Dua Saidi Linyama, ahukumiwa kifungo cha miaka saba jela kwa kukutwa na silaha (bomu), kinyume cha sheria

Roving Journalist

JF Roving Journalist
Apr 18, 2017
2,812
11,987
SHURA YA MAIMAMU TANZANIA

MMOJA KATIKA KESI ZA MASHEIKH AFUNGWA JELA MIAKA 7, LEO JUMATATU TAREHE 4/12/2023.

Mwishoni mwa juma lililopita Waislamu 7, wanaotuhumiwa na Serikali ya Tanzania kwa Ugaidi walifikishwa Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam.

Wao ni sehemu ya wenzao 82, waliobaki katika Gereza Kuu la Ukonga Jijini Dar es Salaam kwa zaidi ya miaka 9, sasa.

Walipofikishwa mahakamani tarehe 01/12/2023, sita kati yao wailiachiwa huru na mmoja hukumu yake iliakhirishwa.

Wale sita walioachiwa huru walikamatwa tena na Polisi palepale Mahakamani na yule mmoja alirejeshwa gerezani.

Aidha yule aliyerejeshwa gerezani Bwana Dua Saidi Linyama, leo alipelekwa mahakamani na kuhukumiwa kifungo cha miaka saba jela kwa madai ya kukutwa na silaha (bomu), kinyume cha sheria.

Tukio la Bwana Dua lilianza tarehe 26/8/2015, jioni akiwa katika shughuli zake alikamatwa na kikosi maalum cha usalama na kwenda naye kituoni kwao.

Kisha siku hiyo hiyo walikwenda naye katika nyumba alipokua anaishi Tegeta Mivumoni na kuingia naye chumbani kwake.

Baada ya hatua hiyo walitoka na kurudi naye kituoni kwao. Kabla ya kuondoka naye, wakazi wote wa nyumba hiyo waliamriwa kuhama kwa muda, na kisha nyumba hiyo ilizungushiwa utepe maalum na kuwekwa chini ya doria ya Polisi.

Siku ya piliyake (tarehe 27/8/2023), Polisi wakiwa na Bwana Dua, walikwenda kwa Mwenyekiti wa Serikali ya Mtaa kisha kwa pamoja wakenda hadi nyumbani kwa bwana Dua na kumuacha kwa muda ndani ya gari akiwa chini ya ulinzi.

Askari na Mwenyekiti waliingia chumbani kwa Dua na baada ya muda walimchukua wakaingia naye chumbani kufanya upejuzi na kukuta kitu walichodai ni bomu.

Hivyo ndivyo ‘bomu’ la ‘Ugaidi’ wa Bwana Dua lilivyopatikana.

Pamoja na Polisi kupata hicho kinachoitwa ushahidi uliomtia bwana Dua hatiani, lakini mtu huyo wamekaa naye gerezani kwa zaidi ya miaka 8, wakidai wanatafuta ushahidi.

Kuhusu Masheikh sita waliochukuliwa na Polisi, baada ya Shura ya Maimamu Tanzania, kufuatilia kwa kina wameachiwa leo kwa utaratibu wa jeshi la Polisi Tanzania, wanaouita ‘dhamana’(yaani mtu anawekwa chini ya ulinzi bila ya kutamkiwa tuhuma na mwisho anadhaminiwa bila ya kutamkiwa tuhuma).

Dhamana hiyo imetolewa kwa masharti matatu. Lakwanza watuhumiwa hao kudhaminiwa na nduguzao. Pili wataripoti kituo Kikuu cha Polisi kila baada ya siku thelathini. Na tatu wataomba kibali cha Polisi kila wanapotaka kusafiri nje ya mkoa wa Dar es Salaam.

Aidha Shura ya Maimamu Tanzania inajiandaa kukata rufaa dhidi ya hukumu ya miaka saba iliyotolewa leo kwa Bwana Dua Saidi Linyama.

KATIBU MKUU SHURA YA MAIMAMU TANZANIA
 
Mbona kama ushahidi ni wa kupandikizwa?

Hakimu au Jaji aliyeamua kesi hii anaonesha amepokea maagizo
 
Kuna jambo hatulijui ila waendelee kukaa huenda ni mnyaazi anawajaribu hakuna udini hapo maana kuna viongozi wa kiislamu wameshapita na wangeweza kuongelea hilo ila walipiga kimya wakijua kuna jambo ngoja tuone litaishia wapi japo familia zao zinateseka sana kuona wapendwa wao wapo ndani huenda bila makosa au wanamakosa hapo mwananchi wa kawaida hawezi jua....

Kama ni magaidi kweli wafungwe tu maana uta picha msongamano kama ule wa kkoo sikukuu mtu mmoja aende na watu 300 ni kitu kisicho kubalika
 
Back
Top Bottom