Ajenda ya wapinzani hasa CHADEMA ni nini?

Ibambasi

JF-Expert Member
Jul 25, 2007
9,284
4,688
Tangu Rais John Pombe Magufuli aingie madarakani, vyama vya upinzani, hasa CHADEMA (kwa sababu vingine ni viko kwenye hibernation), kama ilivyotarajiwa, vilianza na vinaendelea na ukosoaji (upingaji?) dhidi ya utawala wa Magufuli. Binafsi, nakiri wazi kabisa mpaka leo hii sijapata kuelewa nini hasa ni agenda za CHADEMA (isomeke upinzani) kwa sasa.

Walianza na kupinga bunge kuoneshwa kwenye runinga wakisema ni kuminya uhuru wa habari. Bahati mbaya wapinzani hawa hawakusema ni kfungu kipi cha sheria kinasema lazima matukio ya bunge yaonekane “live” kwenye runinga. Wakati mjadala huo ukiendelea, zikaibuka harakati za kile kilichoitwa Umoja wa Kupinga Udikteta Tanzania (UKUTA) wakidai utawala wa sasa ni wa kidikteta. Sijajua nini vilikuwa vigezo vyao vya kufikia maamuzi hayo. Kama ilivyotegemewa Magufuli alisema hajaribiwi na maandamano yakayeyuka siku mbili kabla. Baadaye likaja suala la Mkurugenzi wa Sera na Utafiti wa CHADEMA, Ben Saanane kudaiwa kutekwa na serikali na kufichwa kusikojulikana. Wapenzi wa CHADEMA wakaandaa mpaka fulana ambazo ziliuzwa kwa bei ya Tshs. 10,000/- za #bringbacksaanane#. Hilo nalo limetupwa kapuni.

Hatujapumzika likaletwa suala la njaa. Hapa sasa mpaka vyombo vya habari vikaingilia kati, kwamba ng’ombe wanakufa, wananchi wanakufa njaa, hali ya chakuwa ikidaiwa kuwa mbaya sana. Kuna muda nilisikia Radio Clouds wanamuhoji kiongozi mmoja huko Rorya akisema kwa muda huo walikuwa wanategemea chakula kutoka Kenya. Lowassa akasema alikuwa anaenda nje ya cnhi kukusanya misaada ya chakula (kwwnye 2007 hivi alwahi kwenda Thailand kuleta mvua ya kutengeneza, kujaza bwawa la Mtera, sijui ilifikia wapi) Magufuli akasema njaa hakuna na kila mtu alime kwa kuwa hali ya mvua ilikuwa inatengemaa. Kelele za njaa zikapotea na hakuna tena taarifa za watu kufa njaa. Likaja suala la uchaguzi wa chama cha Mawakili. Hiuli nalo likawa agenda ya CHADEMA ati kwa vile tu Lissu alikuwa mgombea. Magazeti ikawa ni kila siku uchaguzi. Hawakutuambia rais wa TLS ana mustakabali gani na maisha ya watanzania.

Likaja suala la vyeti vya Makonda. Hili, ni wazi lilitokana na Paul Makonda kumtaja Freeman Mbiowe katika uhusiuka wa mihadarati, pamoja na vigogo na wafanyabiashara wakubwa na viongozi wa dini (Gwajima). Hapa sasa moto ukawa mkali kidogo, Gwajima na Mange (kwa support kubwa ya CHADEMA) wakidai makonda hakufaulu kidato cha nne na anatumia vyeti visivyo vyake. Wakaunganisha hoja hii na msimamo wa Magufuli wa kupambana na watu wanaotumia vyeti visivyo vyao. Ajabu ni kwamba Mange na Gwajima wanatoa tuhuma dhidi y Makonda wakimtaka athibitishe kuwa ana vyeti. Wakasahulisha kwamba anayetoa tuhuma ndiye mwenye wajibu wa kuthibitisha. Isitoshe hakuna mamlaka yoyote ile iliyosema Makonda hana vyeti au anatumia vyeti visivyo vyake. Mashambulizi yakahamia kwenye utu wa Makonda na makisha yake binafsi, mpaka nay a familia yake kutoka kwao. Mapambano haya yakawa kwenye mitandao, ambayo kimsingi ni “cyber-bullying”. Yote ni kumpatia pressue Magufuli amuondoe Makonda. Wakasahu kwamba Serikali haiendeshwi kwa taarifa za mitandaoni pasi na ushahidi thabiti. Magufuli akasimamia kwake na siku ya uzinduzi wa ujenzi wa “flyovers” akaweka wazi msimamo, Makonda chapa kazi.

Likaja suala la “uvamizi” wa Clouds Media. Hili sasavyombo karibu vyote vya habari vikaungana kumsulubu Makonda (actually Magufuli). Ni mara ya kwanza kushuhudia wapinzani na mahasimu wa kibiashara (Radio One/ITV, E-FM & Clouds) wameungana. Hii ni kwa vile maslahi yao yameguswa kwa njia moja au nyingine na Makonda au utawala wa Magufuli. Nape naye kwa vile Makonda alimtaja Wema kwenye sakata la mihadarati, ama kwa kujua au kuchotwa akili na “wajanja” wachache, akaunda Tume yake, (sijui kwa sheria ipi) kuchunguza tukio la “uvamizi”. Suala ambalo, kama lilikuwa kweli, lilipaswa kuwa suala la jinai Nape akalifanya lake. Wakati akijua msimamo wa Magufuli kuhusu Makonda, Tume ikafanya kazi chini ya saa 48 na kutoa taarifa Makonda akitiwa hatiani bila kusikilizwa. Sijui mpala leo kama Clouds waliwahi kusajili Polisi “uvamizi” huo kwa ajili ya upelelezi wa jinai.

Magufuli akafanya mabadiliko madogo ya baraza lake, ambapo Prof. Kabudi akawa Waziri wa Sheria na Dr. Mwakyembe akapelekwa Habari na hivyo kufanya Nape awe nje ya baraza. Nape huyu au vuvuzela kwa jina ambalo chadema waliompatia, akageuka shujaa na msema kweli na mwenye msimamo (rejea twits za Zitto Kabwe na wanachadema wengine). Nape aliyelalamikiwa kuzuia mBunge “live” (hata taarifa yke ipo) akaitwa mtetezi wa uhuru wa habari! Siku ya pili tangu mabadiliko madogo yafanyike akataka naye kufanya press conference kumjibu aliyefanya mabadailiko. Mkutano haukufanyika na tukio hilo likawa habari kubwa sana (kwa sababu za wazi). Tukaambiwa Kinana (Katibu Mkuu) wa CCM angeongea yake ya moyoni, CHADEMA na wapinzani wa Magufuli wakashangilia sana. Kinana hakuongena na mambo yakaishia hapo. Juzi tukamuona Mnyika akitoa tamko la kudai sababu za Magufuli kumuondoa Nape. Inashangaza sana, maana wakati anateuliwa hawakuomba sababu na zaidi walipinga uteuzi wake.

Limekuja suala la mchanga wa dhahabu. Kilio cha wapinzani na watanzania kwa jumla ni kuwa wachimbaji wa madini wanatupunja sana. Nakumbuka miaka ya 2008-9 Rais Kikwete aliunda Tume na Zitto akawa mmoja wa wajumbe. Tume hii lifanya kupitia mikataba ya uchimbaji madini ingawa matokeo yake hayakuwa ya kuridhisha sana. Ni Zitto huyu huyu, wakati huo akiwa CHADEMA alisema mchanga wa dhahbu unaosafirishwa unaipotezea nchi mapato makubwa na kwamba tunahitaji kinu cha kuchambulia mchanga huo hapa nchini. Magufuli ametoa zuio la usafirishaji wa mchanga na wapinzani wake sasa wanalalamika kwamba tujiandae dhidi ya kesi nzito nzito za kuvunja mikataba utadhani walishaiona hiyo mikataba. Kwenye mitandao sasa kumezuka “wachambuzi” wa suala la mchanga, ambao wengi ni wafuasi wa CHADEMA (upinzani) na kitu kimoja wanachokubaliana ni kwamba Rais Magufuli amekosea kuzuia usafirishaji wa mchanga, na kwamba nchi hii haina uwezo wa kuchenjua huo mchanga. Unabaki kujiuliza, wapinzani na watanzania wengine wanataka nini? Wanapinga nini na wanapenda nini?

Kwa sasa imebaki kuwa JK tutakukumbuka daima. Wanajisahulisha ni JK huyu huyu aliyeitwa dhaifu na John Mnyika. Wanadai rais Magufuli anaingilia mihimili na vyombo vingine. Juzi kijana Nay wa Mitego aliimba wimbo wa WOTE akielezea hisia zake kuhusu utawala. Alipokamatwa na Polisi malalamiko yakawa makubwa sana kwamba Magufuli anakandamiza uhuru wa kujieleza. Waziri Mwakyembe jana akatoa taarifa kuwa Rais Magufuli ameagiza kijana huyo aachiliwe huru na wimbo uendelee kupigwa na akimwomba aongeze mashairi kuhusu mambo kama mihadarati, rushwa, ukwepaji kodi, n.k. kibao kimegeuzwa sasa kwa nini Rais Magufuli anaingilia kazi za Polisi na BASATA!

Wakati ule Edward Lowassa amewajibishwa na Tume ya Richmond, mjadala ulikuwa mkali bungeni mpaka Philemon Ndesamburo akasema watu wa aina hiyo (mafisadi) wanapaswa kupigwa risasi hadharani au kunyongwa kama huko China. Malalamiko kipindi cha JK yalikuwa tume nyingi zinapoteza muda, sasa hatuna tume ila maamuzi bila tume wale wale wanalalamika.

Wapinzani wanataka nini? Je wana hoja zozote dhidi ya Magufuli na utawala wake?

Maswali ya kujiuliza:

Agenda kuu za sasa za wapinzani ni nini?

Je katiba mpya iliyopigiwa kelele wapinzani hawa wameridhika kwa yenyewe kuwekwa kapuni?

Kama wao wangeshika uongozi wa nchi hii, ni kipi ambacho wangefanya?

Mtazamo wako nini?
 
Ajenda ya vyama vya upinzani ni kuikumbusha serikali kwamba bei ya sukari imepanda kutoka shs 1,800 kwaka 2014 hadi shs, 3,000 mwaka 2017. Hata wewe mleta hoja unaujua ukweli huu, lakn umejaa unafiki huwezi kusema kweli.
 
Tanzania hatuna upinzani
Tanzania Tuna wahuni wa siasa walio jificha kwenye jina la upinzani!
Kwa anaye Ipenda Tanzania na kuwa ns uchungu na hii Tanzania
Nilazima azidi kumuombea Rais wetu asirudi nyuma
aendelee na msimamo huo huo
lazima kizazi kijacho kimpongeze kwa mema anayo yafanya sasa.
Tanzania tumemptata kiongozi wa ukwelu
kama uhuru wakuamua tumekuwa nao miaka 50 Mbona hakuna jipya!!
 
Hahaha uku kwetu ilipanda toka 2200 mpaka 230
Uko kwenu sjui ni wap
 
AGENDA ya wapinzani sahv ni KUZUIA MAENDELEO Ili serikali ionekane haifanyi kazi
 
Hahaha uku kwetu ilipanda toka 2200 mpaka 230
Uko kwenu sjui ni wap

Acha uongo. Hatukuwahi kununua sukari kwa shs 2,200 kwa kilo katika nchi hii. Na hicho unachosema kufikia shs 230 ni kupanda au kushuka?? acha uongo....
 
Kutumia vyeti feki

Uvamizi wa clouds

Nape kunyooshewa bastola

Uteuzi na utenguzi unaoendelea

Matamko na maelekezo yamekuwa mengi

Hali ngumu ya maisha kwa watanzania

Nakadhalika, nakadhalika
 
Tanzania hatuna upinzani
Tanzania Tuna wahuni wa siasa walio jificha kwenye jina la upinzani!
Kwa anaye Ipenda Tanzania na kuwa ns uchungu na hii Tanzania
Nilazima azidi kumuombea Rais wetu asirudi nyuma
aendelee na msimamo huo huo
lazima kizazi kijacho kimpongeze kwa mema anayo yafanya sasa.
Tanzania tumemptata kiongozi wa ukwelu
kama uhuru wakuamua tumekuwa nao miaka 50 Mbona hakuna jipya!!
Km ulivyokuwa wewe
 
Tafadhali naomba maana ya neno AJENDA, kisha utueleze unajipendekeza kwa nani na kwa maslahi ya nani?
Kisha nikupe majibu.
 
Tangu Rais John Pombe Magufuli aingie madarakani, vyama vya upinzani, hasa CHADEMA (kwa sababu vingine ni viko kwenye hibernation), kama ilivyotarajiwa, vilianza na vinaendelea na ukosoaji (upingaji?) dhidi ya utawala wa Magufuli. Binafsi, nakiri wazi kabisa mpaka leo hii sijapata kuelewa nini hasa ni agenda za CHADEMA (isomeke upinzani) kwa sasa.

Walianza na kupinga bunge kuoneshwa kwenye runinga wakisema ni kuminya uhuru wa habari. Bahati mbaya wapinzani hawa hawakusema ni kfungu kipi cha sheria kinasema lazima matukio ya bunge yaonekane “live” kwenye runinga. Wakati mjadala huo ukiendelea, zikaibuka harakati za kile kilichoitwa Umoja wa Kupinga Udikteta Tanzania (UKUTA) wakidai utawala wa sasa ni wa kidikteta. Sijajua nini vilikuwa vigezo vyao vya kufikia maamuzi hayo. Kama ilivyotegemewa Magufuli alisema hajaribiwi na maandamano yakayeyuka siku mbili kabla. Baadaye likaja suala la Mkurugenzi wa Sera na Utafiti wa CHADEMA, Ben Saanane kudaiwa kutekwa na serikali na kufichwa kusikojulikana. Wapenzi wa CHADEMA wakaandaa mpaka fulana ambazo ziliuzwa kwa bei ya Tshs. 10,000/- za #bringbacksaanane#. Hilo nalo limetupwa kapuni.

Hatujapumzika likaletwa suala la njaa. Hapa sasa mpaka vyombo vya habari vikaingilia kati, kwamba ng’ombe wanakufa, wananchi wanakufa njaa, hali ya chakuwa ikidaiwa kuwa mbaya sana. Kuna muda nilisikia Radio Clouds wanamuhoji kiongozi mmoja huko Rorya akisema kwa muda huo walikuwa wanategemea chakula kutoka Kenya. Lowassa akasema alikuwa anaenda nje ya cnhi kukusanya misaada ya chakula (kwwnye 2007 hivi alwahi kwenda Thailand kuleta mvua ya kutengeneza, kujaza bwawa la Mtera, sijui ilifikia wapi) Magufuli akasema njaa hakuna na kila mtu alime kwa kuwa hali ya mvua ilikuwa inatengemaa. Kelele za njaa zikapotea na hakuna tena taarifa za watu kufa njaa. Likaja suala la uchaguzi wa chama cha Mawakili. Hiuli nalo likawa agenda ya CHADEMA ati kwa vile tu Lissu alikuwa mgombea. Magazeti ikawa ni kila siku uchaguzi. Hawakutuambia rais wa TLS ana mustakabali gani na maisha ya watanzania.

Likaja suala la vyeti vya Makonda. Hili, ni wazi lilitokana na Paul Makonda kumtaja Freeman Mbiowe katika uhusiuka wa mihadarati, pamoja na vigogo na wafanyabiashara wakubwa na viongozi wa dini (Gwajima). Hapa sasa moto ukawa mkali kidogo, Gwajima na Mange (kwa support kubwa ya CHADEMA) wakidai makonda hakufaulu kidato cha nne na anatumia vyeti visivyo vyake. Wakaunganisha hoja hii na msimamo wa Magufuli wa kupambana na watu wanaotumia vyeti visivyo vyao. Ajabu ni kwamba Mange na Gwajima wanatoa tuhuma dhidi y Makonda wakimtaka athibitishe kuwa ana vyeti. Wakasahulisha kwamba anayetoa tuhuma ndiye mwenye wajibu wa kuthibitisha. Isitoshe hakuna mamlaka yoyote ile iliyosema Makonda hana vyeti au anatumia vyeti visivyo vyake. Mashambulizi yakahamia kwenye utu wa Makonda na makisha yake binafsi, mpaka nay a familia yake kutoka kwao. Mapambano haya yakawa kwenye mitandao, ambayo kimsingi ni “cyber-bullying”. Yote ni kumpatia pressue Magufuli amuondoe Makonda. Wakasahu kwamba Serikali haiendeshwi kwa taarifa za mitandaoni pasi na ushahidi thabiti. Magufuli akasimamia kwake na siku ya uzinduzi wa ujenzi wa “flyovers” akaweka wazi msimamo, Makonda chapa kazi.

Likaja suala la “uvamizi” wa Clouds Media. Hili sasavyombo karibu vyote vya habari vikaungana kumsulubu Makonda (actually Magufuli). Ni mara ya kwanza kushuhudia wapinzani na mahasimu wa kibiashara (Radio One/ITV, E-FM & Clouds) wameungana. Hii ni kwa vile maslahi yao yameguswa kwa njia moja au nyingine na Makonda au utawala wa Magufuli. Nape naye kwa vile Makonda alimtaja Wema kwenye sakata la mihadarati, ama kwa kujua au kuchotwa akili na “wajanja” wachache, akaunda Tume yake, (sijui kwa sheria ipi) kuchunguza tukio la “uvamizi”. Suala ambalo, kama lilikuwa kweli, lilipaswa kuwa suala la jinai Nape akalifanya lake. Wakati akijua msimamo wa Magufuli kuhusu Makonda, Tume ikafanya kazi chini ya saa 48 na kutoa taarifa Makonda akitiwa hatiani bila kusikilizwa. Sijui mpala leo kama Clouds waliwahi kusajili Polisi “uvamizi” huo kwa ajili ya upelelezi wa jinai.

Magufuli akafanya mabadiliko madogo ya baraza lake, ambapo Prof. Kabudi akawa Waziri wa Sheria na Dr. Mwakyembe akapelekwa Habari na hivyo kufanya Nape awe nje ya baraza. Nape huyu au vuvuzela kwa jina ambalo chadema waliompatia, akageuka shujaa na msema kweli na mwenye msimamo (rejea twits za Zitto Kabwe na wanachadema wengine). Nape aliyelalamikiwa kuzuia mBunge “live” (hata taarifa yke ipo) akaitwa mtetezi wa uhuru wa habari! Siku ya pili tangu mabadiliko madogo yafanyike akataka naye kufanya press conference kumjibu aliyefanya mabadailiko. Mkutano haukufanyika na tukio hilo likawa habari kubwa sana (kwa sababu za wazi). Tukaambiwa Kinana (Katibu Mkuu) wa CCM angeongea yake ya moyoni, CHADEMA na wapinzani wa Magufuli wakashangilia sana. Kinana hakuongena na mambo yakaishia hapo. Juzi tukamuona Mnyika akitoa tamko la kudai sababu za Magufuli kumuondoa Nape. Inashangaza sana, maana wakati anateuliwa hawakuomba sababu na zaidi walipinga uteuzi wake.

Limekuja suala la mchanga wa dhahabu. Kilio cha wapinzani na watanzania kwa jumla ni kuwa wachimbaji wa madini wanatupunja sana. Nakumbuka miaka ya 2008-9 Rais Kikwete aliunda Tume na Zitto akawa mmoja wa wajumbe. Tume hii lifanya kupitia mikataba ya uchimbaji madini ingawa matokeo yake hayakuwa ya kuridhisha sana. Ni Zitto huyu huyu, wakati huo akiwa CHADEMA alisema mchanga wa dhahbu unaosafirishwa unaipotezea nchi mapato makubwa na kwamba tunahitaji kinu cha kuchambulia mchanga huo hapa nchini. Magufuli ametoa zuio la usafirishaji wa mchanga na wapinzani wake sasa wanalalamika kwamba tujiandae dhidi ya kesi nzito nzito za kuvunja mikataba utadhani walishaiona hiyo mikataba. Kwenye mitandao sasa kumezuka “wachambuzi” wa suala la mchanga, ambao wengi ni wafuasi wa CHADEMA (upinzani) na kitu kimoja wanachokubaliana ni kwamba Rais Magufuli amekosea kuzuia usafirishaji wa mchanga, na kwamba nchi hii haina uwezo wa kuchenjua huo mchanga. Unabaki kujiuliza, wapinzani na watanzania wengine wanataka nini? Wanapinga nini na wanapenda nini?

Kwa sasa imebaki kuwa JK tutakukumbuka daima. Wanajisahulisha ni JK huyu huyu aliyeitwa dhaifu na John Mnyika. Wanadai rais Magufuli anaingilia mihimili na vyombo vingine. Juzi kijana Nay wa Mitego aliimba wimbo wa WOTE akielezea hisia zake kuhusu utawala. Alipokamatwa na Polisi malalamiko yakawa makubwa sana kwamba Magufuli anakandamiza uhuru wa kujieleza. Waziri Mwakyembe jana akatoa taarifa kuwa Rais Magufuli ameagiza kijana huyo aachiliwe huru na wimbo uendelee kupigwa na akimwomba aongeze mashairi kuhusu mambo kama mihadarati, rushwa, ukwepaji kodi, n.k. kibao kimegeuzwa sasa kwa nini Rais Magufuli anaingilia kazi za Polisi na BASATA!

Wakati ule Edward Lowassa amewajibishwa na Tume ya Richmond, mjadala ulikuwa mkali bungeni mpaka Philemon Ndesamburo akasema watu wa aina hiyo (mafisadi) wanapaswa kupigwa risasi hadharani au kunyongwa kama huko China. Malalamiko kipindi cha JK yalikuwa tume nyingi zinapoteza muda, sasa hatuna tume ila maamuzi bila tume wale wale wanalalamika.

Wapinzani wanataka nini? Je wana hoja zozote dhidi ya Magufuli na utawala wake?

Maswali ya kujiuliza:

Agenda kuu za sasa za wapinzani ni nini?

Je katiba mpya iliyopigiwa kelele wapinzani hawa wameridhika kwa yenyewe kuwekwa kapuni?

Kama wao wangeshika uongozi wa nchi hii, ni kipi ambacho wangefanya?

Mtazamo wako nini?
Agenda kuu ya chama cha upinzani ni kuongoza nchi, hata ccm ndio agenda yao ya kuendelea kabaki madarakani.
 
Kumtetea mhujumu wa elimu yetu na jambazi wa kutumia silaha bashite asichukuliwe hatua!

Hasa mwenyekiti mbowe huyo ndio hataki bashite aguswe
 
Back
Top Bottom