Clouds FM acheni Utoto

Clouds FM acheni Utoto

kwa nn aliongea hayo??? kosa ni la nani?? ukiona mtu kafikia hatua ya kutoa kaulo hizo lazima ujipime ulichomkosea mlalamikaji huenda walimfanyia kitu mbaya sna dada wa watu.
Hapa hatuangalii nani alitenda kosa hapa tunaangalia nini kilifuatia baadae! Iwe Clouds ndio wakosaji au hapana, ukweli bado unabaki pale pale kwamba ni Jay Dee mwenyewe ndie alikataza nyimbo zake kupigwa; tena hakukataza kiuungwana, na full kejeli na kujitapa kwamba anaanzisha radio yake... miezi inapita, hiyo radio hatuioni.... watu mkaanza kudanganyana kwamba EFM ndo radio ya Radio! But in addition, wimbo unaozungumziwa hapa ni Alikufa kwa Ngoma ambayo ni ya Mwana FA, Mwana FA na Jay Dee nao hawapo kwenye good terms! Imeshatokea si mara moja wala mara mbili msanii kufuta mistari ya msanii aliyekuwa amemshirikisha kv tu they're no longer in good terms! Hili lilitokea kwa Zay B Vs Nature na hata Diamond na Kiba, bifu lao lilianzia huko... wakafutiana mistari ambayo walishirikiana! So, what if hata Mwana-FA mwenyewe hayupo ready kusikia sauti ya Jide kwenye nyimbo zake??

Kwamba ukiona mtu kafikia kutoa kauli hizo lazima ujipime, hakuna asiyefahamu kwamba Jide ni mtu aliyejaa majivuno, jeuri, dharau na maneno machafu! Jide ni mtu asieyechanganyika na wasanii wenzake lakini bado hilo halimzuii kuingia kwenye migogoro na wasanii wenzake! Katika hali ya kawaida, kv hayupo karibu na wenzake basi hata migogoro kwake isingekua imetokea! Napoteza muda kuongea mengi, lakini hivi karibuni tu tumeshuhudia anavyotumia social networks kusema maovu ya mumewe... mumewe ambae, pamoja na ukaribu wake na watu wa Clouds, lakini wakati wa bifu lao aliamua kusimama pamoja na mkewe! Kwahiyo mtu kama huyo ni ngumu kufikia conclusion kwamba walionza ukorofi ni Clouds! Leo hii Stara Thomas akiingia kwenye mgogoro na yeyote, lazima wadau watajiuliza, what's wrong lakini sio kwa Jide!
 
#Nazdaz tatizo la hawa vijana wa fb ni kupenda kushadadia mambo wasiyoyajua. Muda wote wanawaza siasa tu matokeo yake wanapeleka siasa hata kusikostahili. Kulalama na kulalamika ndo imegeuka kuwa jadi ya Mtanzania. Basi wameamua kuchagua maisha ya kulalamika ni bora wakawa wakweli kwa kila upande badala ya hizi ngonjera za double standards tunazoziona humu kila siku.

FidQ alikua na kipindi pale EATV sijui kimeishia wapi lakini nakumbuka kwenye wimbo wake kachana ukweli kuwa, HAKUNA UHURU WA VYOMBO VYA HABARI, BALI KUNA UHURU WA MWENYE CHOMBO CHA HABARI. KAMWE IPP HAIWEZI KUMPINGA MENGI. Nadhani hakumlenga mengi kama mengi bali alimtolea mfano kuwa vyombo vya habari vipo kwa ajili ya wamiliki wake na sio wananchi. Kwahiyo hizi ngonjera za kuwa mnakuja hapa kushambulia MEDIA Moja ni vyema mkaachana nazo kwani huu ni mfumo na sio suala la mtu binafsi. Na utakapoamua kulielezea ni bora ukawaambia wamiliki wote wa vyombo vya habari kuanzia IPP,CLOUDS GROUP, SAHARA, UHURU, MAGIC,TIMES,MAWIO, TANZANIA DAIMA, NIPASHE nk.
Hilo la siasa hata mie nimeshapata kulisema kwenye posts za nyuma... unajua kuna watu kibao sio watu wa burudani wengine wameijua burudani baada ya kuja mjini na hata wale waliokulia mjini kuna wengine wamekuja kuijua burudani baada ya kutoka kwenye vifungo vya wazazi wao... baada ya kumaliza shule na labda kuingia chuo mwaka wa kwanza ndipo wakaanza kufunguka macho! Hawa wote huwa wanachanganya siasa na burudani kv burudani sio ada yao na haipo kwenye damu zao!! Hawa ni wale ambao wala hawafahamu pale Billz watu wanatimba kila leo bila kujali kwamba mmiliki ni mwenyekiti wa chama fulani cha siasa! Lakini hawa watu waliokurupukia burudani ukubwani, kama Billz ingekuwa inamilikiwa na mtu yule wasiyemuunga mkono kisiasa, kila siku hapa tungeona posts kuhusu Billz! Wengi wao bifu lao na Clouds lilianzia kwa Kibonde ambae kwa asili huwa achgui cha kuongea... hajali kama utachukia au hautachukia! Sugu nae alipoingia kwenye bifu na Clouds, nao wakaingia waziwazima....... Jide alipoingia kwenye bifu, nao wote wakamfuata... kwa mara ya kwanza tukashuhudia vituko vya karne kusikia Jide akiitwa kamanda!

Wapo miongoni ambao wala hawasumbuliwi na hizi siasa lakini hawa ni wale wanaovamia mambo bila kuyafanyia utafiti... ili mradi wenye sauti ya juu wamesema hivi, wao wanameza tu!!
 
Hiyo redio sijawahi kuisikiliza kwa utashi wangu, labda kwenye daladala au nyumbani kwa mtu
 
#Nazdaz tatizo la hawa vijana wa fb ni kupenda kushadadia mambo wasiyoyajua. Muda wote wanawaza siasa tu matokeo yake wanapeleka siasa hata kusikostahili. Kulalama na kulalamika ndo imegeuka kuwa jadi ya Mtanzania. Basi wameamua kuchagua maisha ya kulalamika ni bora wakawa wakweli kwa kila upande badala ya hizi ngonjera za double standards tunazoziona humu kila siku.

FidQ alikua na kipindi pale EATV sijui kimeishia wapi lakini nakumbuka kwenye wimbo wake kachana ukweli kuwa, HAKUNA UHURU WA VYOMBO VYA HABARI, BALI KUNA UHURU WA MWENYE CHOMBO CHA HABARI. KAMWE IPP HAIWEZI KUMPINGA MENGI. Nadhani hakumlenga mengi kama mengi bali alimtolea mfano kuwa vyombo vya habari vipo kwa ajili ya wamiliki wake na sio wananchi. Kwahiyo hizi ngonjera za kuwa mnakuja hapa kushambulia MEDIA Moja ni vyema mkaachana nazo kwani huu ni mfumo na sio suala la mtu binafsi. Na utakapoamua kulielezea ni bora ukawaambia wamiliki wote wa vyombo vya habari kuanzia IPP,CLOUDS GROUP, SAHARA, UHURU, MAGIC,TIMES,MAWIO, TANZANIA DAIMA, NIPASHE nk.

Kujifanya hamsikii haiwasaidii wala haiwajengi/Ninachosema ni kamwe IPP haitompinga Mengi hahahahaaa kile kipindi Mengi ana bifu zito na Rostam Aziz alishawahi kufuta taarifa ya habari ya saa mbili usiku akatumia zaidi ya masaa mawili kumjibu Rostam kuanzia ITV,East Africa Tv,Capital TV mpaka na Redioni alikua anaongea yeye tena ilikua exclusive live mbona watu hawakuongea yule ni mmiliki na ule ndo uamuzi aliochukua hakuna tatizo hata hao TBC wenyewe wapinzani hawawaongelei vizuri sana hasa Chadema so huo uamuzi ni wa kwao na hawavunji sheria za TCRA
 
Clouds ni media kipuuzi sana.
Hivi hii redio bado ina wasikilizaji?
Wanajishushia hadhi sana,Kampuni kubwa kuwa na beef na msanii? Ni Kichekesho sana.
Hivi clouds fm ni kitu gani hicho!?
nshamalizana nao hawa, wajinga sana, hii sio mara ya kwanza, siwapi audience yangu.
Clouds FM wajinga sana...!! Nawachukia mpaka basi..
Ni takataka fulani hivi ya makelele
Mnapata wapi muda ya kusikiliza radio ya wapuuzi wa design hii??
bahati mbaya hata sisikilizi redio
hii ndio bora radio fm na sio radio bora
Wananikera sauti zao hasahasa hicho kipindi, wanajifanya sauti za kidhungu
Hivi hii redio bado ipo hewani?
Mtu mwerevu mwenye akili zake timamu hawez kuiskiliza clouds wala kuitizama.. Cause imejaa mitoto ya uswaz iliyokosa nizamu
Hawa Wafu Fm kiboko yao Sugu tuu.
Hofu yangu ni kwamba, wote nyinyi na wengine kama nyinyi mchango wenu ni sawa na tone la maji kwenye bahari! Si tu kwamba mnajifanya hamuisikilizi wakati mnaisikiliza lakini hata msipoisikiliza, effect take is almost negligible coz', wakati nyie mnajidai hamuisikilizi, there're millions outta there wanaoisikiliza including hao wasanii mnaojifanya kuwatetea!! By the way, Clouds FM ni nini hasa?
CLOUDS-WITH-MINISTER.jpg

Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu – Uwekezaji na Uwezeshaji, Dk Mary Nagu (kati) pamoja na Mkurugenzi wa Mradi wa Superbrands Afrika Mashariki, Bw Jawad Jaffer kwa pamoja wakimkabidhi cheti Mkurugenzi Mtendaji wa Clouds Media Group,Bwa.Joseph Kusaga kwa Clouds Fm redio kuibuka na tuzo hiyo ya ubora kwa mara ya tatu mfululizo. Tukio hilo lilifanyika hivi karibuni katika hoteli ya Hyatt Regency jijini Dar es Salaam.

So what is "Superbrands"?

According to (Superbrands - Wikipedia, the free encyclopedia) The Superbrands organization is an independent arbiter on branding. Its membership programmes pay tribute to the world's leading brands, as selected by experts and consumers. The organization also publishes a series of brand-focused books and publications. Superbrands has launched its programs in many key global markets and has publications in over 86 countries.


Background


Superbrands was founded by advertising executive Marcel Knobil in London in 1994. It began as a radio show on GLR (now BBC Radio London), which was aimed at giving ordinary customers an insight into the significant brands that touched their lives. Due to the success of the show, the Superbrands organization was founded in 1995.
In each country that it operates, it aims to identify brands that perform above and beyond other brands within their respective markets. To facilitate this, each country has an independent and voluntary council, which is made up of notable experts in the branding and marketing communication industry as well as experts from local and international blue-chip organizations. Brands that are rated highly by both the council and consumers are eligible for inclusion in a Superbrands project. Step 1 Study: an independent study elects the strongest brands of the country called Superbrands. Step 2 Reward and Knowledge; Superbrands Seal of Excellence, The Superbrands book. In some countries they also hold seminars and Awards ceremonies.

What is Superbrands and why it is important

Superbrands has launched programmes in over 88 countries including all the key global markets. These programmes aim to identify those brands that are performing above and beyond others within the market. At the heart of each programme is an independent and voluntary council of leading experts comprising individuals with a deep appreciation of the "brandscape" in the country being examined.

The council comprises luminaries from the marketing and communication industries plus notable figures from local and international blue chip companies and media organisations. Only those brands highly rated by the council are invited to join the Superbrands project. Each country has its own local panel to ensure that only the most deserving of brands attain the credential and feature in the project. More http://superbrandseastafrica.com/about-us/

Top 20 Best Radio Stations In Africa



Even with the invention of the television, radios have remained a vital part of our lives – imagine driving your car without the stereo on. What makes the radio still important is the quality of stations, programs, and presenters that we listen to. Africa has thousands, if not running into millions, radio station all across it. Trying to sift through these numbers to list out 20 best radio stations is no small feat. Having a best radio station is subject to preference, so to avoid having a bias list; we randomly select the top radio stations all over Africa. In no particular order, here are the best radio stations in Africa.

1. Radio Citizen FM – FM 106.7, Kenya
2. Peace FM – FM 104.3, Ghana
3. Nile FM – FM 104.2, Egypt
4. Sheger FM – FM 102.1, Ethiopia
5. Breeze FM – FM 99.6, Zambia
6. Rhythm FM – FM 97.3, Nigeria
7. Clouds FM – 88.5 FM, Tanzania
8. Radio Simba – 97.3 FM, Uganda
9. Ukhozi FM – 90.8 – 107.4 FM, South Africa
10. Radio Wave FM – 96.7 FM, Namibia
11. Chada FM – 100.8 FM, Morocco
12. Radio Tiemeni Siantou – 90.5 FM, Cameroon
13. ZiFM Stereo – 106.4 FM, Zimbabwe
14. Radio Vaovao Mahasoa – 106.8 FM, Madagascar
15. Canal A FM – 96.5 FM, Angola
16. Metro FM – 92.4 FM, South Africa
17. Okay FM – 101.7 FM, Ghana
18. Star FM – 96.6 FM, Gambia
19. Wazobia FM – 95.1 FM, Nigeria
20. SaFM – 107.1 FM, South Africa

See More Top 20 Best Radio Stations in Africa. | Network Africa

Niishie tu kusema kwamba, uwepo wenu unatambulika lakini ndio hivyo tena, hamna effect yoyote kwa Clouds FM
Superbrands2.jpg Best Superbrands.jpg
 
hata tv ya kipuuzi. huwa wanatoa lebo kwenye vchupa za maji
 
Maisha ni kuchagua nadhani clouds FM ndo wamechagua aina hiyo ya maisha na sidhani kama wanavunja sheria ingekua kuna kitu hakipo sawa TCRA wangeingilia kati wao ni taasisi binafsi na wana aina yao ya maisha hivyo tuwaache tu kumbukeni Magic FM kwa muda mrefu walikua hawapigi nyimbo za Diamond mpaka pale walipomaliza tofauti zao pia East Africa Tv n Radio kama sio IPP kwa ujumla kuna wakati nao walikua hawachezi nyimbo za ally kiba audio mpaka video so to me sioni tatizo lolote usipopigwa huku utapigwa kule pia dunia ni kubwa huwezi kumfurahisha kila mtu

.... usipopigwa huku, utapigwa kule!
Ahsante sana.
 
Ukabila wenu pelekeni IPP huko kwa wachaga. Pale Clouds hakuna ukabila hizo chuki zako tu... leta fact kuthibitisha upuuzi wako.

Una Uhakika Ukabila Hamna Au Unataka Ujulikane Kuwa Umekomenti Thread
 
Zamani nilikuwa naipenda sn hii radio station ila kuna mtangazaji mmoja alianza kuingiza siasa za chuki kwa kutumia hii radio tangia na bifu kwa baadhi ya wasanii hapo ndo nikaichukia.
 
Habari Wanabodi,

Nipo nasikiliza Clouds FM kipindi cha xxl segment ya "Album Review".Leo wana Review album(2003) ya Mwana Fa ya "Toleo Lijalo" yenye nyimbo kama Wanapendana,Alikufa kwa ngoma etc.Kwenye wimbo wa alikufa kwa ngoma ameimba na Anaconda(Lady Jay Dee) cha kushangaza kwenye huo wimbo wakati wana review ikifika sehemu ya chorus ya jide wana-mute inasikika beat tu.Kitendo cha clouds FM kama taasisi kampuni nzima kuweka beef na msanii mmoja inajidhihirisha Clouds FM ni radio ya wahuni tu.

Clouds FM sio mara ya kwanza kufanya upumbavu huo,nakumbuka kipindi cha nyuma Inspector Haroun alienda nao tofauti,kipindi hiko wimbo wake wa "Buzi" ndio ulikuwa una-hit basi jamaa kila ikifika pale anapochana Inspector sauti wanaondoa inasikika beat tu.

Kwenye ngoma ya Ben Pol "Jikubali" kuna moja ya mstari unaimbwa "Nampenda Lady jay Dee,namzimia Zitto" ile sehemu ya neno Lady Jay Dee wanaisugua(Scratch) na ilo neno halisikiki kabisa.

Kwenye kuadhimisha miaka 15 ya Dully sykes,kwenye promo walikuwa wanapiga nyimbo za nyuma za Dully Sykes,kuna ngoma inahitwa Bijou inavyoanza ina neno "Okay mbili sifuri sifuri nne,P-funky kinywele kimoja" ilipoanza hapo kwenye P-funky wakaikata kabisa wakaipeleka mbele.

Kwa Mchezo huo wa kitoto unaofanywa na Clouds Media inaishushia hadhi sana hiyo kampuni,kitendo cha kampuni hiyo kufanya mambo ya utoto ni wadhi redio inaendeshwa na makanjanja na sio watu wenye ueledi.Clouds FM ikubali pia matakwa ya wasanii,kama msanii akikataa kufanya deal kwa sababu anaona haimfaidishi yeye ni haki yake kukataa na si kigezo cha kutopiga nyimbo zake.

Kuna watu watasema kwamba redio zipo zaidi ya 60 na TV zaidi ya 20 kwanini wasanii wailalamikie Clouds tu? Hapa tunacholalamika ni kufinya(mute) sauti yeyote iliyopo kwenye nyimbo alizoshirikishwa msanii walioenda nae tofauti.Kama wanapiga wimbo wa ben pol waachie wimbo kama ulivyo na si ku-mute majina ya watu waliotajwa wenye beef nao.


CLOUDS MEDIA ACHENI UTOTO.

Mkuu hivi hiyo radio mawingu unaiwaza ..tatizo nadhani unalifahamu kuwa menejimenti yake ni watu wa aina gani..
 
Last edited by a moderator:
Back
Top Bottom