Huu mtizamo ni hasi sana.Mie huwa napinga sana haya mambo ya kuoanisha Ndoa na uongozi.Kwa upande wangu ndoa ni suala linalohitaji,muda muafaka na utayari.Huwezi kuoa eti simply kwa sababu unahitaji uongozi,hayo ni mapokeo ya ki ubinafsi mno,na huwa naona ni mbinu iliyotumika huko nyuma kuwanyima Uongozi vijana,huku wazee wakiendelea kujitwalia madaraka hata kama hawana uwezo.wale vijana wenye tamaa walilazimika kuoa kuwafurahisha tu wazee.binafsi ukiniambia kati ya kiongozi asiyeoa na aliyeoa,ntachagua asiyeoa,kwani atakuwa na muda wa kunitumikia vizuri kuliko aliyeoa,ambaye anaangalia kubalance interest za familia na jamiii.na obvious za familia zitapewa kiapu mbele.
kwa CDM kuwa na viongozi wasio oa au olewa ,kwa upande wangu ni kwa sababu asilimia kubwa kwao ni vijana ambao bado wako kwenye michakato.kupata mwenza ni jambo la muda mrefu,unless kama unataka kuokoteza, hilo hata wiki unapata wa kuoa.Na kwa uelewa wangu mtu makini huwa hakurupuki kwenye hili jambo.