Omutwale
JF-Expert Member
- Feb 4, 2008
- 1,429
- 1,053
Kwenye Vichwa vya Habari za Magezetini kupitia radio asubuhi ya leo nimesikia vijana zaidi ya 600 wamemuomba Lowassa agombee Urais. Habari hii imenikumbusha mbinu aliyopata kuitumia Lowassa mwaka 1995 katika kujipendekeza ili aonekane anaungwa mkono na Wananchi wengi. Mwaka ule Lowassa kwa kutumia fedha na "watu" alioojaaliwa na mungu (siyo Mungu), alitoa kandarasi ya kuandikwa barua toka kila mkoa na kila wilaya zikipendekeza kwenye chama kwamba kimteuwe kuwa mgombea wa Urais! Barua ziliandikwa katika nafsi ya Wananchi zikitaka kuonyesha kwamba Lowassa anaungwa mkono na Wananchi na zilitumwa makao makuu ya ccm. Uzuri wakati ule Taifa lilikuwa bado linao Wazee makini wasiokubali upuuzi ufanyike kunajisi utakatifu wa Taasisi ya Urais bila kukemea. Badala ya kumsaidia Lowassa kuufikia Urais, hizi barua ziliongeza mashada kwenye kaburi la kuuzika urais wake kipindi kile. Na ndiyo chanzo cha sehemu ya chagizo la Mwalimu kuuliza "…..huko Ikulu kuna nini?"
Nimeona ni vema kuwakumbusha na kuwafahamisha watanzania hasa vijana wa leo ambao mfumo wa elimu umewadhulumu somo muhimu kama historia ya nchi na uzalendo, wajue kwamba michezo mingi anayoicheza Lowassa leo siyo mipya na ni out of date!
Huyo Lowassa ana nini la kujivunia mpaka aombwe??? Nawalaumu sana viongozi wa dini kwa kuwa isingekuwa wao kudharirisha madehebu yao kwa kumpa huyu Farisayo jukwaa kwenye madhabahu Takatifu, labda Lowassa angetafuta kuongoka kwanza kabla ya kuendeleza hizi sanaa. Na labda hawa wachache wanaohadaiwa na drama za Lowassa kutokana na ukaribu na Makanisa wasingepotea njia?!

Nakubaliana na weweNa hayo maneno watakuwa wameambiwa waseme, Lowasa huwa anajiandalia hadi mapokezi