Clouds kwa hili la Clouds Plus mmezidi!

Clouds kwa hili la Clouds Plus mmezidi!

~~>>>Acha kulalamika.. Kama unaona anakudhulumu acha kilipia. Kwani umelazimishwa???
 
~~>>>Acha kulalamika.. Kama unaona anakudhulumu acha kilipia. Kwani umelazimishwa???
Utakuwa mbuzi kama unahisi kuhoji ni kulalamika, mwanadamu ni lazima utafute why? Katika kila jambo si tu kukubali kisa umeletewa. Acha tuwasaidie na wengine we nenda kamliwaze mkeo kitandani
 
Haya mambo mengine yawe nami mapka basis hata kma kutafuta cyo tena kihivi yani ulipie king'amuzi alafu bado tena ulipie channel iliyoopo kwenye king'amuzi yani ni swa nakulipia ving'amuzi viwili kwa wakati mmoja wapiga dili bado wapo

Sent using Jamii Forums mobile app
Kuna wizi wa kutumia shule ndo huu mkuu. Kama shule hamna kichwani watu wa hivi watawapata wengi sana, si unajua wajinga ndio waliwao
 
Watanzania watu wa hovyo sana na ndo maana mnatesana sana na kuishi kwa visasi. Sishangai kuona wenzetu wakilalamika kwenye huduma kuongezeka hata senti lakini kwa hapa Tz utaitwa mwehu ... Labda kwa kukusaidia, si kila anayesema basi kashindwa hilo jambo.

Naamini nimeanza kuitumia Azam hata kabla labda hujawaza kuitumia kama kweli unayo na huu ni mwaka wa 5 sasa unaisha naitumia Azam na ukitaka reg# yangu pia ntakupa ukahiki. Nimelipa vifurushi vyote kwa utashi wangu na hakuna mwezi sijalipia wala kukwama kulipa.

Kwahiyo usifikilie tunaongea kisa hatuwezi kumudu ama labda ni pesa nyingi, lah! Tunaongea kama watanzania na kama jamii ya watanzania. Tunaelewa pia ni soko huria lakini mwanadamu unahitaji kuhoji na kutafiti kwasababu una utashi na haliwezi kuwa kosa. Si ajabu kuhoji kwangu hapa kuna kitu nadevelop ambacho wewe huwezi kukielewa badala yake utaona tu eti watu wanalalamika.

Usipende kudharau vitu vidogo ukafikiri ni vikubwa pekee ndo vinakufanya kuwa mwanadamu ama kwasababu tu wewe vidogo vyote unavyo. Katika kuongea hivi tunapata nafasi ya kuwasaidia wengine wengi sana na ndo maana ya kuongea haijalishi hicho kitu kwako kinahusika kiasi gani.
Grow big and not fat!

Kuangalia Clouds Plus ni hiyari Jamaa ameiweka kibiashara hivyo kama unahitaji lipia, mbona Azam walipoongeza Azam sports2 wameoongeza elfu tatu ili uione? kifurushi mwanzo kilikuwa 15,000/= lakin kwa sasa tunalipa 18,000/= hilo hujaliona na wewe unasema nimtumiaji wa muda mrefu wa AzamTv, ukilipia ile 15,000/= huoni Azam Sport2. Acha chuki binafsi kama huwezi lipia piga kimya
 
ndiyo maana imeitwa Clouds plus yaani wewe plus 3000 kama hutaki unaacha tu.
 
Download Afrobox japo ni yao, me naTafuta App ambayo in Channels za tz, at the end huyu lazma niangalie kvyovyote bila buku3.
Ukipiga hesabu ya bundle unayotumia kutizama via afrobox utakuta ni heri ulipe hiyo 3000 kwa mwez maana kutazama channels online kunahutaji bundle ya kutosha so kwa mwezi utatumia kiasi gani.
Hapo ni sawa na kuruka mkojo ukakanyaga mavi
 
ndiyo maana imeitwa Clouds plus yaani wewe plus 3000 kama hutaki unaacha tu.
Watanzania watu wa ajabu kweli, hii channel haina hata miezi mitatu toka iongezwe.
Wakati haipo wala hawakulalamika, kwahiyo kama mtu anaona kulipia 3000 ni bei si anaipotezea tu kama vile kipindi ambapo haikuwepo.
Mbona azam sports2 hawalalamiki inapowabidi walipie 3000 zaidi kuipata.
Wengine wanadai kuwa haina chochote, lakini still wanalalamika kutoiona.
Mimi personally sioni la maana kwenye hiyo clouds plus na siwezi kuilipia maana haina effect kwangu.
Mimi channel nnayopenda ni IDX, discovery na national geographic yani hizo hata wangesema kuipata IDx uongeze 3000 ngelipa tu.
 
Huyu Ruge na uongozi wake wana njaa ya tumbo kinouma.. mambo gani sasa haya wanaleta... hivi huko plus kuna nn cha ajabu...!!!
 
Slogan yao sasa wanasema fursa inaanzia sokoni kwa hiyo kafanya king'amuzi cha azamu kama soko kisha kaleta biashara yake ya clouds plus now anapiga tu hela buku 3 tatu
 
kaz kwa wapenda fiesta/clouds....... c wengine hatuna presha.
 
Wangeachia Rai Italy kwenye kifurushi cha 18000/- halafu wangefuta channel zote za bongo movie ningefurahi sana kwangu mimi binafsi.
 
Ni ajabu wewe kila kitu unatafuta jinsi ya kuteka pesa iwe kiharali ama kwa mizengwe. Sie watumiaji wa Azam TV tuna vifurushi vyetu 3 ambavyo kwa idadi ya chaneli zote zilizopo zitapatikana pale utakapoweza kulipia kile cha juu kabisa. Sasa sijui huu ndo utaratibu gani kwamba unaamua kachaneli kako ka clouds plus basi wewe unaingia na kifurushi chako cha kipekee kabisa na unahitaji 3000.

Kwamba naweza nikalipia kifurushi cha juu kabisa na nikapata zote ziwe za ndani ama nje, michezo ama habari, vichekesho ama burudani na ntazipata zote isipokuwa ile ya kwako ya Clouds Plus. Hii ni hatari, inaonesha ni kwa kiasi gani wewe ni wa kipekee lakini pia labda chaneli yako ni ya kipekee na nzito kupita zote katika dekoda nzima ya Azam TV .

Najiuliza tu, ikiwa na Azam angesema sie wanamichezo tunatakiwa kulipia labda 5000 kwa ajiri ya chaneli ya Azam sports2 na labda ikasemwa pia kwa sie wafatiliaji wa muvi za Nigeria tukaambiwa tulipie 3000 ili kuiona Chaneli ya AMC sielewi kama leo watizamaji tungeweza kweli kugharamia dekoda kama dekoda na bado tukaweza kumudu kulipia kila chaneli kwa pesa yake. Tunamshukuru sana Bakhresa kwa hili ijapo bado wengi wetu tunajiuliza ni nini haswa nia ya Ruge na Clouds Plus yake.

Kama ni njaa ya pesa basi hii itakuwa ni hatari sana. Tunaelewa umetoka kuchukua viingilio vya ndondo, sahivi unajiandaa kupiga za Fiesta na bado inakuingia akilini kuchajisha bei yako kwa ajiri ya chaneli yako tukufu. Huu kama siyo kukosa utu na aibu basi itakuwa ni tamaa kali sana. Ingekuwa ndo mwendo kwamba tulipie kila kitu kwa kitu sijui kama kweli tungefika, haya bwana.
Kwani kwenye hiyo channel kuna nini cha ziada? Kama ni michezo ukilipa 15 kuna channel kibao, kama ni muvi za kibongo sinema zetu IPO, kama ni muziki zipo kibao; mfano etc, eatv, AZAM 2 NA za nje. Clouds plus kuna nn special? Naomba mnijuze. Ikiwezekana kwe dikoda yangu waiondoe tu hiyo channel sina haja nayo.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Jamaa anajua kucheza na akili za watu..achana name hilo.hebu fikiria kaja na tatu mzuka..yote hiyo ni kutengeneza mifereji ya pesa..ila uzuri ni kwamba hulazimishwi..uamuzi ni wako.
Mbona hiyo tatu mzuka iko kila mahali, EA RADIO ipo na hata huko kenya ipo.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Huu ni ujinga tcra wamelala tu

“Start where you are. Use what you have. Do what you can.”

 
Back
Top Bottom