Cleopa D. Msuya: Nimemkubali

Cleopa D. Msuya: Nimemkubali

Majoja

JF-Expert Member
Joined
Jun 10, 2011
Posts
612
Reaction score
188
Katika kipindi cha 45 minutes cha ITV leo jioni , mtoa mada alikuwa CD Msuya, Waziri Mkuu na Makamu wa Kwanza wa Rais, enzi ya Mwalimu.
Kwa hakika amenikosha sana.
Bado ana data na current za kiuchumi-inaelekea nafuatilia sana current events
Hana papara wala jazba kujibu maswali, na alikuwa composed.
Lakini zaidi ya yote ameiasa nchi mambo makuu yafuatayp
  • kuwawezesha wakulima kutukia mbegu bora, utaalam bora wakilimo, na mechanization
  • ameishauri serikali kupunguza matumizi(kuachana na mashangingi)
  • kuongeza uzalishaji mali-katika kilimo n.k. ili kuongeza pato la taifa nahatimaye kupunguza kuporiomoka kwa shilingi yetu
Kwa jinsi alivyokuwa akijieleza kwa ufasaha, tofauti kubwa imeonekana , ukilinganisha na "Mawaziri vijana" wetu waliopo sasa.
Walioona tupeni maoni, good or bad.
 
niliiona kwa vipande lkn mzee anaonekana yuko vizuri sana na hazina ya ufahamu na hekima kama akina JK wakipenda kumtumia! Natamani pia ningeona mahojiano kama hayo yakifanywa na mawaziri wakuu wastaafu John Samwel Malecela na Edo Lowassa,lakini kwa kifupi Mzee CD Msuya yuko vizuri sana.
 
Nakuunga mkono kwenye wazo hili ila naona umemsahau SAS.
 
@Kinyamana E.Lowasa siyo waziri mkuu mstaafu!, tuendelee....
 
Tatizo ni kwamba tofauti na ilivyo kuwa kwa Nyerere hawa viongozi wetu wastaafu wengi wana ushawishi kidogo mno kama wanao kabisa. Sidhani hata kama wanafuatwa kwa ushauri na kama wanafuatwa kutoa ushauri sina ushahidi wa ushauri wao kufanyiwa kazi. Wazee wetu hawa wamekua vyombo vya public relations kwa kualikwa tu kwenye hafla mbali mbali.

Mimi ninge washauri hawa wazee pamoja na kujitokeza kwa mahojiano kama hivi waandike vitabu vingi kuhusu maisha yao na utumishi wao.
 
Alikuwa na mapungufu yake,lakini nimekuja kuona yalikuwa ni mapungufu ya kibindamu tu,japo kwa muda ule wa Mwalimu vilikuwa na vigezo vikubwa japo yeye hakupata kutamkiwa HAFAI,na wala HAKUJAPATA kusikika fununu [Rumous] kuwa MWALIMU hamtaki,nafikli halijikita sana Serikalini as a STATESMAN than being a POLITICIAN.

Ni moja ya watu kwa uzoefu wake nilitoa thread kama kuna watu muhimu sana sasa ningeambiwa wamshauri Kikwete as a panel ya kumshauri Jakaya Kikwete,hasa katika kipindi cha SINTOFAHAMU nyingi katika historia ya Taifa hili huyu nae ni kichwa kizuri ukizingatia uvumilivu na kutokuwa na papala na ukinganganizi usio na busara.
 
Msuya was a technocrat who became a politician by accident. I have interviewed him several times and he knows his stuff. Kikwete is not the kind of leader who will search for advice from someone who was bigger before him. He just does not have that in his personality.
 
Msuya kiongozi mzuri na wengine wote. Sioni kwa nini anaingizwa Kikwete humu; kwanza Msuya hata afanye nini hamfikii Kikwete, kwa sababu kikwete Ni RAIS, na akimaliza anakuwa RAIS MSTAAFU.

Kumkashifu kikwete ni kuwakashifu waliompigia kura.

Tusiende huko kwa sasa. tubaki na CD MSUYA, Amekubaliwa.

Mie pia nimemkubali; kapeleka umeme mwanga, Bunda kuna nini?
 
Utumbo mwingine bwana!!
 
Alikuwa anaogopaogopa kukosoa moja kwa moja, sijajua kwanini!
Wanajifanya wanabusara hadi mambo yanaharibika 1kwa1!
Mtangazaji nae alikuwa mbwiga tu anashindwa kumuuliza maswali vizuri, sijui kasoma wapi yule!? Ya msingi ya kuuliza yalikuwamengi sio kumwacha msuya akieleze kirahisi vile!
 
leo anazungumzia kuwawezesha wakulima kutumia mbegu bora, kipindi kile alisema kila mtu ataubeba mzigo wake mwenyewe........
 
Katika kipindi cha 45 minutes cha ITV leo jioni , mtoa mada alikuwa CD Msuya, Waziri Mkuu na Makamu wa Kwanza wa Rais, enzi ya Mwalimu.
Kwa hakika amenikosha sana.
Bado ana data na current za kiuchumi-inaelekea nafuatilia sana current events
Hana papara wala jazba kujibu maswali, na alikuwa composed.
Lakini zaidi ya yote ameiasa nchi mambo makuu yafuatayp
  • kuwawezesha wakulima kutukia mbegu bora, utaalam bora wakilimo, na mechanization
  • ameishauri serikali kupunguza matumizi(kuachana na mashangingi)
  • kuongeza uzalishaji mali-katika kilimo n.k. ili kuongeza pato la taifa nahatimaye kupunguza kuporiomoka kwa shilingi yetu
Kwa jinsi alivyokuwa akijieleza kwa ufasaha, tofauti kubwa imeonekana , ukilinganisha na "Mawaziri vijana" wetu waliopo sasa.
Walioona tupeni maoni, good or bad.

Hivi wakati yeye yuko kwenye system kwa nini hakufanya hayo anayoyasema? Hivi pia ilikufurahisha kipindi kile aliposema kila mtu atabeba msalaba/ mzigo wake mwenyewe?
 
Msuya was a technocrat who became a politician by accident. I have interviewed him several times and he knows his stuff.
Lazima tumpe respect Mzee CD, kama alivyokuwa akifahamika,kwa kuwa anajua yanayoendelea nchini pamoja na kwamba hakukulia kwenye siasa, bali katika utendaji serikalini(technocrat).
Data alizotoa , na ziko kwenye finger tips, msikilizaji unapata picha ya huyu mzee kuwa he knows his stuff.
Inasikitisha kuwa watu kama hawa hawana forum ya kuishauri serikali, kwa kulinganisha na uzoefu wao.
 
Unamkumbali kivipi? Wakati wa utawala wake kafanya nini cha kukumbukwa?
Ni kweli kabisa na hili ndio la kuliangalia, kama ni maneno matamu wengi tu leo hii tunaweza kuwahoji wakatupa hayo maneno matamu, swali la msingi linabaki pale pale watanzania tulifaidika na nini wakati wa wake, what legacy did he leave for us.........!
 
Former minister Msuya namkubali kwa jinsi alivyo hojiwa na kujieleza kwa umahiri ila yule aliyekuwa akimhoji aliogopa kumuuliza maswali magumu.
Kumbe pia ni chairman wa bodi TBL!
 
niliiona kwa vipande lkn mzee anaonekana yuko vizuri sana na hazina ya ufahamu na hekima kama akina JK wakipenda kumtumia! Natamani pia ningeona mahojiano kama hayo yakifanywa na mawaziri wakuu wastaafu John Samwel Malecela na Edo Lowassa,lakini kwa kifupi Mzee CD Msuya yuko vizuri sana.

Marekebisho kidogo tu Kinyamana. Edo Lowassa hakustaafu bali alijiuzulu kwa kashfa ya ufisadi. Labda ungemwita waziri mkuu MJIUZULU.
 
Kwa jinsi nilivyomsikiliza jana, anafaa kabisa kurudia nafasi ya uwaziri mkuu, lau kama ingekuwa i nawezekana!
Wakuu, nilimsikia mtangazaji akimtaja pia kwa cheo cha Makamu wa Rais...je alikamata nafasi hiyo kwa muda gani?
 
Inawezekana ameongea vizuri ila binafsi sijaona hayo mahojiano ila kiukweli huyu jamaa ukiangalia kwa umakini yeye ni kati ya vyanzo vikuu vya mmomonyoko wa maadili ya kiuongozi na ufisadi. Tatizo watanzania ni wepesi sana wa kusahau. Huyu jamaa alivyokuwa kiongozi alipeleka umeme huko milimani kwao ambako kwa hali ya kawaida hakufikiki kabisa kwa gharama kubwa za serikali, huu ulikuwa ubinafsi mkubwa na chimbuko la ufisadi tunaouona sasa.

Sielewi kwanini mnamsifia kwa anayoyaongea badala ya kuweka data alivyokuwa na cheo kikubwa kabisa serikalini alifanya nini ? Hata huyu JK mnamponda leo baada ya miaka 10 mtasifia kweli na kumuona ni kiongozi mwenye busara na jasiri. Watanzania tusiwe wepesi wa kusahau.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom