COLLAR BOMB ROBBERY: Tukio la wizi wa benki kwa kutumia Bomu lilowaumiza vichwa FBI kwa miaka minne

August 28,2003 saa 8:28 mchana,

Mwanaume wa makamo Brian wells anaingia katika benki ya PNC iliyopo Erie, Pennsylvania akiwa ameshika fimbo fupi ya kutembelea huku akionekana na uvimbe wa ajabu kwenye kola ya shati yake.. Anaelekea moja kwa moja kwa mhudumu wa benki na kumtolea kikaratasi kidogo chenye maandishi

"Gather employees with the vault access codes to vault and work fast to fill a bag with $250000,you have only 15 minutes" (kusanya wafanyakazi wenye mamlaka ya kufungua sehemu salama ya fedha,jaza dola 250000 kwenye begi,una dakika 15 tu)

Mhudumu huyu anamuangalia Brian Wells kwa mshangao, Wells anahisi kama hajaeleweka vizuri,ananyanyua shati lake juu kuonyesha kitu kama chuma cha ajabu alichovaa mwilini mwake, anaachia tabasamu pana huku akisema "it's a bomb mom" (ni Bomu hili mama)

Mhudumu huyu anamwambia Brian Wells kua hakuna njia ya kuweza kufungua sehemu salama ya kuhafadhia fedha(vault) kwa muda ule, anachukua begi la Wells na kuweka dola 8072 alizokua nazo kisha anampa, Wells anazipokea kisha anatoka nje na kuingia kwenye gari na kuondoka...

Baada ya mawasiliano na vyombo vya usalama,ilichukua dakika 15 tu Brian Wells kutiwa nguvuni, akapigwa pingu na polisi, Muda wote alikua anajitetea kwa nguvu kua alishikwa na kundi la watu weusi, wakamvisha hilo Bomu shingoni huku wakiwa wamemshikia bastola, huku wakimuamuru akaibe benki na wakampa muda maalamu la sivyo watalifyatua lile Bomu

"It's gonna go off" (litalipuka) Haya ni maneno ambayo Brian alizidi kuwaambia polisi, hali iliyopelekea polisi kukaa nae mbali huku wakiwa wamemueka chini ya usalama na kupigia simu kitengo kinachohusika na mabomu( bomb squad)..

Mpaka hapa vyombo vya habari vishafika vikirekodi kila kitu kilichokua kikiendelea.. Akiwa chini ya ulinzi Brian anaendelea kulalamika "I have no time left" (sijabakiza muda mrefu)... Kuonyesha alivyo mfanyakazi mwenye nidhamu na kazi, Brian anawauliza polisi kama wamempiga bosi wake kumjulisha kinachoendelea, ghafla Bomu lile linaanza kutoa sauti kuashiria kulipuka, beep... beep...beep.... BOOM!!! Bomu linalipuka linamchana kifuani na kuacha tundu kubwa kifuani mwake, anahangaika muda mfupi na kuaga dunia majira ya saa 9:18 mchana, kitengo cha mabomu kinawasili baada ya dakika tatu Brian Wells kufariki

View attachment 460228
Brian wells akiwa chini ya ulinzi

Polisi wanaanza uchunguzi kubaini ukweli wa hili tukio, waanza kupekua gari la marehemu Brian na kukuta from fimbo fupi ya kutembelea ambayo Brian alionekana akaiingia nayo benki, inabainika hii si fimbo ya kawaida, Bali ni bunduki iliyotengenezwa kwa muundo wa fimbo. Pia watalaamu wa mabomu wanabaini kua Bomu lile limetengenezwa kwa utaalamu wa hali ya juu, hivyo inawapa hofu kua linaweza kua tukio la kigaidi.

Ushahidi mkubwa ni vikaratasi vyenye ujumbe ulioandikwa kwa mkono vilivyopatikana kwenye gari ya Brian Wells. Vikaratasi hivi vilikua na michoro,ramani,maelekezo pamoja na vitisho ambavyo vilimuelekeza Brian jinsi ya kufanikisha tukio zima..

"Follow the rules and live,disobey and die.. The only way to survive is completely cooperate" (fata masharti uishi,kiuka ufe...njia pekee ya kusalimika ni kutupa ushirikiano)
Haya ni maneno yaliosomeka kwenye moja ya vikaratasi hivyo..

View attachment 460231
fimbo ya kutembelea aliyokua nayo Brian ambayo ni bunduki

Polisi wanaanza kufatilia Maelezo Yale na kudhani huenda wakampata aliyesuka huu mpango.. Kikaratasi cha kwanza kilikua na maelekezo kua Brian akishaiba benki aendeshe gari mpaka mgahawa wa Mc Donald, nje pale afunue chini ya kopo la ua atakuta kikaratasi chenye Maelezo yafuatayo. Kabla ya kukamatwa Brian alikua ashatelekeza agizo hili, akapata kikaratasi kingine kilichomuelekeza aende mpaka mtaa wa PEACH Kuna mahali penye miti mengi atakuta kopo lililofungwa Uzi kwa nje hapo atapata maelekezo yanayofata

Lakini Brian akawa ndio ameshashikwa Kabla ya kwenda mtaa wa peach.. Wachunguzi wakaamua waende wao huku,walivyofika wakalikuta kopo lenye lilifungwa Uzi kwa nje,kulifungua wanatahamaki kulikuta lipo tupu, hii inawapa picha kuwa huenda aliyepanga tukio hilo alikua akifatilia tukio lote na akaamua kuja kutoa ushahidi baada ya Brian kushikwa..

Utata mwingine unakuja pale Brian alipokufa akiwa amevaa fulana mbili huku ya juu ikiwa na neno kubwa GUESS!! fulana ambayo ilidhibitishwa hakuenda nayo kazini siku ile na ndugu yake wa karibu akaja kudai kua si fulana ya Brian... Maswali yakazidi kuongezeka, kwanini aliyepanga tukio lile aache maelekezo sehemu za wazi?? Kwanini amchague Brian Wells?? Kuona kesi inakua ngumu ikabidi wawakabithi 'wazee wa kazi' FBI

FBI WANAINGIA KAZINI

Wazee wa kazi wanaingia kazini, cha kwanza wanaipa hii kesi jina "collar bomb case" msako unaanzia mahali wanapouza makaki ya kulisha(pizza).. Sehemu hii ijulikanayo kama Mama Mia Pizza-Pia ndipo hasa Brian wells alipokua akifanya kazi.. Hapa FBI wanapata habari zinazowashtua, Bosi wake Brian Wells(miaka 46) anadai kua Brian ndiye mfanyakazi wake mtiifu, ndani ya miaka kumi alizofanya kazi hapo, Brian alichelewa siku moja tu kazini na ni siku ambayo paka wake kipenzi alikufa.. Siku ile ya tukio,ilipigwa simu na mtu akitaka kuletewa pizza mbili, japokua Brian alikua kamaliza zamu yake alikubali kuzipeleka

Hapa FBI wanapata mwanga,wanaifatilia simu ile na kugundua ilikua ikielekeza mahali pa mafichoni ambapo kulikua na mnara.. Simu ilipigwa kwa kutumia simu za kibandani(booth)... FBI wanaenda mpaka eneo lile lakini hawakuti cha maana cha kuwasaidia, ni mahali tulivu ambapo panafikika kwa njia ya vumbi,karibu na mnara huo anaishi mwanaume BILL ROTHSTEIN, katika kuhojiwa mwanaume huyu anayeongea kwa mbwembwe sana anaonekana kutojua chochote kuhusu hili tukio.. Je inawezekana BILL ROTHSTEIN mwanaume mwenye miaka 59 anayeishi mwenyewe kushikilia siri kubwa nzito????

SEPTEMBA 20,2003 SAA 3:54 ASUBUHI
Haijapita hata mwezi baada ya tukio,Bill Rothstein anainua simu yake na kubonyeza namba 911 kisha anapiga, simu inapopokelewa anasema "At 8645 peach street in the garage, there is a frozen dead body,its in the freezer" (mtaa namba 8645 peach,Kuna maiti iliyoganda,IPO katika jokofu)
Polisi kufika hapa wanapata mshangao mkubwa, mahali ambapo Rothstein Kawaelekeza ni nyumbani kwake, ikabidi wamshike, baada ya mahojiano Rothstein anasema alikua kwenye mfadhaiko kwa wiki mzima,ilifika mahali akatamani kujiua, akawaonesha ujumbe wa kujiua(suicidal note) aliotaka kuuacha ambapo alikua akiwaomba msamaha wote aliokua anawajali na wanaomjali,pia katika ujumbe huo alisisitiza hakuhusika kwa namna yoyote na kifo cha maiti ile ndani ya jokofu... Kosa kubwa sana tena sana alilofanya bwana Rothstein ni kuandika mwisho wa ujumbe wake maneno

"This has nothing to do with the Brian wells's case" (hii haihusiani na kesi ya Brian wells
)

View attachment 460232
rothstein

JIM RODEN, ndiye hasa huyu bwana mdogo ambaye maiti yake imekutwa kwenye jokofu, Rothstein anawambia polisi kua alipokea simu kutoka kwa mpenzi wake wa zamani MARJORIE DIEHL ARMSTRONG ambaye alidai kua kamuua mpenzi wake waliyekua wanaishi nae kisa ugomvi wa fedha, alikua anahitaji msaada wa kufuta ushahidi pamoja na kuutupa mwili, hivyo Rothstein akaenda mpaka kwa Marjorie na wakasaidiana kuiyeyusha bunduki iliyotumika kwa mauaji na kuupeleka mwili kwa Rothstein wakiwa na mpango wa kuuweka kwenye jokofu mpaka ugande kisha wausage na kwenda kuutupa.. Hivyo Rothstein akadai nafsi ilimsuta na alikua akiogopa Marjorie anaweza kumuua na yeye kufuta ushahidi zaidi hivyo akaamua kupiga simu polisi

Rothstein alishafanya makosa kuitamka kesi ya Brian Wells lakini kinachomsaidia ni kua FBI ndio wanashugulikia hii kesi na hawakutilia maanani kesi hii ya kifo cha bwana mdogo Jim RODEN.. Hatimaye mwanamama Marjorie Diehl Armstrong anashikwa na kuhukumiwa miaka ishirini jela.. Mwaka 2004 July Rothstein anafariki kwa ugonjwa wa limfoma(lymphoma)

April 6, 2005 SAA 8:24 mchana

FBI wanapokea simu kutoka kwa askari magereza alipofungwa Marjorie diehl Armstrong akidai mwanamke huyo ana taarifa nyeti kuhusu kesi ya Brian Wells.. FBI hawapotezi muda wanaenda mpaka gerezani kukutana na mwanamke huyu ambaye anawaambia kua wakimuhamisha gereza na kumpeleka karibu na la nyumbani kwao na kumpunguzia miaka katika ile 20 aliyohukumiwa atawaambia kila kitu

Baada ya makubaliano mwanamke huyu anawaambia kua Rothstein(ambaye ashakufa mpaka muda ule) ni muongo na ndiye hasa alikua kiongozi(mastermind) wa kesi ya 'collar bomb'... Anaendelea kuwaambia kua yeye haisuki na tukio lile kwani yeye alimsaidia tu Rothstein kukusanya vifaa vya kutengeneza Bomu, mshtuko mkubwa ni pale anapowaambia FBI kua aliyelipukiwa na Bomu Brian Wells hakua mhanga(victim) wa tukio lile Bali naye alikua mshiriki katika mpango mzima...

Uchunguzi zaidi unaibua mashushushu wa FBI ambao wanakuja na ushahidi kua mwanamke huyu Marjorie alisikika Mara kwa Mara akijisifa kuhusika na tukio lile,pia alisikika akidai alimuua mpenzi wake Jim RODEN maana alishtukia mchezo wote, pia alisikika akijisifu kua yeye ndiye aliyempima shingo Brian Wells... Pia wanaleta mezani mtuhumiwa mwingine wa kesi hii KENNETH BARNES... Mpaka hapa FBI washaelekeza macho yao kwa mwanamke huyu Marjorie, ikabidi wakaangalie kama ana rekodi yeyote ya uhalifu(criminal record)..kuja kufungua faili lake FBI wanapigwa na butwaa...

View attachment 460234
marjorie

Marjorie ana rekodi nyingi za uhalifu, akiwa na miaka 35 alimuua mpenzi wake Robert Thomas kisha akaja kudai alikua akijihami akashinda kesi,miaka minne badae mime wake Richard Armstrong alikufa kifo cha utata,akiwa na jeraha kichwani lakini hapakua na ushahidi wa kutosha kumfunga Marjorie, pia waligundua Marjorie alikua ni mwanamke mwerevu sana hali iliyofanya kuhisi anaweza kua kahusika katika kupanga tukio la collar bomb,cha kushangaza zaidi inabainika Marjorie na mtuhumiwa mpya Kenneth Barnes aliyewasilishwa na mashushushu ni marafiki wakubwa..

FBI inamtafuta Kenneth Barnes ambaye alikua jela pia kwa muda ule kwa kesi ya madawa ya kulevya, anakubali kutoa ushirikiano kwa makubaliano ya kupunguziwa miaka jela, anawapa uhakika FBI kua Marjorie anahusika na mpango mzima wa collar bomb. Anadai walikubaliana fedha watakazopata atapewa yeye kenneth, alafu Kenneth atamsaidia Marjorie kumuua baba yake ili Marjorie aweze kurithi Mali zake.

Kesho yake FBI wanafika kuonana na Marjorie wakiwa na nyuso za furaha,wanamueleza wana ushahidi wote kuweza kumshtaki upya, Marjorie anaonekana kukasirika sana,anaanza kuongea mfululizo,anawaomba akawaonyeshe alipokua siku ya tukio la Bomu, wanaongozana na maafisa wa FBI huku njiani Marjorie akiwa anaongea sana, baada ya safari ile Marjorie anatishia hatotoa ushirikiano tena mpaka watakapompa dili zuri la kupunguza miaka yake jela tena kwa maandishi, maafisa wa FBI wanaangalia usoni kisha mmoja anatabasamu na kusema. "The woman has already told us more than we needed to know" (huyu mwanamke kashatueleza zaidi ya tunayohitaji kuyajua)

Baada ya wiki anajitokeza mwanaumme mwingine ambaye alikua katika mpango ya tukio hili,baada ya kuona wenzake washatiwa nguvuni anahisi hatosalimika, Kabla ya kuongea chochote anaingia makubaliano ya maandishi na FBI kua hatofungwa wala kutajwa iwapo atasema kila kitu,wanakubaliana, Mwanamme huyu anasema kua wahusika walikua Rothstein,Marjorie, Kenneth Barnes na marehemu Brian Wells mwenyewe.

Rothstein ndiye alitengeneza Bomu na alikua hana shida na pesa, bali ni mtu ambaye alikua akipenda sifa na kazi zake hivyo yeye kwake Bomu lake kutumika katika tukio lile aliona sifa tosha

Marjorie alikua akihitaji fedha zile ili ampe Kenneth amuue baba yake ili Marjorie achukue urithi, swali tata linakuja, inakuaje Brian Wells mwanaumme mpole akihusishe na mpango huu hatari? Hapa ndipo huyu mwanaume anazidi kuwashangaza FBI

Brian wells alikua ana uhusiano na kahaba kwa makubaliano kua Brian awe anamletea madawa ya kulevya yule kahaba kisha anapewa ngono kama malipo,hapa ndipo brian wells anafahamiana na Kenneth Barnes ambaye alikua muuza madawa ya kulevya, ikafika muda Brian akawa na deni kubwa la Kenneth hapa ndipo akapewa hili dili, ila Brian aliambiwa kua litatumika Bomu feki na waliandika vile viujumbe ili iwapo Brian akikamatwa basi ajitetee kua alitekwa

Lakini muda ulipofika walimgeuka na kumfunga Bomu la ukweli huku wakiwa wamemshikia bunduki..

JULY 14 2007 SAA 4 ASUBUHI
"Liar, liar , liar " (muongo,muongo,muongo)
Hii ni kauli aliyokua akiitoa Dada yake Brian wells kuelekea kwa Mary Buchanan wakili wa serikali ambaye alikua ameitisha mkutano wa vyombo vya habari na kuwaeleza kua baada ya miaka minne FBI wamepata ufumbuzi wa 'collar bomb case'

Hii ni baada ya Buchanan kusoma ripoti yote na kusisitiza kua marehemu Brian wells awali alikua kwenye mpango wa tukio zima Kabla ya kugeukwa na wenzake na kufanywa muhanga. Marjorie alifungwa maisha, huku Kenneth akipigwa mvua ya miaka 45. Buchanan alisema baadaye walianza kusalitiana wao kwa wao ikianza na Rothstein kumchomea Marjorie kwenye kesi ya kifo cha mpenzi wake.Aliyesalimika alikua marehemu Rothstein ambaye alifariki Kabla ya ukweli kufahamika na hakuwahi kulipa makosa yake..

Mchunguzi wa makosa ya kijasusi wa FBI JIM FiSHER aliifunga hii kesi kwa kutoa maneno yafuatayo kwenda kwa Rothstein

"The son of a bitch ended up winning,he died with the secret, he got the last laugh,he escaped punishment and detention, leaving us with this idiotic bunch of questions"

SOURCE
•FBI RELEASED FILES ON THE COLLAR BOMB CASE

Kwa wapenzi wa filamu,kisa hiki utakipata chote kwenye filamu ya 30 MINUTES OR LESS
Weekend njema wadau.

~Mark pawelk~
30 minutes or less kitu kama nilishaona hii movie ila sina uhakika kama ndo yenyewe ila storyline ina modification kidogo

Actor ni yule jesse heselberg wa kweye now you see me

Ila safi sana mkuu kuna watu dunia hii wana akili za ajabu wana plan ambazo ukifkiri mpaka kichwa kinauma
 
unasoma makala hadi unahisi kama ndo unautangazia uma mbele ya waandishi wa habari. imekaa poa mkuu
 
30 minutes or less kitu kama nilishaona hii movie ila sina uhakika kama ndo yenyewe ila storyline ina modification kidogo

Actor ni yule jesse heselberg wa kweye now you see me

Ila safi sana mkuu kuna watu dunia hii wana akili za ajabu wana plan ambazo ukifkiri mpaka kichwa kinauma
Hio movie waliitengeneza based na hii collar bomb ROBBERY case, ni movie tamu sana
 
  • Thanks
Reactions: 314
Mkuu Asante kwa kunitag shida mpaka muda huu sijapata notification ila sio mbaya nilikuwa tuko Pamoja mkuu
 
Duuh nimekumbuka novels za James Hardley Chase....
 
Bonge La Hadithi, the bold pitia huku ila naomba na mimi unitag kwa stori kali zaidi
 
Safi sana mkuu, kumbe hawa jamaa wakishahitimisha kesi zao ndio huandika tukio zima na kuliachia mtandaoni!

Sijui kama hapa kwetu wana utaratibu huu ila ingependeza sana kama wangeiga, watu tungepata kujifunza mengi.
Hawa wa kwetu hovyo wetu wanawaza kubambikia watu makesi mazito mazito ukiwa bado mjanja unabambikwa na AK47 iliyofanya matukio makubwa huko nyuma mpk huonekane huna hatia ulishakaa jela miaka 15

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom