Clouds FM (Power Breakfast): Ni sahihi kabisa Bunge lisionyeshwe LIVE!

Clouds FM (Power Breakfast): Ni sahihi kabisa Bunge lisionyeshwe LIVE!

Status
Not open for further replies.
kituo kimejaa mabwabwa tu,unprofessional journalists "makanjanja" wanataka wajipendekeze nao wapate ukuuu wa wilaya..wanazungumza mambo ya "kisoro" kweli na ni watu wazima kabisa na akili zao.hoja za msingi na maana zinazogusa maslahi mya wengi kupata taaarifa wanaona kwao hazina maana!!!!! wapuuuzi kweli hao

si muda wote wana porojo. Kadhalika huwa wanasaidia kuondoa stress kama huwa unasikiliza jahazi
 
clouds fm kuna hawa watu wawili gerald hando na ephrahim kibonde
1. Wanahamishia personal issues na feelings zao +/- redioni
2. Uchaguzi wao wa maneno ni mbovu kupindukia

ila kwa kweli watangazaji wengine clouds fm wako poa, mfano mmoja ni millard ayo.
 
Naomba ni wakumbushe kitu kidogo Moja ya vitu vilivochangia Genocide Rwanda Ni Vyombo vya habari Hususan Watangazaji wa Redio.Maana yake ni Kama Kuna Watangazaji Ambao hawajui kuchuja mambo na kusema yale tu ambayo wanapaswa kusema Utangazaji style hiyo ni hatari...Jamani Siolazima kila kitu ujifanye unataka kutoa maoni vingine Kaa kimya..Kiukweli so mara ya kwanza hao ndugu wanatoka nje ya mstari So guys naamini mnaelimu ya hiko mnachokifanya so Msitukane Elimu yenu
 
Mtangazaji anayeharibu kazi pale clouds ni Ephraem Kibonde, kwanza ni mbabe sana hoja zake nyingi ni za kibabe, yupo biased mno na aache tabia ya kujisifia kwa kila kitu. kile ni chombo ambacho kinasikilizwa na watanzania wote . sio ooh mara gari langu, watoto wangu, mke wangu mzuri sana, mke wanu ni mpishi mzuri sana, so what, akiwa mpishi mzuri anakusaidia wewe na familia yako na sio sisi watanzania. wengine kwa kweli siku hizi sisi tumehamia channel zingine maanake tunakuwa bored mno kutokana na tabia ya baadhi ya watangazaji wakiongozwa nakibonde.
 
Wiki mbili zilizopita kwenye PB Paul James alimwuliza swali la kisheria Gerald Hando, Gerald akasema sifaham ila ngoja tumulize Barbra atakua anajua maana previous boyfriend wake alikua mwanasheria! Sikuamini nlichoskia..personal issues za mtangazaji mwenzako unaziweka wazi kiasi hicho! Mwanzoni nlidhani anatania ila reaction ya Barbra ndo ikanionesha kuwa Hando karopoka! Maskini mdada wa watu alihamaki na kuweka tangazo ili kupotezea wakati PJ anaongea!
 
Inasikitisha sana kwa clouds kuwa kinyume na hoja nyingi zenye maslahi mapana kwa taifa.Binafsi ni kijana mdogo,nlkuwa mdau wa redio,lkn napoteza ham kabsa ya kutune hii radio.

Nimekuwa nikijiuliza,iv kijana wa tanzania anahitaj burudan kubwa kias hcho frm clouds coz hawana kpindi very substantial kwa vijana!cku hz namskilizaga shafii dauda2.Eti loveness love(dva),huyu dada anahamasisha ngono2 na si love km mantiki ya neno ilivo.Clouds ni janga kwa vijana na taifa zma.
 
bunge wamekosea. acha tuone wawakilishi wetu wanachosema. tuone hoja zao. tuone kama wanaishia kupiga usingiz tu au la kule mjengoni. tuone kama wanaishia kusifiana tu na kutumia muda mwingi kukaribisha wageni na ndugu zao na watu waliowasaidia kwenye uchaguz. tuone kama wanawajibika ipasavo huko. kaz ya bunge ni kusimamia serikali. acha tuone hyo sirikali inavyosimamiwa. acha tuwape sifa wabunge wanaoisimamia vzur
 
Nasubiri kuona reaction ya vyombo vya habari na sisi wananchi!

Hivi bunge kuoneshwa live ni hisani? Tuache ujuha tena tulipaswa kukemea hili kwa nguvu zote!

Kuhusu Clouds tuwaache jamani tujadili hoja hakuna watu wenye akili timamu mle!

Watu wanatafuta Ukuu wa Wilaya na Ubunge. Subirini mtaona kadiri siku zinavyoenda. Dunia inapigania uhuru wa habari na demokrasia, kutoonyesha Bunge live ni harakati za kulinda ufisadi na ubovu wa jinsi Bunge linavyoendeshwa kwa manufaa ya wachache. Wanachotaka mafisadi kupitia Bunge hili, habari iwe inachujwa kwa manufaa yao. Hawataki itokee tena Wassira amulikwe akiwa amepiga usingizi wa mchana!!

Shame on Clouds FM.
 
Tangu jana baada ya katibu wa bunge kutangaza mpango wa kusitisha kutoonyesha live matangazo ya bunge. Radio clouds fm kupitia kipindi cha jana na leo asubuhi Power Breakfast - Jicho la ng'ombe wanaunga mkono hoja ya katibu wa bunge kuwa ni sahihi kabisa kwa bunge kutooneshwa live kwa sababu wao wanaamini ndio sababu ya wabunge kuvunja kanuni za bunge kwa kupoteza muda kujadili mambo yasiyo ya msingi na kuacha yale ya msingi.

Ni lini clouds FM au clouds TV waliwahi kurusha matangazo ya bunge live? Hii radio imeibuka na tabia ya kudandia hoja na kutetea jambo linalotangazwa na CCM au serikali. Miaka ya nyuma radio hii ilionekana kuwa na mvuto kwa jamii kwaani haikuwa na mlengo wa kisiasa. Lakini siku zinavyoenda ndiyo inazidi kuharibu utamu wa habari kwa wasikilizaji. Kwa hili la bunge clouds FM wamechemsha kwani siyo hoja yao kwa sababu hawajawahi kurusha matangazo ya bunge live kwa TV au Radio. Tunawashukuru TBC na STAR TV kuteletea habari za bunge live. Clouds media acheni kutafuta umaarufu nyie bado wachanga hata matangazo yenu bado ya kitoto. Ndiyo maana utakuta vipindi vyenu ni vya kitoto kama jicho la ng’ombe, leo tena, jahazi, heka heka. Ushauri: Watangazaji fanyeni kwanza utafiti kabla ya kuanza kuitetea serikali na CCM. Tunajua kuwa baadhi ya watangazaji ni makada wa CCM lakini msitumie taaluma zenu vibaya.
Tunajua kipindi cha bunge watu hawasilizi clouds radio fm hivyo mnakosa wasikilizaji. Bunge lililochangamka limesababisha kupendwa na wananchi tofauti na bunge la miaka ya nyuma. mfano miaka ya nyuma ukienda Salon za nywele usingeweza kuwakuta vijana wanaangalia bunge, lakini kwa sasa bunge lina mvuto kuangalia. Clouds Media mmefulia.
 
Nipe qualifications zao ni-analyze uwezo wao wa kuchambua mambo hasa yanayowagusa wenye nnchi.
 
tangu jana baada ya katibu wa bunge kutangaza mpango wa kusitisha kutoonyesha live matangazo ya bunge. Radio clouds fm kupitia kipindi cha jana na leo asubuhi power breakfast - jicho la ng'ombe wanaunga mkono hoja ya katibu wa bunge kuwa ni sahihi kabisa kwa bunge kutooneshwa live kwa sababu wao wanaamini ndio sababu ya wabunge kuvunja kanuni za bunge kwa kupoteza muda kujadili mambo yasiyo ya msingi na kuacha yale ya msingi.

Ni lini clouds fm au clouds tv waliwahi kurusha matangazo ya bunge live? Hii radio imeibuka na tabia ya kudandia hoja na kutetea jambo linalotangazwa na ccm au serikali. Miaka ya nyuma radio hii ilionekana kuwa na mvuto kwa jamii kwaani haikuwa na mlengo wa kisiasa. Lakini siku zinavyoenda ndiyo inazidi kuharibu utamu wa habari kwa wasikilizaji. Kwa hili la bunge clouds fm wamechemsha kwani siyo hoja yao kwa sababu hawajawahi kurusha matangazo ya bunge live kwa tv au radio. Tunawashukuru tbc na star tv kuteletea habari za bunge live. Clouds media acheni kutafuta umaarufu nyie bado wachanga hata matangazo yenu bado ya kitoto. Ndiyo maana utakuta vipindi vyenu ni vya kitoto kama jicho la ng'ombe, leo tena, jahazi, heka heka. Ushauri: Watangazaji fanyeni kwanza utafiti kabla ya kuanza kuitetea serikali na ccm. Tunajua kuwa baadhi ya watangazaji ni makada wa ccm lakini msitumie taaluma zenu vibaya.
Tunajua kipindi cha bunge watu hawasilizi clouds radio fm hivyo mnakosa wasikilizaji. Bunge lililochangamka limesababisha kupendwa na wananchi tofauti na bunge la miaka ya nyuma. Mfano miaka ya nyuma ukienda salon za nywele usingeweza kuwakuta vijana wanaangalia bunge, lakini kwa sasa bunge lina mvuto kuangalia. Clouds media mmefulia.


mode hii ilikuwa habari tofauti. Siyo mwendelezo wa hii.
 
kuliko kupunguza stress na jahazi,bora nishushie kinywaji baridii maana ukiwasikiza, unazidi kuongeza stress
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom