Ngalikihinja
JF-Expert Member
- Sep 1, 2009
- 34,637
- 38,026
Tumerudi enzi za ujima
Mtangazaji wa Clouds FM Radio leo asubuhi katika kipindi cha Power Breakfast - Jicho la ng'ombe amesema ni sahihi kabisa kwa bunge kutooneshwa live kwa sababu wao wanaamini ndio sababu ya wabunge kuvunja kanuni za bunge kwa kupoteza muda kujadili mambo yasiyo ya msingi na kuacha yale ya msingi.
Anasema kwa sababu wanajua wanaonekana basi mbwembwe, madoido, mihemko, mshawasha na mengine mengi yamekuwa yakifanywa na wabunge isivyo kawaida.
Anadai anashukuru kwa katibu wa bunge kuliona hilo.
Wazo langu:
Je, mtangazaji huyu anajua maana ya demokrasia? Haki za binadamu? Katiba ya jamuhuri ya Tanzania 1977?
Na anachoshabikia ni kwa maslai ya taifa? Je, anachokubaliana nacho ndicho walicholenga walioleta swala la kutoonesha bunge live?
Na kweli maana utawasikia wakisema.... CLOUD SI REDIO YA KUSIKILIZA........ TUWASUSIE KUWASIKILIA..... lakini mara wanakuja na thread iwahusuyo Clouds, sasa unaanzishaje thread kama huwasikilizi? mnapoanzisha thread za kutuhamasisha tuwasusie ndo wanapata uhakika kuwa wanasikilizwa vinginevyo wakipotea humu JF watajuwa hawasikilizwi. SOMETIMES UJINGA WA MTU NDO UNAAMSHA BUSARA ZAKO, NA TUJAJUWA UWEPO WA WENYE AKILI KWA UWEPO WA WAJINGA... UKIWAONDOA WAJINGA DUNIANI HUTAJUWA NANI ANA AKILI..Mimi nadhani tu hitimisho ni kwamba Sikiliza Redio Clouds at your own risk, tumeshachoka na kelele kuhusu clouds Fm.
chukua like 100.Kumbe hii radio bado ipo eeh, king'amuzi changu hakiikamati kabisa....
Kama nchi hii ni ya kipumbavu kiasi kwamba tunashindwa kusimamia sheria na waandishi wa habari wanaunga mkono basi umaskini tulio nao ni halali yetu. Tuendelee humu humu kwenye vicious cycle. Bunge linazo kanuni na taratibu za kushugulikia wavunja kanuni, inakuwaje zisitumike hizo. Basi tuzuie madaladala yasitembee mjini kwa kuwa madereva wake wanavunja sheria za barabarani,,, hapana, atakayevunja sheria ashugulikiwe ipasavyo. Ndani ya bunge kuna spika dhaifu anayeshindwa hata kuwaadhibu wavunja kanuni za bunge, and in fact spika ndio bingwa wa kuvunja kanuni.
Hii radio watangazaji mabwabwa wengi, hawana uhuru wa kueleza wanachokiamini
Clouds majinga tu
........
Alaf hawajali muda kabisa, wanatumia muda wa kipindi kingine kujadili ushuzi tu. Eti wanabishana kama tv ina kiuno! watu wazima kabisa yan!mie daima huwa siikubali hata kidogo hii media maana wamejaa uashbiki majungu na umbea
Wewe kwako labda spotsi ekstra, mwingine labda leo tena, mwingine labda power breakfast, mwingine labda jahazi, mwingine labda ala za roho.... MWISHO WA SIKU WANASILIZWA MUDA WOTE... Ni ukweli usiopingika kuwa hakuna mtu anayependa na kusikiliza vipindi vyote yva redio fulani, iwe unaipenda au la..... kwa hiyo na kwa clouds hivyo, tumegawana vipindi hata kama tunaikandya.. WEWE UMEJIGAWIA SPORTS EXTRA NA MWINGINE KINGINEchukua like 100.
hii redio itakuwa na mabwabwa kibao, mie nishaacha zaman kusikiliza labda tu sports extra. kwanza redio ya kihuni tu vipindi havianzi kwa wakati, baadala ya saa tatu kamili usiku utakuta wanazidisha dk 10, huku nako kale kabinti kanaingiza sauti yake eti kameliwa muda wake wa kuongea upuuzi kuharibu watoto wetu tu. very disorganized kabisa.
Ni ukweli usiopingika kuwa hata usome vipi, burudani nyingi tunapata toka kwa wa LY (la saba), waliokataa shule ... etc. etc.. Kwa mfano, diamond anapendwa sana lakini kaishia level ipi ya elimu? Haya akina Twanga, FM akademi, Aunt Ezekiel, LULU, kaole wote, etc etc mzee Yusuph wanaburudidha wenye masters, PhD, Degree mbalimbali, lakini uelewa wao na shule zao ndo kama akina Clouds.... Mr Blue kaishia la ngapi? lakini tunaburudishwa naye... akina Barnarba, Linah, Lady JD yale yale tu.... Tuwaseme clouds kwa uelewa wao lakini pia tuwaseme wanaofanana na wao isije ikawa CHUKI BINAFSIHao watangazaj uelewa wao ni mdogo sana.sijajua CV zao.lkn inaonesha pass-mark zao zpo chini sn.ila kwa vle mungu kawapa uwezo wa kuongea,kwa maana co mabubu,ndo wanajiropokea.nlikuwa napenda sn kuickilza radio hyo kila nkienda job,na-tune station hyo.kwa sasa,completely cwez ckiliza tangu nigundue wana akili ndogo sn ya kuweza kuniongeza ki2!
hawa watu wanachekesha. juzi sote tulikuwa tunaangaika kuangalia mdahalo wa wagombea urais Kenya na kable ya hapo ilikuwa USA. Hivi kweli sisi tukiwa na mdahalo kama ule, kweli unadhani ni watu wangapi (ordinary people) watahangaika kutuangalia?Tumerudi enzi za ujima