Come back Kikwete: Uliwezaje kufanya yote haya?

Come back Kikwete: Uliwezaje kufanya yote haya?

Nawasalimu kwa jina la Muumba wana jamvi.

Ndugu zangu ugumu wa maisha umenifanya niwakumbuke viongozi hawa mahili waliowai kuliongoza taifa letu kwa mafanikio makubwa sana.

Miaka ya kwanza ya utawala wa kikwete na waziri mkuu Lowasa maisha yalikuwa safi maendeleo yalionekana shule za kata zilijengwa wanafunzi wa elimu ya juu walipata mikopo fursa za uchumi zilifunguliwa apa rejea bodaboda, kuanzishwa kwa izi tigo pesa, m pess na nyingine watu walipata ajira walimu wote walikuwa wanapata ajira bila matatizo barabara zilijengwa kwa kasi nk.

Wakati huo nilikuwa namkubali sana Lawasa na Kikwete adi Lowasa anajiuzuru niliumia sana ila baada ya kuaminishwa kuwa ni fisadi niltokea kumchukia sana.

Kumchukia Lowasa kulinifanya nifanye makosa makubwa sana ktk uchaguzi uliopita kwa kumchagua bwana yule anayetaka watu tuishi kama shetani. Nilikuwa na imani kubwa sana juu ya bwana yule kuwa atatuvusha apa Kikwete alipotuacha kumbe nilkosea mtu pekee ambaye angetuvusha ni yule nilieaminishwa miaka michache iliyopita kuwa ni fisadi.

Kwenye ili niwalaumu wana siasa wa upinzani na chama tawala kwa kuniaminisha kuwa jamaa ni fisadi kwa interest zao binafsi pia waandishi hawawezi kukwepa lawama hizi.

Niwalaumu CCM kwa kutompitisha Lowasa kutogombea Urais maana kama angepitishwa kule leo tungekuwa tunaishi kama malaika.

Kutoka moyoni kabisa nimewasamehe viongozi hawa wawili Kikwete na Lowasa ata kama waliiba kweli ila wakati wao mambo yalikuwa yanaonekana Mungu awape maisha marefu
Hawa mods cjui wanatumia nn kufikili unawezaje kuunganisha uzi huu unaongelea kikwete na lowasa na uzi unaongelea kikwete peke yake ovyo kabisa yan
 
TIGO NAO WANAPUNGUZA WAFANYAKAZ, HUKU KUNA INTAKE 2 ZA WAHITIM WA UALIM WAPO MTAANI, CRDB WAMEFUTA FAMILY DAY, BARCLAYS TZ WAMEFUTA PARTY YA MWAKA ILA YA KENYA WANAFANYA,
 
Kuajiri
Kujenga barabara
Kuongeza mishahara ya watumishi
Kununua dawa mahospitalini
Kuwalipa wabunge mishahara mikubwa
 
Simply coz alitegemea misaada kutoka nje ko aliweza kufanya hayo na mengine makubwa zaidi
 
Kuajiri
Kujenga barabara
Kuongeza mishahara ya watumishi
Kununua dawa mahospitalini
Kuwalipa wabunge mishahara mikubwa
JK alipokea nchi deni la taifa lilikuwa around 10 trillions lakini hadi anaondoka ameacha deni la around 40 trillions, mkuu bado tu unauliza aliwezaje kufanya yote hayo? Next time jiongeze kidogo
 
JK alipokea nchi deni la taifa lilikuwa around 10 trillions lakini hadi anaondoka ameacha deni la around 40 trillions, mkuu bado tu unauliza aliwezaje kufanya yote hayo? Next time jiongeze kidogo
Kwani huyu kapokea deni sh ngapi na mpaka sasa limefika wapi?? Tena ndani ya mwaka mmoja,twende kwa takwimu sahihi
 
JK alipokea nchi deni la taifa lilikuwa around 10 trillions lakini hadi anaondoka ameacha deni la around 40 trillions, mkuu bado tu unauliza aliwezaje kufanya yote hayo? Next time jiongeze kidogo
Si hivyo tuu, kuna bonds na mikopo mingine haikuwekwaga wazi ambayo ilikuwa ina-mature after 10 yrs hivyo zigo lake anabeba Magufuli sasa hivi.
 
Si hivyo tuu, kuna bonds na mikopo mingine haikuwekwaga wazi ambayo ilikuwa ina-mature after 10 yrs hivyo zigo lake anabeba Magufuli sasa hivi.
Kwa hiyo huyu jamaa yenu hayo maswala yameshamshinda tayari? kwa nini haweki wazi kazi ni kuwahadaa watu kwa matamko yasiyo na msingi.
 
Mbona watanzania mmekuwa wanafiki kiasi hiki?
Mkuu si swala la unafiki napia si m bezi raisi wangu wa sasa kwa utendaji wake nafikiria tu kwa maana niwengi wanayaona maisha ni magumu sana kwa sasa kwakuwa walitarajia mengi ila hayajatokea mapema kama walivo taraji
 
JK alipokea nchi deni la taifa lilikuwa around 10 trillions lakini hadi anaondoka ameacha deni la around 40 trillions, mkuu bado tu unauliza aliwezaje kufanya yote hayo? Next time jiongeze kidogo
Kwa mwaka uliopita serikali imekola trillion 17,kuna mabadiliko yeyote?
 
Mkuu si swala la unafiki napia si m bezi raisi wangu wa sasa kwa utendaji wake nafikiria tu kwa maana niwengi wanayaona maisha ni magumu sana kwa sasa kwakuwa walitarajia mengi ila hayajatokea mapema kama walivo taraji
Mkuu unamaanisha watanzania wanaishi kwa hisia?
 
Mkuu unamaanisha watanzania wanaishi kwa hisia?
Inawezekana kwa maana wengi hufikiri mabadiliko ya kihuduma za jamii pamoja na kiuchumi niswala ambalo huchukua muda mfupi kumbe ni mlolongo wa mambo mengi na utakao husisha kuumiza hisia na maisha kiujumla kwa wachache na kufaidisha wengi ambao huchukua mda kidogo tofauti na matarajio ya watu
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom