Clouds yaipotezea UKAWA

Clouds yaipotezea UKAWA

Hata ningekuwa mimi ningewapotezea vilevile maana hawana maana kabisa ila ni walafi wa madaraka tu....wanafanya hivi ili walazimishe kuundwa serikali ya mpito ya umoja wa kitaifa ili tu waingie madarakani kwani wanajua fika kuwa kwenye ballot hawapenyezi...

Kwanini hawapenyi inashindikanaje😎 kwa uelewa wako kama nyooka unafikiri wanauchu wa madaraka?! Kweli hamnazo
 
Nikiwa katika foleni kuelekea kuwajibika, napenda kusikiliza uchambuzi wa magazeti kutoka ktk radio tofauti tofauti.

Nimefungulia radio clouds, wakati Paul James (PJ) akichambua magazeti walipofikia kusoma habari ya Ukawa, Barbara Hassan akamwambia PJ hawa tuwapotezee maana wao wametupotezea.

Badala ya kurudi bungeni kusimamia tupate katiba nzuri wameamua kutupotezea basi nasi tusiwape kichwa tuwapotezee.
Kauli ambayo imeungwa mkono na PJ na Mbwiga na kuendelea kusoma habari zingine.

Hii inaonyesha ni kiasi gani wananchi wamekereka na ukawa waliokuwa wanawategemea kuleta changamoto kubwa ktk bunge la katiba hatimae kupata katiba nzuri.

Je maamuzi yao yametokana na uchanga wa uzoefu ktk siasa hasa katika mambo makubwa kubwa kama katiba kwa kutojua athari zake?

Au ni kususa baada ya kuona matumaini yao kuona yamepotea ya kuivunja Tanzania?

Maana kama ni kuleta machafuko hilo wasitegemee maana waTanzania hatujakulia katika mazingira hayo??

Nawasilisha.

Rich Pol acha kuushangaza umati..unaposema wananchi wanaichukia ukawa unaongea wananchi gani??kama ni wakina Wasira,Sita,Nchemba na baadhi ya viongozi wa CCM sawa..ila ujue kua hata hao wanachama wa CCM baaadh wanaishangilia ukawa kila kukicha kwa kuyamulika yale ambayo wao wameshindwa kuyamulika kwakua wapo ndani ya CCM....Unapokuja kutuelezea maoni ya wachumia tumbo wa clouds hapa ambao tunajua sababu ya kushabikia CCM ntakushangaa sanaa...eti mbwiga,PJ,Babraa..embu waulize huwa wanatumia mda wao kufatilia mambo ya katba pamoja na kusoma rasimu ya warioba ilivyo watakwambia hapana zaid ya kufatilia mambo hayo kwenye magazetu ya uhuru..wakati mwingine muwe manapost mambo ambayo yanaeleweka hata km umetumwa ku post sio uonekane -------- hata na wapumbavu...
 
Mtoa mada nimefurahishwa na hii mada leo kwani hata mimi wakati huo wa asubuhi nilikuwa kwenye foleni nikielekea kibaruani. binafsi navutiwa sana na ubunifu wa kimatangazo wa clouds FM ila kuna kitu ambacho mara nyingi sana wanakosea. Tanzania imekuwa nchi ambayo kil mtu anaweza kuzungumza kila kitu hata kama hana uelewa nacho. Wageiga mfano wa redio one na nyinginezo ambazo issue kama hizo huwa hawachukui upande wowote. Clouds FM Radio imekuwa na muonekano wa Ki CCM sana na mara nyingi wako upande wa serikali na chama tawala hata kwa mabo ya kipuuzi. Kwa kweli mnaboa sana maana hicho kitendo ni sawa na kukashifu mawazo na maoni ya watu wengine ambao wana mitazamo tofauti. Si vizuri kuleta mitazamo yako binafsi na kuizungumza kwenye vyombo vya habari kama vile ndio mawazo ya kituo au ya walio wengi.... CLOUDS FM mnanikera sana kwa hilo na sijui kwanini hambadiliki.....
Nikiwa katika foleni kuelekea kuwajibika, napenda kusikiliza uchambuzi wa magazeti kutoka ktk radio tofauti tofauti.

Nimefungulia radio clouds, wakati Paul James (PJ) akichambua magazeti walipofikia kusoma habari ya Ukawa, Barbara Hassan akamwambia PJ hawa tuwapotezee maana wao wametupotezea.

Badala ya kurudi bungeni kusimamia tupate katiba nzuri wameamua kutupotezea basi nasi tusiwape kichwa tuwapotezee.
Kauli ambayo imeungwa mkono na PJ na Mbwiga na kuendelea kusoma habari zingine.

Hii inaonyesha ni kiasi gani wananchi wamekereka na ukawa waliokuwa wanawategemea kuleta changamoto kubwa ktk bunge la katiba hatimae kupata katiba nzuri.

Je maamuzi yao yametokana na uchanga wa uzoefu ktk siasa hasa katika mambo makubwa kubwa kama katiba kwa kutojua athari zake?

Au ni kususa baada ya kuona matumaini yao kuona yamepotea ya kuivunja Tanzania?

Maana kama ni kuleta machafuko hilo wasitegemee maana waTanzania hatujakulia katika mazingira hayo??

Nawasilisha.
 
Nikiwa katika foleni kuelekea kuwajibika, napenda kusikiliza uchambuzi wa magazeti kutoka ktk radio tofauti tofauti.

Nimefungulia radio clouds, wakati Paul James (PJ) akichambua magazeti walipofikia kusoma habari ya Ukawa, Barbara Hassan akamwambia PJ hawa tuwapotezee maana wao wametupotezea.

Badala ya kurudi bungeni kusimamia tupate katiba nzuri wameamua kutupotezea basi nasi tusiwape kichwa tuwapotezee.
Kauli ambayo imeungwa mkono na PJ na Mbwiga na kuendelea kusoma habari zingine.

Hii inaonyesha ni kiasi gani wananchi wamekereka na ukawa waliokuwa wanawategemea kuleta changamoto kubwa ktk bunge la katiba hatimae kupata katiba nzuri.

Je maamuzi yao yametokana na uchanga wa uzoefu ktk siasa hasa katika mambo makubwa kubwa kama katiba kwa kutojua athari zake?

Au ni kususa baada ya kuona matumaini yao kuona yamepotea ya kuivunja Tanzania?

Maana kama ni kuleta machafuko hilo wasitegemee maana waTanzania hatujakulia katika mazingira hayo??

Nawasilisha.

Je, kama ukawa nao wakiamua kupiga kampeni ya kusema wananchi wanaowaunga mkono waipotezee clouds kama wanavyotaka wao,watabaki salama?

Mi nadhan clouds wangeondoa msemo wao wa radio ya watu kwani kiuhalisia si radio ya watu tena.Ni redio ya ccm!
 
Nilikuwa nasikiliza hii radio lkn nikaanza kujipunguza taratibu, nikabaki na magazet kwa asubui, ushauri wangu ws bure sikilizeni east Africa radio asubuhi mkiwa mnaenda kwenye mihangaiko yenu, awamlishi msikilizaji sumu

Mapinduzi ya EATV yanahamia EA radio sasa ......mimi jioni nasikiliza EA radio ....good music na habari serious si mizaha ya kitoto na matangazo meeeeeeeeeeeeengi ..............

Issue si Clouds kupendelea upinzani bali wafanye kazi ya kuhabarisha na kuchambua ikibidi kwa kuhoji watu wenye misimamo tofauti ili waendelee kubaki na wasikilizaji wanaoamini watapata habari za pande zote ......

BTW Kusaga hana cha kupoteza sasa hivi ............ hajali .....hataki kuwaudhi "wakubwa" tu ......😛eep:
 
Kwa uwezo wako mdogo wa kufikiri Babla, Mbwiga na PJ ndo maoni ya wananchi????

Swali zuri sana, mleta mada uwezo wake wa kuchambua mambo mdogo sana. Yani mtazamo wa mtangazaji anadhani ndo maoni ya wananchi!!! This is terrible
 
yan mleta uzi mwnyw anaonesha biasnes. Lakin sikulaum labda pengine hujui vizur media n journalism proffssn. Walichofanya babra na pj ni udhalilishaji wa taaluma nzima ya habari tanzania, siimzungumzii mbwiga coz ni mbigaa kama jina lake. Pj ana B.a ya masscomm ya tumain unvrsty nmemshangaa sana kusupport ujinga alioukua anauongea babra eti UKAWA wanapowasoma wanawapa kiki!!! sijui elimu yake babra hassan vizur, lakin kumbe anaezafanya kipnd cha mariam wa migomba au dida!! NI BORA HABARI WASINGEISOMA KABISA KULIKO KUSEMA ON AIR VILE THAT WAZ LACK OF PROFFESIONALISM INDEED!! MASOUD MASOUD aliwai sema zamani kulikuwa na radio presenters ila siku hizi kuna presenters tuu. Presenters hawajui ethics hawaijui taaluma, hawajui doctrine of separation!! Wao wanachojua kuongea nyuma ya mic tuu. Inauma na inakera sana.
 
Mapinduzi ya EATV yanahamia EA radio sasa ......mimi jioni nasikiliza EA radio ....good music na habari serious si mizaha ya kitoto na matangazo meeeeeeeeeeeeengi ..............

Issue si Clouds kupendelea upinzani bali wafanye kazi ya kuhabarisha na kuchambua ikibidi kwa kuhoji watu wenye misimamo tofauti ili waendelee kubaki na wasikilizaji wanaoamini watapata habari za pande zote ......

BTW Kusaga hana cha kupoteza sasa hivi ............ hajali .....hataki kuwaudhi "wakubwa" tu ......😛eep:
Tumieni hata akili zenu basi msitumie za kuambiwa tu kwa mfano ukienda pale ubungo au mwenge hata hapa dodma uanze kuhoji watu unajuaje kuwa huyu msimamo wake ni tofauti make mimi nijuavyo unahoji kwanza halafu misimamo yao utajua baada ya kujoji.
 
Hiyo radio bado ipo??? kuwajadili humu ni kuwapa kick tu kwanza p ya ishashuka zamani sana
 
Hao nao watangazaji au wasemaji WA redioni. Wenhe akili timamu woote wanafagilia UKAWA wenye mtindio WA ubongo au waliopata matatizo ya akili na kufumaa. Viva ukawa aluta continue
 
Na Karoli Vinsent
SAA chache kupita Baada Radio ya
Clauds Fm kutangaza Rasmi
kutozisoma Habari zozote
zinazowahusu Wajumbe wanaunda
umoja wa Kutetea Katiba ya
Wananchi UKAWA, kwa kile
wananachodai Umoja huo hauna
jipya bali unataka umaharufu tu.
Kauli hiyo ya ambayo
inakwenda kinyume na Maadili ya
Vyombo vya Habari imetolewa leo na
Mtangazaji wa Kipindi cha Power
breakfast Babla hassani wakati
wakichambua magazeti ya siku
ambapo alisema kwa sasa
hawatazisomi habari zozote
zinazohusu umoja huo wa Ukawa kwa
madai umoja huo ni wabinafsi na
hawana jipya bali wanataka
Umaharufu.
Naye Mwanasheria wa Umoja
wa kutetea katiba ya Wananchi
UKAWA ,Tundu Lissu amewavaa na
kusema Radio hiyo inajimaliza na
ndio itakuwa inaonekana wazi
inapendelea Upande moja Kisiasa.
Kauli hiyo Tundu
Lissu,ameitoa mda huu wakati
alipokuwa anaongea na Mwandishi
wa Mtandao huu,Kuhusu wao Ukawa
wamepokeaje Taarifa hiyo ya
kutosomwa Habari zao kwenye Radio
hiyo.Ambapo Lissu alisema hizo
taarifa anazisikia na kama ni kweli
wametangaza hivyo watakuwa
wamejimaliza.
“Kwanza nimezisikia hizo
taarifa na kama kweli aliyosema huyo
mtangazaji ndio msimamo wa Radio
nzima basi watakuwa watu wa Ajabu
sana maana leo Nchi nzima habari ya
Mjini ni Ukawa,leo utasemaje ukawa
ni wabinafsi wakati wasomi na watu
wengine wanaungana na sisi leo
inakuwaje Radio hiyo iseme hivyo
kama wako upande mmoja wa
Kisiasa weseme”alisema Lissu.
Tundu Lissu,ambaye naye ni
Mjumbe wa Bunge maalum la Katiba
alizidi kusema yeye sio mwanahabari
bali anachokijua huo utakuwa
msimamo wa Radio nzima na wao
Ukawa hawata ogopa na kuacha
kuwatetea wananchi kwani wako kwa
ajili ya kuwakomboa wananchi na
hawezi kukatishwa na tamaa na watu
wachache wenye maslai ya upande
mmoja.
“Harafu inashangaza sana
leo nchi nzima inazungumzia Ukawa
harafu mtua aseme leo Ukawa
utotangaza habari zao kwa misingi
hipi?”alihoji Tundu lissu.
Kauli hiyo ya Tundu
Lissu,imetolewa saa chache kupita
baada Mtangazaji wa kipindi cha
Power Breakfast Babla
Hassani,kutangaza Rasmi kwamba
hawatasoma Habari zozote
zinazohusu Umoja huo.
“Mimi Naona kusoma Story
zinahusu Ukawa tunawapa kiki tu
wao siwamekuwa kutupotezea
kutorejea Bunge I whon doing,vile
vikao vinawanufaisha watanzania
wote wao ni wabinafsi tu,the best
ican do tuwapotezea Habari zao, na
ukiona habari inahusu Ukawa tu
usisome hapa kwenye Redio,na wakae
huko nje atuwataki Ukawa
bungeni”alisema Babla Hassani.
Kauli hiyo ya iliungwa Mkono
pia na Mtangazaji wa mwengine wa
kipindi hicho, Paul Jems
anayejulikana kwa jina la Umaarufu
“PJ” naye alisema kwanzia sasa
hatazisoma habari zozote zinazohusu
Umoja huo kwani wanapoteza pesa
za wananchi bure kwa kususia bunge
hilo.
Msimamo huo wa Watangazaji
hao unakwenda Kinyume na Mmiliki
wa Radio hiyo ya Clauds Fm Joseph
Kusaga alipokuwa anahojiwa na
kipindi kimoja cha runinga kutoka
nchini Uingereza kinachojulikana,The
Sporah Show ambapo katika kipindi
hiko alisema Radio yake haina
upande wowote wa Kisiasa na
kuongeza ni Redio huru inayofanya
kazi bila kushabikia upande wowote.
Lakini kwa sasa kauli ya
Mmiliki hiyo inakwenda tofauti na
ilivyo,na kama Radio ikifanya kama
inavyofanya hivyo kwa sasa,Basi
Redio hiyo itapelekea machafuko
makubwa kama yaliyowai kutokea
nchini Rwanda na kuua maelfu ya
watu,na sababu kubwa ni Radio za
nchini humu zilikuwa na misimamo
kama walioyonayo Clauds.
Umoja huo wanaupinga wa
Ukawa unaundwa na Muunganiko wa
Vyama vikuu vya Upinzani ikiwemo
Chama cha demokrasia na
Maendeleo CHADEMA,Chama cha
wananchi CUF,Chama cha Mageuzi
NCCR,ND pamoja na Baadhi ya
wajumbe 201 walioteuliwa na Rais
Kikwet e.
Umoja huo umegoma kurejea
kwenye Vikao vya Bunge la katiba kwa
madai rasimu inayotokana na Maoni
ya wananchi kuchakachuliwa,na
kitendo hicho cha Ukawa kimeungwa
mkono na wananchi mbalimbali
wakiwemo Viongozi wa Dini pamoja
wajumbe wa iliyokuwa tume ya Jaji
warioba.
source full habari blog.
 
Duh huyo mwehu aliye ongea kama anajuwa vichwa vya watanzania vinawaza nini aendeleye kushangilia kama hajuwi basi awatake radhi mara moja ili asije jutia siku aliyo zungumzia hivyo!
 
umaharufu na harafu ndio nini?

G.
mzee upo???walikuzingizia umekufa....
CC:Dinazarde
[h=3]Napenda Kufahamu Wana JF[/h] Started by Dinazarde, 9th June 2014 16:05
Kuna uzi nimeuona wa kuwakumbuka waliofariki mle ndan ya uzi kuna post inasema kua [URL="https://www.jamiiforums.com/member.php?u=128624"]Gogle
amefariki pia kuna uzi ulitolewa wa kuhusu kifo chake kua alizikwa kisutu.

Mwenye kujua atuambie maana wengine hatufahamu kama ni kweli inasikitisha sana namuomba utafiti pia na wengine mnaojua
Tutammiss sana Gogle
[/URL]
 
Back
Top Bottom