Clouds Wanadhalilisha Taasisi ya Urais

Clouds Wanadhalilisha Taasisi ya Urais

Kinachofanywa na clouds ni swala ambalo pengine serikali kupitia wizara ya kazi na vijana ingeweza kuwa imefanya. Lakini kwa wao kama private sector wamefanya uzalendo. Ndo maana Rais amewaunga mkono na kuwapongeza. Ile inayorushwa ni clip ya sauti ya rais akiwapongeza wakati wa kuhitimisha fursa. Sioni kama kuna ubaya wowote kufanya hivyo.

Uko sawa kabisa me naona ilikuwa ni vizuri kwa rais kuwaunga mkono kwani walichokifanya ni kizuri sana wameamsha hari kwa vijana sema kuna watu wamezaliwa kupinga kila kitu hata kama ni kizuri
 
Kuna vitu ambavyo lazima tuyaangalie kwa undani. Walichokifanya Clouds ni kitu cha kuigwa kutumia Jingle ya sauti ya Rais wangu ni kuwaambia watanzania kuwa wanazo Baraka zote toka kwa Rais.

Rais anatoa shukurani zake na kutuaminisha watanzania Fursa ilikuwa ya kuigwa.

Tuache kuwa biased. Tanzania ni yetu wew ukiona Negative sisi Tunaona Positive things.
 
hata mie nimeliskia. ni aibu sana kwa taasisi ya urais. ila serikali inachekacheka tu
 
Hata mm linanikwaza kwakwel..
Hua cluds hawatumiagi akili kbs cjui wanadhan tangazo likitangazwa na raisi ndo kweli watakua ivo.
So so boring....
 
Skuizi ndo mana kila brazamen na wapiga debe vituoni ndo mana wanautaka urais hyu mkuu wetu kauvunjia heshima sana
kamata fursa twenzetu...iko powa fursa ndio jambo la msingi kwa sasa
 
labda kwanza nijue,,
lile tangazo kalitoa yeye kweli ama ni wale wataalam wa kuigiz sauti,,,
na je alitoa authority kuigizwa???
 
Inawezekana kawekeza pale so ni moja ya wajibu wake ktk suala la promo.
 
Clouds inaweza kuwa biashara yake utajuaje huenda ni mkakati wa biashara ukiwa ikulu
 
Mi binafsi nimelizikia hilo tangazo. Actually ni part ya speech kuhusu fursa ambayo Jk aliitoa pale Diamond Jubilee. Jamaa wa clouds wanaitumia sana ku capitalize their media.
 
Mwl Nyerere aliwaambia ukulu si mahala pa wahuni na machekibob nyie mkamuona anawivu na chuki kwa kaka mkuu.. Haya sasa na mtashuhudia mengi

Hahaha...pale mpaka mdumange utachezwa.
 
JK ameufanya Uraisi ni Kuongoza sio Utawala,hataki aonekane kama dikteta au Mfalme,JK mtu wa watu.hana majigambo wala kusujudiwa,wala Ikulu hataki ionekane kama peponi ni nyumba yetu na kila Mtu alieiletea Taifa heshma anawezakwenda,zamani hata Waandishi wa habari walikuwa Ikulu wanaiona kama Peponi.Jamaa akiondoka tutamkumbuka.

Utamkumbuka wewe,mkeo,familia yako na watu kama wewe. Sijawahi wala sintakuja kumuelewa huyu rais wako,anafanya mambo ya ajabu ajabu tu,bora akaongoze Tz mtoto aliyemaliza 4m 4 shule ya kata kuliko huyo check ndugu yenu.f.kabisa.
 
jambo pekee ninalo mpendea raisi wangu wala hana makuu....nenda fb uone machekbob na wauza sura waliobahatika kupiga picha na raisi, walivyozitupia ktk wall zao.kwa rais dikteta kama paul kagame au mzee m7 cjui kama hili linawezekana kwa raia wake.
 
Kihistoria taasisi ya urais Tanzania inaheshimika sana. Ukiangalia utawala wa Nyerere, Mwinyi kidogo pamoja na kwamba aliichezea sana taasisi lakini Mkapa alirudisha heshima. Ukweli JK ameifanya taasisi ya urais imekuwa tu kama manager wa bendi fulani.

Nimesikitishwa na kitendo cha Clouds kumtumia JK kutangaza biashara yao. Wanaweka sauti ya JK ikiisifu Clouds kama sehemu ya tangazo la biashara kuitangaza Clouds na kiukweli kiitifika hawapaswi kufanya hivyo. Hivi itakuwaje leo Rais akitumika kutangaza Coca Cola au Azam Cola? Naiomba serikali ijue urais ni taasisi si mtu hivyo vitendo vya kudhalilisha taasisi yetu vikome mara moja. Kama JK anataka kutangaza biashara asubiri amalize kipindi chake cha urais.

Tatizo ni kwamba kile kiredio huwa sikisikilizi, hivi huwa sauti ya Kikwete inasikika sana saa ngapi ili ni-tune nisikie huo utumbo?
 
Tatizo Rais hasikilizi hiyo redio. Sasa atajuaje kama amewekwa kwenye tangazo? Na je alitengeneza tangazo au speech yake ndio imefanywa tangazo?. Kama alitoa speech ndio watu waka edit nakufanya tangazo mbona kawaida tu.. Na sio Jk tu Marais wengi speech zao zinawekwa kama tangazo,!!
 
Wapika majungu.. mmetoka redio iman, sasa mpo clauds. Majungu ndani ya chama nayo yameiva.... mnayapaku sasa!!!!!
 
Kinachofanywa na clouds ni swala ambalo pengine serikali kupitia wizara ya kazi na vijana ingeweza kuwa imefanya. Lakini kwa wao kama private sector wamefanya uzalendo. Ndo maana Rais amewaunga mkono na kuwapongeza. Ile inayorushwa ni clip ya sauti ya rais akiwapongeza wakati wa kuhitimisha fursa. Sioni kama kuna ubaya wowote kufanya hivyo.
Si kuna waziri wa wizara husika kwanini mpaka atumike Jk, au anatengeneza mazingira?
 
Back
Top Bottom