Watu kama wewe mtasababisha JF ionekane haina tofauti na genge la wahuni siku si nyingi. Watu mnachangia kipuuzi kitu ambacho hamjakisikia. Hivi Clouds walichofanya ni kuchukua sauti iliyotokana na speech yake alipoalikwa kuwa mgeni rasmi kwenye semina ya Fursa. Nashangaa wenyewe mawazo na mtazamo hasi dhidi ya JK na Clouds mnasema amefanya tangazo. Kwanini msijadili yanayojiri kwenye saccos yenu ya Kaskazini.
hapo kwenye red tatizo ni wanyonyaji na hawataki kukubali hili, pili ina watangazaji wa radio haina waandishi wa habari.Ni kweli kabisa, lakini kwa nini kila wanachofanya clouds fm kionekane kibaya?!!
Kihistoria taasisi ya urais Tanzania inaheshimika sana. Ukiangalia utawala wa Nyerere, Mwinyi kidogo pamoja na kwamba aliichezea sana taasisi lakini Mkapa alirudisha heshima. Ukweli JK ameifanya taasisi ya urais imekuwa tu kama manager wa bendi fulani.
Nimesikitishwa na kitendo cha Clouds kumtumia JK kutangaza biashara yao. Wanaweka sauti ya JK ikiisifu Clouds kama sehemu ya tangazo la biashara kuitangaza Clouds na kiukweli kiitifika hawapaswi kufanya hivyo. Hivi itakuwaje leo Rais akitumika kutangaza Coca Cola au Azam Cola? Naiomba serikali ijue urais ni taasisi si mtu hivyo vitendo vya kudhalilisha taasisi yetu vikome mara moja. Kama JK anataka kutangaza biashara asubiri amalize kipindi chake cha urais.
Mijitu mingine bana sijui ilikuja duniani kufanya nn maana hayajui chochote kazi kufuata mkumbo tu!
Sikia wewe kaole tukufundishe ethics-Haitakiwi kutumia kitu chochote toka kwenye taasisi ya Ikulu kwa faida ya watu wachache!Hiyo ni sawa na JK kuwasadia Clouds kwenye biashara zake!Kuna watu kama ww wanapenda sauti ya JK kwenye hilo tangazo la Clouds so watafungua radio na TV zao na kufanya views waongezeke na wao kuongeza bei ya matangazo yao!Lkn ww huyajui haya nakuonea tu bure kukueleza!
Sijapata kuona hapa Obama eti anachukuliwa sauti yake na MSNBC waweke tangazo labda awe amenunua mwenyewe hasa kipindi cha uchaguzi!
Ikulu yetu imevamiwa!
Soma na kuelewa kabla ya kumwaga licomment lako linalodhihirisha kujua wewe ni mkurupukaji
Aisee nilikuwa nasoma hizi posts huku nacheka. Wengine wanaomponda humu ndio wamekuwa vinara kumsifia sasa hivi.Naomba Mwenyezi Mungu aniweke hadi 2016 ili niwaone Wa TZ watakavyokuwa wanamkumbuka JK.
cc. Ritz naomba uje unikumbushe, muda ukifika inshallah!!