJII HII, chama ambacho kinaogopa mikwara ya watawala hivyo kila wanalolipanga wanashindwa kulitimiza (UKO WAPI UKUTA AU PEOPLE'S POWER)
 
Kuhusu J, Mtatiro shame CUF na kuelekea CHADEMA wala hilo haliwezi kuwa Tatizo kwa CUF ambao wanajitoa nafsi na mali zao katika kuifanya CUF kuendelea kuwa NGANGARI.

CUF ilikuwa na watu wenye ushawishi mkubwa ambao walipokuwa wanasimama kila mtu anaacha yake kuwasikiliza.

Watu kama nyaruba, TAMBWE hiza, Shaibu akilombwe, Lipumba walikuwa nguzo muhimu katika CUF jee walipohama CUF iliyumba au ilizidi kuimarika!!!???

Katika vyama vyote vya upinzani katika INJI hii hakuna chama ambacho kimeandamwa na chama tawala na kupandikiziwa kila aina ya propaganda zaidi ya CUF.

CUF imeitwa chama cha wapemba, waislamu, chakigaidi hadi kufikia kupakaziwa kuwa wameagiza kontena la majambia kwa ajili ya ugaidi.

Ni CUF hiyo hiyo makumi ya wanachama wake wameuliwa, kunajisiwa, kuwa wakimbizi, kuwa walemavu, kuvunjiwa makaazi yao, biashara zao, kuwekwa ndani kwa kwa uhaini. WADANGANYIKA acheni kujitekenya na kucheka wenyewe kwa kuidharau CUF na kuipaisha CHADEMA kuwa ndio wapinzani halisi. SIKU ZOTE UDOGO WA CUF ni UDOGO wa nyuki (si mnakumbuka NGANGARI NA NGUNGURI!!??) Na wingi wa CHADEMA na wingi wa INZI si mnakumbuka UKUTA!!!???
 
namfahamu Julius.

mzee wa "The Struggle"

mpambanaji wa ukweli.

hata mawe ya Revolution Square ya UDSM yanamjua kwa namna alivyo na moyo wa uchungu wa kuona Watoto wa Tanzania wanakomboka kifikra, na siku inakuja yatakaposema kuwa ameisaliti ardhi ya Tanzania na Watanzania kwa kujiunga na CCM, chama ambacho kinatawala kwa sababu ya umbumbumbu na umasikini wa Watanzania walio wengi.

si mtu wa kupoteza, ila aliamua tu mwenyewe (pengine kutokana na ushauri mbaya) kupotea.

ngoja nimvutie pumzi nione kama hii nayo ataichukulia kuwa ni crap au ni 'Sauti ya Nyikani'
Duh!.
P.
 
director1, usitake kumdanganya mwenzio aachie ulaji hapo CUF!, mwenzako hapo ni naibu katibu mkuu ambayo ni very senior position. Juzi wakati wa uchaguzi mdogo wa Igunga, Mtatiro aliidhinisha malipo ya milioni 50 kulipia ile helcopter bila kushauriana na yoyote hapo CUF, hii ikiwa ni ushahidi kuwa pia anayo purchasing power kubwa, unataka aende chadema akafe njaa?!.

Kwa Tanzania tuna wanasiasa wa aina mbili, aina ya kwanza ni wanasiasa ambao siasa kwao ndio professional na ajira zao za kudumu kuendeshea maisha yao. Hawa wanaingia siasa ili waweze kuishi ndio maana Lipumba ndiye mgombea wa kudumu wa urais wa muungano kwa tiketi ya CUF.Wengi wa wanasiasa walioko CCM na CUF ndio wa kundi la kwanza. Kundi la pili la wanasiasa wa bongo, ni wale wanaoingia siasa kwa kutaka kuwatumikia wananchi, hawa wanauchungu na umasikini wa Tanzania hivyo wanaingia siasa ili kuleta mabadiliko, wengi wa walioko Chadema ndio kundi hili la pili.

CUF ni chama cha siasa cha wachumia tumbo, kinagombea uongozi ili kupata ulaji, baada ya kufunga ndoa na CCM, wanagawana ulaji, hapo sasa hakuna kingine wanachotaka ni kugawana tuu keki ya taifa na kula kwa ulaini, hivyo Mtatiro hapo alipo ni pazuri sana kwa ulaji, msimdanganye ahame aachane na ulaji aje Chadema kwenye struggle ambapo kwa sasa anakula kwa kuypewa, akienda Chadema, itambidi ale kwa jasho lake!.

Mtatiro usidanganyike, jitulize tuu hapo hapo ulipo, endelea kujilia kwa ulaini, 2015 kombea tena ubungo uendelee kusindikiza huku ukijilia kwa ulani. Kama unaweza kujipatia ulaji kwa ulaini na mteremko kama huo ulionao hapo CUF, kwanini ukapande milima na mabonde kama Chadema?.
Tena kutokana na jina la Julius, wewe ni mtaji muhimu sana CUF, naomba usifikirie kabisa kuhama, chama kitakufanya mgombea wa kudumu wa jimbo la Ubungo kama alivyo Prof. Lipumba ni mgombea wa kudumu wa urais wa muungano.
Uliona mbal sana PASCO
 
Naamini katika kujenga mfumo thabiti, na mfumo thabiti hutafutwa katika kipindi kirefu. Kuna baadhi yetu hudhani CUF itakufa na kuwa imepoteza mwelekeo, lakini napenda ifahamike kuwa CUF haitakufa na haitapoteza mwelekeo.

KUMBUKA for every decision there is a consequence. Nilijua dhahiri kuwa CUF inaweza kuwa kwenye wakati mgumu katika miaka kadhaa ijayo. Nilitambua kwamba nina jukumu la kujiunga na chama ambacho kiko wazi katika utendaji wake, chenye falsafa niliyodhani ni sahihi, chenye viongozi imara wenye malengo ya kuikomboa nchi kwa wakati sahihi na kwa kutumia njia za wazi na sahihi. Sikujali propaganda za Udini na Upemba na uislamu na upwani na uarabu na misimamo mikali n.k. Vitu ambavyo vilihusishwa na CUF kwa lengo la kuisaidia CCM na baadhi ya vyama ambavyo wakubwa walihitaji vishike dola baada ya CCM.

Nilihitaji chama ambacho nitakuwa na forum huru inayoweza kufanya maamuzi kwa pamoja bila shinikizo la mtu mmoja au wawili ndani ya chama(SIMAANISHI KUWA CHADEMA WANA MFUMO HUU).

Nimewahi kufuatwa na mhe. Freeman Mbowe ili nijiunge CHADEMA na nilimpa msimamo wangu kuwa nitajiunga na chama chochote pale nitakapoamua kufanya hivyo, baada ya hapo alinitumia delegations mbalimbali zinishawishi lakini niliomba nipewe muda.

NCCR MAGEUZI pia wamewahi kunifuata mara kadhaa kwa kumtumia Mwalimu Nderakindo Kessy na Mwalimu Mvungi ambapo niliwajulisha pia mtizamo wangu.

Viongozi wa CCM ambao wamewahi kufanya dhahiri mazungumzo name wakiniomba nijiunge CCM kwa ahadi kemkem ni wengi mno na tena mara nyingi, amewahi kutumwa Mzee w Wassira(TYSON), NIMROD MKONO, KINGUNGE, RIDHIWANI na wakati fulani waziri Mkuu(wa wakati huo) LOWASSA- amewahi kunisisitiza sana nijiunge CCM na ku-transform harakati za vyuo vikuu katika forum za CCM ili matatizo mengi ya wanafunzi wa elimu ya juu yatatuliwe lakini nilikataa. Baada ya maelezo haya naomba ifahamike kuwa ninavisheshimu sana vyama vyote ikiwemo CHADEMA, CCM, NCCR n.k ikiwa ni pamoja na viongozi wote wa vyama husika. Kwani naamini katika uwanja wa kisiasa tunatofautiana kimtizamo na kimaamuzi tuu.

Naomba ifahamike kuwa siko CUF kimaslahi (KAMA AMBAVYO BAADHI YA WADAU WANAJARIBU KUWAAMINISHA WENZAO) kwani ningetaka maslahi ningejiunga CCM chama chenye dola na pesa za kufa mtu. Siku zote katika maisha yangu pesa ni kitu ambacho hakininunui.

Maisha yangu hayaendeshwi kwa njaa kwani tangu utotoni mimi nimekuwa mjasiriamali mzuri.

Naomba nikubaliane na Director kuwa CCM ndiye mgomvi wetu mkubwa na ndiye adui wetu mkubwa. Na lazima tupambane na adui huyu hadi mwisho. Na ninaomba nitoe mtizamo kuwa ikiwa tutapata katiba mpya yenye demokrasia pana, ya wazi na isiyopendelea upande wowote lazima CCM wataondoka madarakani kupitia masanduku ya kura. Na hata wana CCM walioko hapa wanajua kuwa hivi sasa kwa hali ya maisha ya watanzania na mfumuko wa bei, kukithiri kwa umasikini n.k. hawatakuwa na karata tena 2015 hata zikichangiwa NIGERIA hazitachangika. Na katika hili mie namshukuru ndugu Jakaya kwa sababu anaimaliza CCM vizuri na hakutakuwa na dawa ya kuifufuaHAKUNAGA DAWA!

Kwa mtizamo wangu, CUF ilipaswa kupongezwa sana kwa kuwa chama cha kwanza cha upinzani kuingia serikalini upande wa Zanzibar kwani haikuja kirahisi sana. Badala yake wenzetu wanatangaza kuwa CUF ni CCM B na kuwa isichaguliwe.

Hoja ya kujiunga CHADEMA kwangu si hoja nzito sana japo sipingani na mtizamo wako. Mimi siwezi kukimbilia CHADEMA ati kwa sababu ina nguvu sana sasa. Siwezi kuwa kiongozi nisiye na visheni kiasi hicho. Kama CHADEMA wataongoza dola 2015 hiyo pia siyo sababu ya mimi kujiunga huko kwani ikiwa watu wote tutaenda kuongoza dola kupitia basi la CHADEMA at that time nani atawasemea wananchi?Nani anayetudanganya kuwa ati mwisho wa harakati za kuikomboa nchi ni pale ambapo CHADEMA watakuwa madarakani? Naogopa sana mtizamo huu wa kuamini chama kama vile dini, hata CUF msije kuiamini kama dini yenu, muihoji na muifanyie uchambuzi wa kina. Mitizamo ya namna hii ni ya kuua demokrasiaWengi wetu tukumbuke kuwa ukiingia madarakani watu wengi huanza kukuhoji, so wachache kati yetu tusidhanie madarakani kuna raha, ni stress za hali ya juu. Kwa hiyo mie sitajiunga CHADEMA ati kwa sababu inaweza kuongoza dola kabla ya CUF na ati kwa sababu imeahidi maziwa na asali, tunaweza kuwaacha wakaongoza halafu wakashindwa na wananchi wakatafuta chaguo lingine na chaguo likawa CUF.


Jambo lingine ni hii dhana ya kuhamahama, leo CUF ikifanya vibaya hapa na pale tuhamie wanakofanya vizuri kama CHADEMA n.k. Na ikitokea huko CHADEMA wakaanza kushuka kisiasa ndo tunahamia Chama kingine tena, huku ni kujikosesha mtizamo mpana wa kiukombozi na ni kujigeuza bidhaa, kamwe mimi siwezi kugeuka bidhaa.Ningehama CUF kama kingeacha misingi yake ya uadilifu, kuunganisha, kutetea wananchi na kutengeneza taifa la pamoja lenye maendeleo ya dhahiri. Ikiwa CUF itaanza kufuja pesa, kuongozwa kidikteta au na mtu mmoja au kikundi cha watu wachache n.k. nitafanya maamuzi tofauti.Hata kama iko katika SUK- Serikali ambayo imeundwa kikatiba hatujakosea popote, ikiwa tuko SUK ili kufuja pesa za umma sawa! Ikiwa tuko SUK kula na kunywa na kusaza sawa! Lakini kwa sababu tuko SUK ili kuibadili Zanzibar na kuleta maendeleo, hakuna kosa tulilofanya. Hizi propaganda za U-CCM B zitaisha tu iwapo nia yetu ya kuiendeleza Zanzibar itaanza kuonekana dhahiri. Kuna vitu ambavyo vimeshaanza kuonekana kama vile upandishwaji wa bei ya karafuu kutoka tzs 5000 hadi 15,000 kwa kilo(Hili lilikuwa kwenye ilani ya CUF na tumeingia serikalini Zanzibar tumefanikiwa kulibadili na wananchi wanafahamu hivyo) Muda si mrefu yatapatikana mambo mengine kadhaa na yataonesha umuhimu wa CUF katika SUK ZNZ.Lakini kwa sababu CUF imeendelea kushikilia misingi yake ya uanzishwaji, kazi yangu inabakia kuwa moja tu! Kupigana kuendelea kuijenga CUF ambayo inadogoeshwa kwa propaganda za hali ya juu. Kuna vyama haviamini kuwa vitaongoza dola CUF ikiwepo, vinapigana kufa na kupona kuona CUF inakufa, NDOTO ZA MCHANA KABISA!


Na ninataka niwahakikishie wana JF kuwa CUF itaendelea kusimama kwa sababu ina mfumo hadi chini, ndiyo maana hata Igunga tumepata kura 2000 ambazo wadau wanatucheka, lakini zina maana kubwa sana hata kama zimeshuka kutoka 11,000, kuwa kuna watu wanaiunga mkono CUF bila kujali propaganda wala kugawiwa fedha.Kwa wale wanaochekelea kuwa CUF lazima iendelee kushughulikiwa wanafanya makosa makubwa sana. Hii ni kwa sababu katika uhalisia nchi haihitaji vyama vyenye misingi imara na visheni pana vife kupisha chama fulani kingie madarakani. Nchi inahitaji tuiondoe CCM madarakani, tuweke chama kingine madarakani na tuwe na vyama kadhaa vyenye nguvu ambavyo vitakifanya chama kipya kisiwaburuze wananchi. Kwa wale ambao wanaona huu ni mtizamo finyu na mwembamba wataona nini kitakuja kutokea iwapo moja kati ya hayo yanatokea. Na ikumbukwe kuwa CCM ikishaondoka itakufa kabisa. CCM itakufa kwa sababu ni chama ambacho kimetawala kwa muda mrefu, kikiondoka kwenye ulingo wa siasa kinaondoka kabisa, labda kifufuliwe tena baada ya miaka 100 na vitukuu vyetu. Kwa hiyo kwa vyovyote vile panahitajika vyama vilivyojijenga na imara kama CUF vilindwe na kila mwanademokrasia ili wananchi wawe na mbadala kila chama kilichoko madarakani kitashindwa.


Mwisho nataka kusisitiza kuwa CCM lazima itaondoka 2015, hivi sasa hakuna namna ambavyo CCM itaokoka. Leo hii hata serikali haina pesa za kusimamia nchi, serikali inafilisika. Mafisadi wamepamba moto, lakini sikio la kufa halisikii dawa. Iacheni CCM ijifie, tupate chama kingine kisha baada ya hapo tutajua FUTURE ya taifa letu. Nashukuru wa maoni na mitizamo yenu nyote hata kama iko tofauti na mtizamo wangu. Kila mtu ana mtizamo wake na huo ndio mtizamo wangu katika masuala muhimu mliyouliza.

Nitajibu maswali mengine yoyot emuhimu kwa kadri yatakavyoongezwa hapa, lakini kwa kifupi.
Julius Mtatiro +255 717 536 759 (juliusmtatiro@yahoo.com),
Naibu Katibu Mkuu,
Chama Cha Wananchi CUF,
Tanzania Bara.
01 Novemba 2011.
Nakutafakari sana kwa muktadha wa leo.
P.
 
Back
Top Bottom