Complicated Marital Status za wana CDM na Urais 2015

mkonowapaka

JF-Expert Member
Feb 19, 2010
1,493
767
Hello JF......

ni mara chache sana kupost jukwaa hili...mara nyingi huwa ni mchangiaji au msomaji wa masuala mbalimbali ya kisiasa yanayoendelea kutokea kila siku nchi hii..........

Upepo wa kisiasa umeendelea kuibadili nchi yetu kila kukicha....si jambo la ajabu kukuta watu wamekaa tena vijijini wakijadili mambo mbalimbali ya kisiasa....

nakipongeza pia chama changu cha Chadema kwa kuendelea kuwaamsha watanzania walio wengi juu ya mambo muhimu yanayowahusu na wanachopaswa kukifanya...binafsi nimeamshwa zamani sana.........

sina shaka na uwezo wa wana CDM katika kuwamsha watanzania walio wengi ........katika kujazia kile kilichozungumzwa na bwana Sita leo.........naomba pia safu nzima ya wana CDM kila mmoja kw anafasi yake ajitazame upya status yake maritually..........viongozi (wa CDM) wengi wao wamekua na status zinazofanana na sio sifa nzuri kwa kiongozi hasa wa kiafrika.kama kweli tunatetea tamaduni zetu za Kitanzania tulizorithishwa na babu zetu basi tuliangalie na ilo,na kama kweli tunajiandaa kuchukua dola ya nchi hii..tujipange safu hiyo....................huu ni mtazamo wangu na wala siwakilishi mawazo ya mtu mwingine...viva CDM
 
japo mume/ mke bora sio kigezo cha kukufanya kiongozi bora kwa maoni yangu naona inatoa picha ya wewe ni nani kama mtu wa kawaida kwa kuangalia mwenza wako na jinsi unavyoendesha familia yako.
Kama hujawahi kushika madaraka yoyote makubwa na huna uzoefu ndoa ni moja ya sehemu ya kukutathmini uwezo wako wa kiutawala.

Japo mtoa mada kagusia CDM mi naona linatuhusu sote bila kuangalia itikadi.
 
Lete hiyo List ya ambao unataka waoe au waolewe tuijue, maana wengine hatukuwa tunafuatilia marital status za watu!!!
 
Rais wa Botswana hajaoa.

Na Botswana imetupita kiuchumi mpaka uongozi bora na demokrasia.

Go figure.

Baada ya kuwa makamu wa Rais kwa miaka 10, kwa kifupi kama 'profile' yako inakubeba hakuna tatizo
 
Ndoa ni kielelezo cha nidhamu

kabisa family life or marriage life is important to society...maana ukiwa kama kiongozi ndio unatakiwa uwe mfano kwa jamii...sasa kama mtu ukok solo unakaa ikulu matokeo yake utaanza kuwaingiza akina wema sepetu ikulu sasa kama baadhi ya viongozi tunawaona wanavyofanya bt ikulu au sehemu ya heshima inatakiwa kiongozi awepo pale na familia yake...Huwezi kuona nchi ka america or britain kiongozi yuko solo
 
Huwezi kuwa na urafiki na CAMERON kama utakuwa umeoa jinsia tofauti!
 
VIONGOZI wote mafisadi ndani ya CCM wana NDOA na nyumba ndogo kadhaa. Na kwa kweli ndoa na familia ni moja ya chagizo kali za kuwafanya VIONGOZI wetu wawe wezi, mafisadi. Angalia mtu kama Mkapa alivyovurugwa na fisadi Anna na EOTF yake. Muangalie Ridhiwani anavyomchafua Kikwete sasa na utajiri usioelezeka. Angalia mzee Kingunge na utajiri wa kijana wake Kinje. Angalia Lowasa na Fred wake. Angalia Daniel Yona na vijana wake.
Kwa akina mama walivyo na nguvu nyingi siku hizi kwenye ndoa, ni bora tu tupate Rais bachela.
 
Ndoa inatowa picha ya reliability ya huyo mtu (ingawa sio cases zote); Huwezi fananisha reliability na comittment ya Mwanaume/Mwanamke ambae yupo ndani ya ndoa na yule ambae ni nje ya ndoa hasa kwa mambo ambayo ni ya msingi katika maisha ya kila siku. Na hio ndio ilikuwa inamsumbua sana Mzee Slaa katika kusafisha kashfa ambazo zilikuwa zikurushwa kwake dhidi ya tuhuma za kuishi na kimada badala ya mke na watoto.
 
Kinachoongoza ni akili ya mtu na si utupu wake. Unless kama kuna tafiti zilizofanyika kuthibitisha kuwa ubungo wa binadamu siku hizi upo kwenye utupu.
 
kabisa family life or marriage life is important to society...maana ukiwa kama kiongozi ndio unatakiwa uwe mfano kwa jamii...sasa kama mtu ukok solo unakaa ikulu matokeo yake utaanza kuwaingiza akina wema sepetu ikulu sasa kama baadhi ya viongozi tunawaona wanavyofanya bt ikulu au sehemu ya heshima inatakiwa kiongozi awepo pale na familia yake...Huwezi kuona nchi ka america or britain kiongozi yuko solo
Kule Marekani na Uingereza VIONGOZI wanaongoza kwa mujibu wa SHERIA. Wanaongoza kwa mujibu wa KATIBA zao. Hapa kwetu ukiwa na mke na watoto wenye nguvu wanakuwa WABIA wako kwenye URAIS. Wanakusaidia kuteua. Wanakusaidia kutawala. Wanakuandalia hotuba. Wanakulazimisha kuiba. Wanakuingiza kwenye madili ya ajabu. Unafanya biashara hadi IKULU yetu.
 
Back
Top Bottom