Chuo Kikuu Dodoma (UDOM) Wataka Lowassa agombee urais 2015

R.B

JF-Expert Member
Joined
May 10, 2012
Posts
6,296
Reaction score
2,578
Wanafunzi zaidi ya 600 wanaosoma Chuo Kikuu Dodoma (UDOM) ambao walimaliza elimu yao ya Sekondari katika shule za Kata nchini, wamemuomba Mbunge wa Monduli,Edward Lowassa kugombea urais katika uchaguzi mkuu wa mwaka 2015.

Wawakilishi wa wanafunzi hao wapatao 40,juzi jioni walimtembelea kiongozi huyo nyumbani kwake maeneo ya Area C mjini hapa na kula naye chakula cha usiku, huku wakimueleza kuwa wapo tayari kumpigia debe, kumchangia fedha za kuchukua fomu pamoja na kuwashawishi vijana wenzao kwamba Lowassa ndiye kiongozi anayefaa kwa sasa.

Hafla hiyo pia illihudhuriwa na viongozi mbalimbali pamoja na wanafunzi hao.

Chanzo: Mwananchi
 
Papa LOWASA KIBOKO. YAANI YEYE KAANZA KAMPENI ZA UCHAGUZI MAPEMA, MIAKA 2 KABLA YA WAKATI.
 
Hayo ni mawazo yao kumuka siyo udom ni kikundi cha watu 600 wametimizs lengo la kutoa mawazo yao.
 
Kawaita mwenyewe huyoo. Jamaa bado anaota Urais! Nadhani anajisafishia njia ya kufilisika. Ameanza kampeni muda mrefu sana kwa kumwaga mapesa kanisani. Sasa amehamia vyuo vikuu! Pole Lowasa. Angalia vizuri maana na Wasira naye anautaka huohuo URAHISI (Urais)kwa tiketi ya chama "chetu".
 
Hiki Chuo Ni cha hovyo Sana, sijui kilianzishwa kwa ajili gani? Ccm wangeendeleza Tu Chuo Chao pale kivukoni badala ya kutumia pensheni zetu kujenga hiyo takataka.

Kikwete aliwatumia kama condom. Wamehamia kwa Laigwanan naye awatumie, hawa watoto waliberali nini?
 
ungefanya utafiti kwanza kabla ya kurusha matusi,mimi nipo hapa UDOM,Kimsingi hakuna yeyote aliyefanya ujinga wa namna hiyo..watu wako bize na mitihani na wengine tayari walishaondoka kwenda likizo,sasa unaporusha matusi kwa kitu ambacho sicho sahihi hututendei haki kabisa,binafsi nimeumia kurushiwa matusi kwa habari ya uongo...
 
kwa UDOM sishangai hata kidogo,mmesahau mwaka 2010 walichanga viboom vyao wakamchukulia form ba'mwanaasha????kwa kujikombakomba hao ndo wenyewe,hao hawana pesa walienda kufata msosi tu huko area C
 
ungefanya utafiti kwanza kabla ya kurusha matusi,mimi nipo hapa UDOM,Kimsingi hakuna yeyote aliyefanya ujinga wa namna hiyo..watu wako bize na mitihani na wengine tayari walishaondoka kwenda likizo,sasa unaporusha matusi kwa kitu ambacho sicho sahihi hututendei haki kabisa,binafsi nimeumia kurushiwa matusi kwa habari ya uongo...

labda 2010 hukuwepo UDOMA,ILA WENZENU WALITUMIWA VIZUUURI,NA MWAKA ULOFATA AKAWATWANGA MABOM
 
Wanaoichafua UDOM na kui link na CCM hamtutendei haki kabisa,kila chuo kina UVCCM cha ajabu hapa UDOM japokuwa UVCCM ni wachache sana na wanafanya kazi zao kwa kujificha wakiogopa kuzomewa na wanafunzi,lakini cha ajabu kila wakifanyacho wanafiki wanasema UDOM imefanya hiki...huu ni ujinga mkubwa,hata kumchangia kikwete form mwaka 2010 walifanya UVCCM baada ya kupewa pesa na mkuu wa mkoa wa wakati huo wakishirikiana na Katibu mkuu wa wakati huu mzee Makamba,lakini wenye chuki wakasema UDOM imemchangia kikwete! Binafsi habari hizi huwa nazikuta jamii forums tu,nadhani ifikie hatua uwongo huu ukome,,,mbona hamuandiki harakati za CHADEMA? mbona hamuandiki habari za BAVICHA UDOM kujenga ofisi zao? Mbona hamuandiki habari za wanafunzi wa CHADEMA ambao ni wengi zaidi chuon kufanya mikutano ya hadhara vijijini wakati wa weekend kuelimisha umma kuhusu mambo ya msingi? Ufikie wakati upotoshaji huu ukome,uongo na uzandiki dhidi ya UDOM ufikie mwisho,hamuwatendei haki wanafunzi na walimu ambao ni wana mageuzi....mleta mada omba radhi jukwaani,ni tabia mbaya kudanganya umma
 
ungefanya utafiti kwanza kabla ya kurusha matusi,mimi nipo hapa UDOM,Kimsingi hakuna yeyote aliyefanya ujinga wa namna hiyo..watu wako bize na mitihani na wengine tayari walishaondoka kwenda likizo,sasa unaporusha matusi kwa kitu ambacho sicho sahihi hututendei haki kabisa,binafsi nimeumia kurushiwa matusi kwa habari ya uongo...

Njaa mbaya. Inawezekana hao wanaokwenda likizo wamepita kuvuta mkwanja. Nashauri vijana hao waanzishe umoja wao, Ward Schools University Students Association (WASUSA) ili wamsaidie EL katika kufikia malengo yake.
 
Huku kukiwa na minongono juu ya Waziri mkuu wa zamani Lowassa kutajwa kugombea urais ktk uchahuzi mkuu ujao huku yeye binafsi akiwa hajatoa tamko, wanafunzi wa chuo kikuu cha Dodoma waliosoma shule za kata wamemtaka Waziri mkuu huyo wa zamani kuchukua fomu kugombea urais mwaka 2015. Hayo yalisemwa juzi ktk hafla iliyofanyika nyumbani kwa Lowassa Monduli ambapo wanafunzi hao walimtembelea.

Source: Gazeti la Nipashe.
 
Wanaoichafua UDOM na kui link na CCM hamtutendei haki kabisa,kila chuo kina UVCCM cha ajabu hapa UDOM japokuwa UVCCM ni wachache sana na wanafanya kazi zao kwa kujificha wakiogopa kuzomewa na wanafunzi,lakini cha ajabu kila wakifanyacho wanafiki wanasema UDOM imefanya hiki...huu ni ujinga mkubwa,hata kumchangia kikwete form mwaka 2010 walifanya UVCCM baada ya kupewa pesa na mkuu wa mkoa wa wakati huo wakishirikiana na Katibu mkuu wa wakati huu mzee Makamba,lakini wenye chuki wakasema UDOM imemchangia kikwete! Binafsi habari hizi huwa nazikuta jamii forums tu,nadhani ifikie hatua uwongo huu ukome,,,mbona hamuandiki harakati za CHADEMA? mbona hamuandiki habari za BAVICHA UDOM kujenga ofisi zao? Mbona hamuandiki habari za wanafunzi wa CHADEMA ambao ni wengi zaidi chuon kufanya mikutano ya hadhara vijijini wakati wa weekend kuelimisha umma kuhusu mambo ya msingi? Ufikie wakati upotoshaji huu ukome,uongo na uzandiki dhidi ya UDOM ufikie mwisho,hamuwatendei haki wanafunzi na walimu ambao ni wana mageuzi....mleta mada omba radhi jukwaani,ni tabia mbaya kudanganya umma

unachobisha awakwenda ???????????? au unabisha tu
 
...hao wanafunzi pamoja na kufika chuo kikuu bado hawajajitambua tu!?...kweli "NI RAISI SANA KUMTOA NYANI PORINI LAKINI NI-VIGUMU SANA KULITOA PORI KICHWANI MWA NYANI"...
 
Isomeke hivi vijana wa UVCCM udom wamtaka lowasa......
 
Nina mashaka na GPA watakazopata Wanafunzi hao.Wanaonekana wachumia tumbo waliopitiliza.

Si ajabu walitoa maneno hayo kwa matarajio ya kupiga mzinga. Yaani wahuni wajikusanye huko tu na njaa zao kali kali wajifanye wawakilishi wa wanafunzi wote? Ni nani aliwatuma? Hawana tofauti na wale walioenda kula mishikaki kule Monduli walipotoka huko wakawa waropokaji wakubwa

Vibaka wamekusanyanana na kupeana sapoti. Eti watasaidia kuchangisha hela?ha ha ha ha! ------
 
Back
Top Bottom