Kwa jinsi nilivyomsikiliza jana, anafaa kabisa kurudia nafasi ya uwaziri mkuu, lau kama ingekuwa i nawezekana!
Wakuu, nilimsikia mtangazaji akimtaja pia kwa cheo cha Makamu wa Rais...je alikamata nafasi hiyo kwa muda gani?
No PJ, hafai hata kidogo. Kujibu maswali siyo tija. Tija ni uzalendo na kufanya mambo yanayookoa maisha ya watanzania hasa wakati huu mgumu tulio nao. Hawa wazee wetu mnaowapa sifa kuwa wanajua kujibu maswali wanafanya nini mda wote huo mpaka nchi ididimie kiuchumi hivi. Wameshindwa hata kupaza sauti pale mambo yanapoenda mrama. Msuya ni muoga kama pinda. Angalia jana wakati anajieleza alishindwa kusema ukweli kuwa serikali imeshindwa akabaki kujingatangata. Musya, Malecela, Sumaye & Lowasa ni mizigo ya moto.Bora hata Warioba na SAS kidogo wanaichallenge serikali mambo yanapoenda mrama.