yupo na waziri mkuu mwingine mwenye busara nawe umemsahau JSW.Nakuunga mkono kwenye wazo hili ila naona umemsahau SAS.
yupo na waziri mkuu mwingine mwenye busara nawe umemsahau JSW.Nakuunga mkono kwenye wazo hili ila naona umemsahau SAS.
Mimi personally nimefanya nae kazi ni mchapa kazi mzuri saaaaaaaana.Kwa jinsi nilivyomsikiliza jana, anafaa kabisa kurudia nafasi ya uwaziri mkuu, lau kama ingekuwa i nawezekana!
Wakuu, nilimsikia mtangazaji akimtaja pia kwa cheo cha Makamu wa Rais...je alikamata nafasi hiyo kwa muda gani?
yupo na waziri mkuu mwingine mwenye busara nawe umemsahau JSW.
Mnyonge mnyongeni lakini hakh ake mpeni.
hakuna mtu mahiri na mwenye uwezo mkubwa miongoni mwa mawaziri wakuu wooote huko Tanzania zaidi ya ahali yangu SALIM Ahmed SALIM.
Hata JK Nyerere alilijua hilo
Its unfair ndugu yangu.CD Msuya didn't abide by rule of the game when he was a player, he's now 'seeing' others not abiding by the rule of the same game while playing.
Badala ya kukaa dak 45 ITV angepeleka ushauri wake huo kwenye vikao vya chama chake tawala. Anajua hatosikilizwa!
Hivyo tuliyosikia jana kayasema ili tumwone yy si kati ya waharibifu. Kwani ni lini Tanzania tuliwahi ku export kingi kuliko tunach import?
Who knows how rich is Msuya anyway? Mwenye kujua naomba anijuze.
niliiona kwa vipande lkn mzee anaonekana yuko vizuri sana na hazina ya ufahamu na hekima kama akina JK wakipenda kumtumia! Natamani pia ningeona mahojiano kama hayo yakifanywa na mawaziri wakuu wastaafu John Samwel Malecela na Edo Lowassa,lakini kwa kifupi Mzee CD Msuya yuko vizuri sana.
tatizo kubwa sidhani kama ni hao viongozi wastaafu perse. Nadhani wamechoka kudharauliwa na viongozi waliopo madarakani. kama ulivyoonyesha, viongozi wetu wa sasa wamekuwa wajuaji kiasi kwamba hawapati shida kuomba ushauri kutoka kwa vichwa hivi vilivyotangulia, hii ni mbaya sana hasa ukizingatia kuwa nchi inakabiliwa na matatizo mengi sana na kuna watu wenye uzoefu wa kutosha wa jinsi ya kukabiliana na matatizo hayo.Tatizo ni kwamba tofauti na ilivyo kuwa kwa Nyerere hawa viongozi wetu wastaafu wengi wana ushawishi kidogo mno kama wanao kabisa. Sidhani hata kama wanafuatwa kwa ushauri na kama wanafuatwa kutoa ushauri sina ushahidi wa ushauri wao kufanyiwa kazi. Wazee wetu hawa wamekua vyombo vya public relations kwa kualikwa tu kwenye hafla mbali mbali.
Mimi ninge washauri hawa wazee pamoja na kujitokeza kwa mahojiano kama hivi waandike vitabu vingi kuhusu maisha yao na utumishi wao.
Ndugu yetui, matatizo mengi ndo yaanzia hapo - URAIS.Msuya kiongozi mzuri na wengine wote. Sioni kwa nini anaingizwa Kikwete humu; kwanza Msuya hata afanye nini hamfikii Kikwete, kwa sababu kikwete Ni RAIS, na akimaliza anakuwa RAIS MSTAAFU.
Kumkashifu kikwete ni kuwakashifu waliompigia kura.
Tusiende huko kwa sasa. tubaki na CD MSUYA, Amekubaliwa.
Mie pia nimemkubali; kapeleka umeme mwanga, Bunda kuna nini?
niliiona kwa vipande lkn mzee anaonekana yuko vizuri sana na hazina ya ufahamu na hekima kama akina JK wakipenda kumtumia! Natamani pia ningeona mahojiano kama hayo yakifanywa na mawaziri wakuu wastaafu John Samwel Malecela na Edo Lowassa,lakini kwa kifupi Mzee CD Msuya yuko vizuri sana.
Mwalimu aliyekuwa Rais kwa zaidi ya miaka 20 nchi hii aliiacha wilaya yake ya Musoma(V) haina maji, barabara ya lami wala umeme.Niliona mahojiano, mzee alijibu vizuri na kwa umakini sana. Madai haya mengine eti alipeleka umeme Mwanga,kwani siyo Tanzania? Ama hawakustahili kupata umeme? Tuache hizo watanzania wenzangu!
kwa hiyo kwa mtazamo wako umeme ni kwa ajili ya wanaoishi kwenye maeneo tambarare tuu eeh? wa milimani hawastahili si ndio!!!
Tatizo watanzania ni wepesi sana wa kusahau. Huyu jamaa alivyokuwa kiongozi alipeleka umeme huko milimani kwao ambako kwa hali ya kawaida hakufikiki kabisa kwa gharama kubwa za serikali!!!!!!!!!!!!????????????
Kwani huko milimani kwao si kuna watanzania wanaishi pia au wao hawastahili kupelekewa umeme, inamaana ulitaka hizo gharama kubwa za serikali zitumike kwenye mashangingi(V8) na posho za wabunge wa viti maalum au sio!!!
Alikuwa anaogopaogopa kukosoa moja kwa moja, sijajua kwanini!
Wanajifanya wanabusara hadi mambo yanaharibika 1kwa1!
Mtangazaji nae alikuwa mbwiga tu anashindwa kumuuliza maswali vizuri, sijui kasoma wapi yule!? Ya msingi ya kuuliza yalikuwamengi sio kumwacha msuya akieleze kirahisi vile!
Kama wewe ni mpare unakila sababu ya kumsifia huyu jamaa, maana wapare walimchagua kuwa mbunge wa maisha wa jimbo la mwanga mpaka alivyoamua kustaafu mwenyewe. Vinginevyo kwa makabila mengine na kwa taifa kwa ujumla, jamaa hana la maana lolote zaidi ya ubinafsi na ukabila uliokithiri enzi za uongozi wake. Kile kirusi cha ubinafsi alichokuwa nacho na upendeleo wa wazi kwa watu wa kabila lake ndio kimezaa sasa na kuleta ufisadi uliokithiri ndani ya nchi hii.