Baada ya Wakili fake kutiwa mbaroni, Daktari fake akamatwa, amekuwa akitibu kwa miaka 16

ChoiceVariable

JF-Expert Member
May 23, 2017
43,124
49,844
Hakuna Nchi Ina vituko kama Kenya

---

David Nyawade kutoka nchini Kenya ameingia matatani baada ya kugundulika kuwa ameifanya kazi ya udaktari kwa zaidi ya miaka 16 huku akiwa hana taaluma ya fani hiyo nyeti ulimwenguni

Daktari huyo anayetajwa kuwa feki katika wasifu wake inaonesha kuwa alisoma Chuo Kikuu cha Makerere kwa masomo yake ya shahada ya kwanza na baadaye alisoma katika Chuo Kikuu cha Stanford mnamo 2020, akibobea katika upasuaji wa mishipa.

Baraza la Madaktari na Madaktari wa Meno nchini humo (KMPDC) limethibitisha kuwa hakuwa na taaluma hiyo na limefikia uamuzi wa kuifungia leseni yake.

"Wagonjwa wanashauriwa kutopata huduma za David Nyawade Onyango"ilisema sehemu ya taarifa ya KMPDC.

Kwa upande wake, Afisa Mtendaji Mkuu wa KMPDC, Dkt David Kariuki, amesema baada ya uchunguzi wa kina waligundua kuwa baadhi ya nyaraka alizokuwa nazo Nyawade ni feki.

Hili si tukio la kwanza la kukamatwa kwa watumishi feki nchini Kenya Nyawande anashukiwa baada ya kupita siku kadhaa tangu mamlaka nchini humo zimshikilie Brian Mwenda, anayedaiwa kuwa wakili feki ambaye kwa zaidi ya miaka kumi amekuwa akijitambalisha kama Wakili wa Mahakama Kuu ya Kenya huku akishinda kesi zote 26 alizozisimamia.
 
Back
Top Bottom