Clouds Wanadhalilisha Taasisi ya Urais

Clouds Wanadhalilisha Taasisi ya Urais

Kihistoria taasisi ya urais Tanzania inaheshimika sana. Ukiangalia utawala wa Nyerere, Mwinyi kidogo pamoja na kwamba aliichezea sana taasisi lakini Mkapa alirudisha heshima. Ukweli JK ameifanya taasisi ya urais imekuwa tu kama manager wa bendi fulani.

Nimesikitishwa na kitendo cha Clouds kumtumia JK kutangaza biashara yao. Wanaweka sauti ya JK ikiisifu Clouds kama sehemu ya tangazo la biashara kuitangaza Clouds na kiukweli kiitifika hawapaswi kufanya hivyo. Hivi itakuwaje leo Rais akitumika kutangaza Coca Cola au Azam Cola? Naiomba serikali ijue urais ni taasisi si mtu hivyo vitendo vya kudhalilisha taasisi yetu vikome mara moja. Kama JK anataka kutangaza biashara asubiri amalize kipindi chake cha urais.
Tatizo huyu raisi wetu ujana mwingi.
Utamsikia akisema katika hilo tangazo" clouds inasikilizwa na vijana wengi mpaka wakati mwingine na sisi unashawika kusikiliza".
 
jambo pekee ninalo mpendea raisi wangu wala hana makuu....nenda fb uone machekbob na wauza sura waliobahatika kupiga picha na raisi, walivyozitupia ktk wall zao.
Titizo anajisahau.
 
Kuna vitu ambavyo lazima tuyaangalie kwa undani. Walichokifanya Clouds ni kitu cha kuigwa kutumia Jingle ya sauti ya Rais wangu ni kuwaambia watanzania kuwa wanazo Baraka zote toka kwa Rais.
Mbona hakuna jipya pale ajili kwa vijana kitambo tulihaidiwa mpaka leo bado msoto.
Nafasi hiyo angeitumia waziri wa wizara husika.
 
Kinachofanywa na clouds ni swala ambalo pengine serikali kupitia wizara ya kazi na vijana ingeweza kuwa imefanya. Lakini kwa wao kama private sector wamefanya uzalendo. Ndo maana Rais amewaunga mkono na kuwapongeza. Ile inayorushwa ni clip ya sauti ya rais akiwapongeza wakati wa kuhitimisha fursa. Sioni kama kuna ubaya wowote kufanya hivyo.

iMind, naunga mkono maelezo yako.
 
Last edited by a moderator:
Japo sijasikia hilo Tangazo lakini Sidhani kama ni vizuri kutumia Taasisi hiyo kwa matangazo. Na mkuu mwenyewe sijui hilo halioni niliwahi kusikia sauti yake kwenye DUNIA YAKO CHAGUO LAKO. Hadi kwenye Fursa nadhani yupo heunda na hisa huko.
Tukimalizana na hao tunaenda kwa wale wanaotumia bendera ya taifa kutangaza bihashara zao.
 
JK ameufanya Uraisi ni Kuongoza sio Utawala,hataki aonekane kama dikteta au Mfalme,JK mtu wa watu.hana majigambo wala kusujudiwa,wala Ikulu hataki ionekane kama peponi ni nyumba yetu na kila Mtu alieiletea Taifa heshma anawezakwenda,zamani hata Waandishi wa habari walikuwa Ikulu wanaiona kama Peponi.Jamaa akiondoka tutamkumbuka.

kwa matatizo haya na hali ya uchumi ilivyo lazima tutamkumbuka
 
Kwani TISS hawasikilizi Redio? Kama wamesikia wametulia then Rais kakubali. Kwanza Rais mwenyewe anafurahia Promo
Kihistoria taasisi ya urais Tanzania inaheshimika sana. Ukiangalia utawala wa Nyerere, Mwinyi kidogo pamoja na kwamba aliichezea sana taasisi lakini Mkapa alirudisha heshima. Ukweli JK ameifanya taasisi ya urais imekuwa tu kama manager wa bendi fulani.

Nimesikitishwa na kitendo cha Clouds kumtumia JK kutangaza biashara yao. Wanaweka sauti ya JK ikiisifu Clouds kama sehemu ya tangazo la biashara kuitangaza Clouds na kiukweli kiitifika hawapaswi kufanya hivyo. Hivi itakuwaje leo Rais akitumika kutangaza Coca Cola au Azam Cola? Naiomba serikali ijue urais ni taasisi si mtu hivyo vitendo vya kudhalilisha taasisi yetu vikome mara moja. Kama JK anataka kutangaza biashara asubiri amalize kipindi chake cha urais.
 
KOVA nae katumika kwnye tangazo la M-PESA...

TANZANIA BHANA...
 
Rais kuongea Clouds sio tatizo. Tatizo ni Rais kutumia fursa aliyopata kuisifia Clouds kama the best media na kimsingi maneno ya Rais yanaonesha kana kwamba hakuna media nyingine kama Clouds which is wrong! Kibaya zaidi, ni Clouds kutumia maneno ya Rais kujitangaza which is absolutely wrong!

Rais ni Rais wa wote na sio wa Clouds peke yao au taasisi nyingine binafsi. Main theme ya speech ya Rais ilikuwa ni issue ya "fursa" kwa watanzania ambayo media nyingine yoyote ina haki ya kuitangaza lakini speech yenyewe inapohusisha promo kwa media mojawapo nadhani itakuwa vigumu kwa media zingine kutangaza speech ya aina hiyo. Unless tuambiwe kwa wakati ule Rais hakuwa anaongea kama Rais bali kama mtu binafsi. Tupende tusipende, ile speech ina kasoro na kasoro hizo zinatumika vibaya.
 
Kinachofanywa na clouds ni swala ambalo pengine serikali kupitia wizara ya kazi na vijana ingeweza kuwa imefanya. Lakini kwa wao kama private sector wamefanya uzalendo. Ndo maana Rais amewaunga mkono na kuwapongeza. Ile inayorushwa ni clip ya sauti ya rais akiwapongeza wakati wa kuhitimisha fursa. Sioni kama kuna ubaya wowote kufanya hivyo.

Jamaa anatumika hapo kama dalali kama ilivyo kwa viongozi wenu wa TZ
 
Acha jazba mkuu........hadi maneno yako unayachanganya? UKULU...........Na hata hivyo, unatuambia tulichagua wahuni na machekibobu kwenda Ikulu? Kweli?

Soma na kuelewa kabla ya kumwaga licomment lako linalodhihirisha kujua wewe ni mkurupukaji
 
Si Mlitaka Raisi handsome, na Mkapata?

Haya Sasa tuvumiliane tu.
 
Raisi wenu ni mvivu wa kufikiri na hata kuwatumia washauri wake ni mvivu
 
Jamani naomba mniunge mkono msimu huu wa uchaguzi mimi nimeona nigombee Urais wazee,
Niliwahi kuwaza muda mreefu kwelikweli ila nilikuwa sijiamimi, lakini baada ya kumuona huyu jamaa anavyoongoza, sasa nimejikubali kuwa hata mimi naweza nikaachana na haya Mambo ya kuvuta waya na kushika tester nikaingia kwenye kazi ya Urais!!
Naombeni sapoti yenu wanajamvi!!
Mimi sitachekacheka kinafki kama huyu pres wetu wa sasa, sitakubali kutumika kibiashara na mtu yeyote, nisingetumika hata kumdhulumu Sugu ile project yake ya Malaria no more, nitajiheshimu jamani, naombeni kuungwa mkono maana umebaki mwaka toka sasa wazee!!
 
Kinachofanywa na clouds ni swala ambalo pengine serikali kupitia wizara ya kazi na vijana ingeweza kuwa imefanya. Lakini kwa wao kama private sector wamefanya uzalendo. Ndo maana Rais amewaunga mkono na kuwapongeza. Ile inayorushwa ni clip ya sauti ya rais akiwapongeza wakati wa kuhitimisha fursa. Sioni kama kuna ubaya wowote kufanya hivyo.

clouds imewashika pabaya....kila siku clouds hiki clouds kile.....FURSA hizo sio clouds kila anayetaka,na leo 02/12/2013 wametimiza MIAKA 14 HONGERA CLOUDS FM MFIKE MIAKA 100
 
dezko mbaya. kitafanywa kisichositahili utaona sawa tu
 
Back
Top Bottom