Clouds TV na propaganda ya vita kisiasa

Clouds TV na propaganda ya vita kisiasa

Hivi kuna watu wanaangalia hii clouds tv nakusikiliza hiyo radio, he he he, mimi niliachaga siku nyingi mpaka nimeisahau kila kitu chao wanajipendekeza kwa serikali, yaani ukisikia unafiki uliotukuka wa kiwango cha juu ndio Clouds FM.
 
Duh umeiandika kwa jaziba kweli kweli. Lakini inategemea pia mtazamo wako na tafasiri unayotaka nayo. Hata hivyo unaweza kulalamikia tangazo hilo TCRA ambako Kamati ya maudhui italiangalia na kulitolea maamuzi.

Kwa nini utengeneze kitu cha hovyo ukisubiri mtu aende TCRA. Hawa jamaa siyo watu wa kuangalia tu. Nilisikia wakihusishwa na wauza madawa ya kulevya na kufanya ushirika nao. Wakati wa kifo cha mangwea mwingine alibanwa makofi hadhalani.

Kinachofanyika ni ule ushabiki wa kumusifia rais kila wakati wakajifanaya ni swahiba wao na sasa wanajaribu kurudi huko huko. Ni ukosefu wa seriusness ambao kwa ujumla pia ni madahala ya elimu ndogo ya wahusika. Huwezi kutoka kwenye uDJ ukawa mawanahabari wa maana, bila elimu.
 
Kituo hiki binafsi cha TV kinahatarisha upendo baina ya wanajamii katika Taifa hili na kuchochea chuki na uhasama kwa kutumika kufanya propaganda za wazi wazi dhidi ya chama pinzani-CHADEMA kwa makusudi kwa kushirikiana na CCM kwa indirect way kwa kichaka cha kutangaza uzalendo!! Tabia hii umekubuhu clouds radio na sasa inaanza kumea kwenye TV!

Kwa watazamaji wa kituo hiki,wataona kuna Tangazo ambalo linaonyeshwa siku hizi linaloanza na wimbo wa Taifa na hatimae mshereheshaji kuanza kuongea na kutaka taifa liombewe huku picha za mnato zikipita!!
Propaganda hii chafu imejaa kwenye picha hizi za mnato ambapo 70% zinaonyesha wabunge wa CHADEMA wakiwa bungeni na kwa kuhusisha pia maneno ya vita na kutolea mifano ya Nigeria,Somalia,Syria,Ukraine etc huku pia yakionyeshwa mafuvu ya watu!!!

Tatzo lipo kwa nini wamebezi tu kuwaonyesha; Tundu Lissu kwa kurudia rudia akiongea na sio Mwanasheria Mkuu aliyejaribu kumpiga Kafulila ndani ya Bunge na hata kumkata kichwa??!!

Anaonyweshwa Ezekiel Wenje mara kadhaa huku akipunga vidole viwili juu na sio Serukamba aliyesema Fuc.k you ndani ya bunge???!!

Anaonyeswha Joseph Mbilinyi akivutwa na walinzi wa bunge na kwa nini sio Juma Nkamia aliyesema haongei na mbwa bali mwenye mbwa ndani ya bunge huku akimjibu binadamu mwenzie??!!

Kwa wafuatiliaji inafahamika wazi kuwa wamiliki wa kituo hiki wapo karibu na watawala na imefikia pahali sasa wakiandaa na kuhodhi dhifa za kitaifa kama tukio la uzinduzi wa video ya uzalendo ya wasanii pale Dodoma,birthday ya Kikwete na keki juu,uzinduzi wa mradi wa Malaria miaka kadhaa iliyopita utafikiri hakuna vyombo cha serikali-TBC TVS na Radio!!

Imefikia pahali hadi Raisi na mawaziri wanatumika na kituo hiki binafsi kuandaa jingles za radio huku wakikiacha solemba kituo cha Umma!!!

Hata propaganda za raisi kijana zilianzia clouds Fm 2012 kwa kuwahusisha January Makamba na Zitto kwenye segment ya kitaa kinasema katika kipindi cha XXL na vinginevyo!!

Mauaji ya Rwanda hata na kule Kenya wakati wa uchaguzi yalichochewa na vituo binafsi vya radio kwa kuchochea chuki dhidi ya upande mwingine/kabila lingine na ndio maana kuna wakurugenzi kadhaa wameshitakiwa kimataifa,clouds nao naona hawaridhiki na faida wanazopata na sasa wanajiingiza kwenye chuki za siasa kwa hadaa za uzalendo!!!
Ni kweli kabisa cloud TV wanaboa sana,wtangazaji wake hawana umahili wowote,mimi naipata kupitia AZAM TV na uwa nikimaliza kuangalia headline za magazeti ITV uwa nashift to clouds na hasahas during world cup.kuna watangazaji wanaboa sana,upeo mdogo wa kuchambua mambo na wanatumia muda mwingi kutaniana wao kwa wao,na mambo mengi ya kipuuzipuuzi,nafikiri its the worst TV station in TZ
 
Hii radio clouds na TV yake mwisho wake ni 2015 wala msipoteze muda wenu kuhangaika na waganga njaa hawa wa clouds
 
Kwa nini utengeneze kitu cha hovyo ukisubiri mtu aende TCRA. Hawa jamaa siyo watu wa kuangalia tu. Nilisikia wakihusishwa na wauza madawa ya kulevya na kufanya ushirika nao. Wakati wa kifo cha mangwea mwingine alibanwa makofi hadhalani.

Kinachofanyika ni ule ushabiki wa kumusifia rais kila wakati wakajifanaya ni swahiba wao na sasa wanajaribu kurudi huko huko. Ni ukosefu wa seriusness ambao kwa ujumla pia ni madahala ya elimu ndogo ya wahusika. Huwezi kutoka kwenye uDJ ukawa mawanahabari wa maana, bila elimu.

Halafu wakina Pasco wanasema tuna mitazamo yetu binafsi hasi dhidi ya clouds,yaani mtu unaona mavi mezani halafu mtu anatetea kwa nini umeangalia??!!
 
Last edited by a moderator:
Mliojitoa mhanga kutazama kituo hicho mjiandae pia kisaikolojia kushuhudia watangazaji wakipigana mande. Kule kwenye redio yao walithubutu wakaweza na wakasonga mbele. Hivi kabisa mtu una tune clouds tv halafu unatulia kutazama, are you serious?
 
Halafu wakina Pasco wanasema tuna mitazamo yetu binafsi hasi dhidi ya clouds,yaani mtu unaona mavi mezani halafu mtu anatetea kwa nini umeangalia??!!
Mkuu MudiBoka, kitendo kuthibitisha una chuki binafsi dhidi ya Clouds, ni hiki sasa cha kuifananisha na ma.i mezani!.
Ndugu, wandugu na bandugu, tupunguze chuki binafsi!.
Chuki ikizidi hugeuka ni ugonjwa!.
Pasco
 
Ni kweli kabisa cloud TV wanaboa sana,wtangazaji wake hawana umahili wowote, na hasahas during world cup.kuna watangazaji wanaboa sana,upeo mdogo wa kuchambua mambo na wanatumia muda mwingi kutaniana wao kwa wao,na mambo mengi ya kipuuzipuuzi,nafikiri its the worst TV station in TZ
Mkuu Ngonani, tujitahidi tuwe na shukrani katika madogo ili tuweze kushukuru kwa makubwa!, Tangu kombe la dunia limeanza, kuna kituo chochote kimewahi kupeleka crew huko kombe linakochezewa?!. Badala ya kuilaumu Clouds, ulipaswa kuipongeza kwa hatua hiyo tuu ya kupeleka team Brazil! kutupatia hicho kidogo walichoweza!. Tuwe na appreciation japo kidogo!, ila pia sishangai, Watanzania wengi ni watu wa kulalamika na kulaumu tuu kutwa kucha!. Think positive, be positive!.
Pasco
 
Ni ukosefu wa seriusness ambao kwa ujumla pia ni madahala ya elimu ndogo ya wahusika. Huwezi kutoka kwenye uDJ ukawa mawanahabari wa maana, bila elimu.
Hapa unachanganya umiliki na uana habari, huyo DJ ni mmiliki na sio mwanahabari, na lengo la msingi la Clouds Radio ilikuwa ni kutoa burudani, habari zilikuja baadae sana!. Mmiliki wa Media kubwa kabisa nchini, IPP Media, ni Mzee Mengi na sio mwana habari!. Mmmiliki wa Media ya pili kwa ukubwa Tanzania, Sahara Media, ni Antony Diallo, sio mwanahabari!, Mmmilikiwa media ya tatu kwa ukubwa nchini, AMG, ni Shabir Abji, sio mwanahabari!. Wamiliki wengine karibu wote wa vituo vyaredio na TV sio wanahabari!. Wanahabari wenye redio zao ni Abdalah Majura na Ahmed Kipozi, hizo redio zao wewe unazikia?.

Pasco
 
Hata jana walijaribu kuwaaminisha watu kuwa milipuko ya arusha inasababishwa na chadema
 
Mkuu MudiBoka, kitendo kuthibitisha una chuki binafsi dhidi ya Clouds, ni hiki sasa cha kuifananisha na ma.i mezani!.
Ndugu, wandugu na bandugu, tupunguze chuki binafsi!.
Chuki ikizidi hugeuka ni ugonjwa!.
Pasco

Mkuu Pasco usitake kupotosha,siamini kama hufahamu matumizi ya lugha ya picha,Nakumbuka kuna wakenya walisema waandishi wa Tanzania huramba viatu!!!
 
Last edited by a moderator:
Kituo hiki binafsi cha TV kinahatarisha upendo baina ya wanajamii katika Taifa hili na kuchochea chuki na uhasama kwa kutumika kufanya propaganda za wazi wazi dhidi ya chama pinzani-CHADEMA kwa makusudi kwa kushirikiana na CCM kwa indirect way kwa kichaka cha kutangaza uzalendo!! Tabia hii umekubuhu clouds radio na sasa inaanza kumea kwenye TV!

Kwa watazamaji wa kituo hiki,wataona kuna Tangazo ambalo linaonyeshwa siku hizi linaloanza na wimbo wa Taifa na hatimae mshereheshaji kuanza kuongea na kutaka taifa liombewe huku picha za mnato zikipita!!

Propaganda hii chafu imejaa kwenye picha hizi za mnato ambapo 70% zinaonyesha wabunge wa CHADEMA wakiwa bungeni na kwa kuhusisha pia maneno ya vita na kutolea mifano ya Nigeria,Somalia,Syria,Ukraine etc huku pia yakionyeshwa mafuvu ya watu!!!

Tatzo lipo kwa nini wamebezi tu kuwaonyesha; Tundu Lissu kwa kurudia rudia akiongea na sio Mwanasheria Mkuu aliyejaribu kumpiga Kafulila ndani ya Bunge na hata kumkata kichwa??!!

Anaonyweshwa Ezekiel Wenje mara kadhaa huku akipunga vidole viwili juu na sio Serukamba aliyesema Fuc.k you ndani ya bunge???!!

Anaonyeswha Joseph Mbilinyi akivutwa na walinzi wa bunge na kwa nini sio Juma Nkamia aliyesema haongei na mbwa bali mwenye mbwa ndani ya bunge huku akimjibu binadamu mwenzie??!!

Kwa wafuatiliaji inafahamika wazi kuwa wamiliki wa kituo hiki wapo karibu na watawala na imefikia pahali sasa wakiandaa na kuhodhi dhifa za kitaifa kama tukio la uzinduzi wa video ya uzalendo ya wasanii pale Dodoma,birthday ya Kikwete na keki juu,uzinduzi wa mradi wa Malaria miaka kadhaa iliyopita utafikiri hakuna vyombo cha serikali-TBC TVS na Radio!!

Imefikia pahali hadi Raisi na mawaziri wanatumika na kituo hiki binafsi kuandaa jingles za radio huku wakikiacha solemba kituo cha Umma!!!

Hata propaganda za raisi kijana zilianzia clouds Fm 2012 kwa kuwahusisha January Makamba na Zitto kwenye segment ya kitaa kinasema katika kipindi cha XXL na vinginevyo!!

Mauaji ya Rwanda hata na kule Kenya wakati wa uchaguzi yalichochewa na vituo binafsi vya radio kwa kuchochea chuki dhidi ya upande mwingine/kabila lingine na ndio maana kuna wakurugenzi kadhaa wameshitakiwa kimataifa,clouds nao naona hawaridhiki na faida wanazopata na sasa wanajiingiza kwenye chuki za siasa kwa hadaa za uzalendo!!!
Nchi inameguka vipande vipande sasa.Angalia mifano hii,
  1. Katika mikutano ya hadhara hasa vijijini salamu tatu hutolewa,Asalaam aleykum,Bwana Yesu asifiwe na Tumsifu Yesu Kristo.
  2. Panda mabus ya mikoani kuna wauza dawa za kichina,salamu ni hivyo hivyo.
  3. Ingia kwenye mitandao ya kijamii angalia kwa mfano thead inayohusu Gaza na Israel shuhudia mpasuko uliopo.
Kuna hitilafu kubwa tayari lakini kwa kuwa wakubwa wanataka ushindi wa kishindo hakuna wa kukemea.
 
Mkuu Ngonani, tujitahidi tuwe na shukrani katika madogo ili tuweze kushukuru kwa makubwa!, Tangu kombe la dunia limeanza, kuna kituo chochote kimewahi kupeleka crew huko kombe linakochezewa?!. Badala ya kuilaumu Clouds, ulipaswa kuipongeza kwa hatua hiyo tuu ya kupeleka team Brazil! kutupatia hicho kidogo walichoweza!. Tuwe na appreciation japo kidogo!, ila pia sishangai, Watanzania wengi ni watu wa kulalamika na kulaumu tuu kutwa kucha!. Think positive, be positive!.
Pasco

Kwa ilo la world cup ni kweli walichangamsha lakini the rest ni pumba,ukisema watanzania tuna tabia ya kulalamika that includes you,hata hivyo sikujua kuwa una ubia na hiyo TV,receive my appology mkuu.
 
Mkuu Ngonani, sina ubia wowote na Clouds Media ila nina little appreciation for the little they did!. Mmiliki Joe ni form four leaver nadhani with bad pass akawa DJ, sasa anamiliki the No. 1 Radio Station in Tanzania, the man is humble and down to earth!. Alipoanza mimi tayari nilikuwa mtangazaji tena niliienda shule!, hakuweza kuajiri watangazaji wasomi kwa sababu hakuwa na uwezo huo, hivyo alichukua vijana wa mtaani tuu ila wenye vipaji na ndio wameifikisha Clouds hapo ilipo sasa!. Its a big step ya kustahili pongezi sio shutuma!.

Kwa hiyo Mkuu sie tukikosoa basi hatufai na hatutakiwi kukosoa kisa wametoka mbali na founder hakwenda shule???!! Kwa ukubwa wao ndio wasikosolewe??!!

Ulishakili tangazo hilo hujaliona na unfortunately huangaliagi clouds tv,hiyo moral authority ya kutetea clouds na kushutumu wakosoaji unaipata wapi na kwa maslahi yapi??!!

Kama hutojali,ulikili kuwa hutazamagi clouds,unaweza kutudokeza kwa nini Mkuu??!!
 
Nobody is perfect, kuna ukosoaji wa manufaa unaitwa "constructive criticism" huu unafanywa kwa upendo na lengo sio kukandia, bali kuonyesha mapungufu ili wahusika wajirekebishe, na ukosoaji wa kukandia au kubondea!. Wako wewe ni wa kukandia na kubondea, huu unaonaga madhaifu tuu, yale mazuri hauyaoni yaani mabaya tuu mwanzo mwisho.

Siangalii Clouds TV kwa sababu natumia kingamuzi cha Explora hakina Clouds TV.

Pasco
 
Hapa unachanganya umiliki na uana habari, huyo DJ ni mmiliki na sio mwanahabari, na lengo la msingi la Clouds Radio ilikuwa ni kutoa burudani, habari zilikuja baadae sana!. Mmiliki wa Media kubwa kabisa nchini, IPP Media, ni Mzee Mengi na sio mwana habari!. Mmmiliki wa Media ya pili kwa ukubwa Tanzania, Sahara Media, ni Antony Diallo, sio mwanahabari!, Mmmilikiwa media ya tatu kwa ukubwa nchini, AMG, ni Shabir Abji, sio mwanahabari!. Wamiliki wengine karibu wote wa vituo vyaredio na TV sio wanahabari!. Wanahabari wenye redio zao ni Abdalah Majura na Ahmed Kipozi, hizo redio zao wewe unazikia?.

Pasco

Hebu nisaidie ni kwa nini Clouds wameshindwa kuwa ni chombo cha habari!
Naomba ufahamu kwamba taaluma yako inakujenga ktk mtindo ambao unaweza kukufanya uweze mambo mengine nje ya taaluma. Mwalimu anajijenga kiakili kiasi kwamba anaweza kujenga hoja na kuwa mwanasiasa. Ni vigumu DJ au baharia kuwa reasonable kiasi cha kuwa mtu wa kujenga hoja.

Clouds wanatimiza matakwa ya mwajili na ndo maana mbali na taaluma, huwezi kuwasikia wakisema baya juu ya rafiki wa mwajili wao. ktk ITV hutasikia hata siku moja wakisema kinyume na Mengi. that is natural hata US ni hivyo. Sijui kama ulisikia mtangazaji aliyeachishwa kazi NBC wakati wa vita ya Iraq?
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom