Clouds TV na propaganda ya vita kisiasa

Clouds TV na propaganda ya vita kisiasa

Boka,
  1. Sijawahi kuparamia miti popote!
  2. Sijawahi kuparamia miti makaburi ya Kinondoni!
  3. Sikumbuki kuhudhuria mazishi ya jaji yoyote Kinondoni!
  4. Sijawahi kuhitaji kumpiga picha EL popote!
  5. Sijawahi muleta update coyote humu jf kumhusu EL!.
Na mwisho, its very unfortunately hula siangalii Clouds TV, hivyo tangazo sijaliona ila nimejibu very generally kuwa Clouds Radio wanafanya kazi nzuri ya kupigiwa mfano, uzuri au ubaya wa tangazo fulani ni perception, ukiisha kuwa na negative atitude kuhusu kitu fulani, unakosa clear vision ba badala yake unakuwa na blurred vision. Nikiliona kama ni kweli linasifa negative hizo ulizozitaja, nitarudi humu na kuomba sorry.

NB. Mimi ni miongoni wa wana jf tuliojitanabaisha wazi kumkubali EL!, kumkubali hakuna maana ni mfuasi!, kuwa mfuasi ni wa kuwa follower!, kumkubali ni accepting!, ukiwa ni follower unakuwa ni follower wa huyo huyo mmoja, lakini kumkubali ni zaidi ya mmoja, yaani namkubali EL ndani ya CCM, nankubali ZZK ndani ya Chadema, namkubali Jussa ndani ya CUF, namkubali Kafulila ndani ya NCCR Mageuzi etc!.

Pia nillisha wahi kuhudhuria mazishi fulani, nikatafuta picha fulani!, nikaparamia kitu fulani, sio makaburi ya Kinondoni, Sio picha ya EL na sio kuparamia mti!.

Pasco

Shukrani Pasco kwa mchango wako na haswa paragraph 2 za mwisho japo hukutaka kueleza bayana lakini ni wazi inatosha kuonyesha unajulikana!!

Umekili hujawahi kuliona tangazo na kuwa umejibu kijumla jumla tu,Naamini unafahamu huu msemo "no research,no right to speak",generalization yako ya kunihukumu kuwa nina mtizamo wangu hasi on the making unaitoa wapi??!!

Pasco conclusion kwa kitu usichokiona utazani umekiona sio dalili au element ya ukanjanja??!! Au ndio weledi wenyewe for the love????!!!
 
lengo na fitina za ruge ni sugu asirudi bungeni 2015.ni mpinzani wake wa jadi.uwepo wa sugu ktk chombo nyeti cha bunge ni pigo kwa mafia wa tasnia nzima ya sanaa nchini.

Mkuuuu....mbowe yuko kimya juu ya hiiii kitu yuko radhi sugu apoteze ubunge na syo Pesa...mynd u ruge ndo alomtumia mbowe kumshinikiza sugu aache bifu nae fuatilia tena show zinazoandaliwa na clouds pale bilcanaz ...yaaan mbowe na ruge ni biznec Patna ...wanamaslahi mapana kuna mchezo mchafu mbowe na ruge wanacheza juu ya sugu...Kweli inapendwa pesa
 
clouds ni agenda ya wachache.... Itaisha tu, hilontangazo likidharauliwa litaonekana halina mantiki yoyote.... Ila chadema wakiliongelea, then litakua na mantiki

clouds ni sawa na glass y bar, utaitumia kubutudika lakini kamwe hutaikumbuka

Mnanivuruga!
 
kaka, ni kwamba mtu makini hawezi kusikiliza clouds radio wala kuangalia TV yao, kwanza hakika huwezi kujifunza chochote kile, hata uangalie toka asubuhi mpaka jioni zaidi utaonyeshwa utupu wa wanawake na lugha za kichochezi kama hizo, pili ndio maana waandishi makini kama akina kayanda ambao wanataruma ya uandishi wameikimbia ile radio, tatu ile radio umeendekeza ukabila kuanzia kwenye kuwatangaza wasanii, mfano sikiliza XXXL, tatu hii radio na TV inatumika kama danguro la kuharibu mabinti na madada zetu angalia BOSS WAO anatumia radio na tv kuwarubuni madada hasa wanao jifanya wako THT rejea ugomvi wa YAHYA NA JIDE, radio clouds na tv nashauri TCRA IWAFUNGIE

Kituo hiki binafsi cha TV kinahatarisha upendo baina ya wanajamii katika Taifa hili na kuchochea chuki na uhasama kwa kutumika kufanya propaganda za wazi wazi dhidi ya chama pinzani-CHADEMA kwa makusudi kwa kushirikiana na CCM kwa indirect way kwa kichaka cha kutangaza uzalendo!! Tabia hii umekubuhu clouds radio na sasa inaanza kumea kwenye TV!

Kwa watazamaji wa kituo hiki,wataona kuna Tangazo ambalo linaonyeshwa siku hizi linaloanza na wimbo wa Taifa na hatimae mshereheshaji kuanza kuongea na kutaka taifa liombewe huku picha za mnato zikipita!!

Propaganda hii chafu imejaa kwenye picha hizi za mnato ambapo 70% zinaonyesha wabunge wa CHADEMA wakiwa bungeni na kwa kuhusisha pia maneno ya vita na kutolea mifano ya Nigeria,Somalia,Syria,Ukraine etc huku pia yakionyeshwa mafuvu ya watu!!!

Tatzo lipo kwa nini wamebezi tu kuwaonyesha; Tundu Lissu kwa kurudia rudia akiongea na sio Mwanasheria Mkuu aliyejaribu kumpiga Kafulila ndani ya Bunge na hata kumkata kichwa??!!

Anaonyweshwa Ezekiel Wenje mara kadhaa huku akipunga vidole viwili juu na sio Serukamba aliyesema Fuc.k you ndani ya bunge???!!

Anaonyeswha Joseph Mbilinyi akivutwa na walinzi wa bunge na kwa nini sio Juma Nkamia aliyesema haongei na mbwa bali mwenye mbwa ndani ya bunge huku akimjibu binadamu mwenzie??!!

Kwa wafuatiliaji inafahamika wazi kuwa wamiliki wa kituo hiki wapo karibu na watawala na imefikia pahali sasa wakiandaa na kuhodhi dhifa za kitaifa kama tukio la uzinduzi wa video ya uzalendo ya wasanii pale Dodoma,birthday ya Kikwete na keki juu,uzinduzi wa mradi wa Malaria miaka kadhaa iliyopita utafikiri hakuna vyombo cha serikali-TBC TVS na Radio!!

Imefikia pahali hadi Raisi na mawaziri wanatumika na kituo hiki binafsi kuandaa jingles za radio huku wakikiacha solemba kituo cha Umma!!!

Hata propaganda za raisi kijana zilianzia clouds Fm 2012 kwa kuwahusisha January Makamba na Zitto kwenye segment ya kitaa kinasema katika kipindi cha XXL na vinginevyo!!

Mauaji ya Rwanda hata na kule Kenya wakati wa uchaguzi yalichochewa na vituo binafsi vya radio kwa kuchochea chuki dhidi ya upande mwingine/kabila lingine na ndio maana kuna wakurugenzi kadhaa wameshitakiwa kimataifa,clouds nao naona hawaridhiki na faida wanazopata na sasa wanajiingiza kwenye chuki za siasa kwa hadaa za uzalendo!!!
 
kaka, ni kwamba mtu makini hawezi kusikiliza clouds radio wala kuangalia TV yao, kwanza hakika huwezi kujifunza chochote kile, hata uangalie toka asubuhi mpaka jioni zaidi utaonyeshwa utupu wa wanawake na lugha za kichochezi kama hizo, pili ndio maana waandishi makini kama akina kayanda ambao wanataruma ya uandishi wameikimbia ile radio, tatu ile radio umeendekeza ukabila kuanzia kwenye kuwatangaza wasanii, mfano sikiliza XXXL, tatu hii radio na TV inatumika kama danguro la kuharibu mabinti na madada zetu angalia BOSS WAO anatumia radio na tv kuwarubuni madada hasa wanao jifanya wako THT rejea ugomvi wa YAHYA NA JIDE, radio clouds na tv nashauri TCRA IWAFUNGIE

Mkuu TCRA haina meno ya kuing'ata clouds media zaidi ya kucheka cheka nayo kwani kuna utatu kharamu unajengeka wa Clouds +serikali+CCM = PROPAGANDA ZA KISIASA NA UTAWALA,labda wapatikane wakina Suarez!!
 
Clouds imekuwa ikifanya kazi ya radio na gazeti uhuru siwezi kushangaa hata kidogo wakifanya mchezo huo mchafu nachotaka kuwaambia uelewa wa wananchi sasa hivi si sawa na miaka ya nyuma na ndiyo maana ITV walichukua tuzo ya kituo bora cha televisheni siyo kwamba walipata tuzo kwa bahati mbaya ni uelewa wa watu kiuchambuzi
 
Katika tv zilizonyuma Tz nahisi hiyo tv.

Mimi ninayo kwenye king'amuzi lakini huwa siiangalii kama ambavyo siangalii TBC.Hivi huwa wana vipindi gani . Na hicho mlichotaja kinaonyeshwa lini na saa ngapi wakuu?
 
Mimi ninayo kwenye king'amuzi lakini huwa siiangalii kama ambavyo siangalii TBC.Hivi huwa wana vipindi gani . Na hicho mlichotaja kinaonyeshwa lini na saa ngapi wakuu?

Mkuu ni tangazo la dakika 3 hivi ambalo linaonyeshwa kwa nyakati tofauti tofauti na mostly saa moja na nusu ya usiku kabla ya habari!!!
 
Chadema walisema watahakikisha nchi haitawaliki

Nakujibu ingawa huwa sipendi kupoteza mda ku-argue na watu wanaolipwa kwa posts kutetea upuuzi na sio kwa msukumo wa uzalendo na mapenzi ya Taifa hili na watu wake!!

Rejea kauli ya Gen Abdallah Shimbo siku kadhaa kabla ya uchaguzi mkuu 2010 ambapo aliitisha waandishi wa habari huku yeye akiwa kama mnadhimu mkuu wa jeshi!!

Rejea kauli ya Waziri Mkuu ndani ya bunge wakati wa vuguvvugu la gesi kule Mtwara alipotoa amri kwa jeshi la Polisi na jeshi ya kuvunja katiba ya nchi kuwa watu wapigwe tu!!!

Rejea Kauli ya Mizengo Pinda pale aliposema kuwa wanaojihusha na mauwaji ya albino wauliwe wakipatikana,pasipokushitakiwa mahakamani!!!

Rejea Kauli ya Kikwete pale Diamond Jubilee alipotoa hotuba ya kupinga mgomo wa wafanyakazi wakiwa wanaongozwa na Mr Mgaya na kuwaambia wakithubutu kuandamana wataambulia mkongo'to na ameruhusu washughulikiwe!!

Ukisharejea hapo then azima busara uje useme hivyo vitendo vinadumisha amani ama??!! Je ndio hatua za kutoa hukumu kwa mkondo wa sheria??!!
 
"TUTAHAKIKISHA NCHI HAITAWALIKI"- Padre Slaa
 
Mkuu ni tangazo la dakika 3 hivi ambalo linaonyeshwa kwa nyakati tofauti tofauti na mostly saa moja na nusu ya usiku kabla ya habari!!!

asante mkuu ingawaje ni ngumu sana kuiangalia.
 
You clearly do not understand the argument made by MoudyBoka . So, your comment is utterly irrelevant.

Mkuu,ignore him,he is a robot from Lumumba street and has been formated to defend his master and his allience!!!
 
Clouds Tv? huku kwetu Serengeti hata Tbccm haionekani seuse clouds!sisi tunaangalia KBC na CITZENTV basi.
 
Hivi kuna haja ya kuihofia a tv hii kweli , matangazo yake yanaanzia posta na kuishia Magomeni Mapipa ........
 
Hiki kituo cha mashoga kisitupozee muda! Imefikia wakati wanapigana studio kugombania mabwana huku kipindi kikiendelea
 
Back
Top Bottom