kailembo milton
Member
- Jan 13, 2013
- 50
- 7
Hawa watangazaji wa clouds fm,nafikiri nao ni magamba,hawana tofauti na spika wa bunge na kaimu wake!
Mtangazaji wa Clouds FM Radio leo asubuhi katika kipindi cha Power Breakfast - Jicho la ng'ombe amesema ni sahihi kabisa kwa bunge kutooneshwa live kwa sababu wao wanaamini ndio sababu ya wabunge kuvunja kanuni za bunge kwa kupoteza muda kujadili mambo yasiyo ya msingi na kuacha yale ya msingi.
Anasema kwa sababu wanajua wanaonekana basi mbwembwe, madoido, mihemko, mshawasha na mengine mengi yamekuwa yakifanywa na wabunge isivyo kawaida.
Anadai anashukuru kwa katibu wa bunge kuliona hilo.
Wazo langu:
Je, mtangazaji huyu anajua maana ya demokrasia? Haki za binadamu? Katiba ya jamuhuri ya Tanzania 1977?
Na anachoshabikia ni kwa maslai ya taifa? Je, anachokubaliana nacho ndicho walicholenga walioleta swala la kutoonesha bunge live?
....baada ya tamko kuwa katibu alinukuliwa vibaya, wanasemaje tena...!!
kwani wao sio Watanzania?au unaposema Watanzania unakusudia nini?