Hapa kwanza ningeomba tuache udini.
Nakupongeza sana mleta Mada,na umeandika vizuri saana tena saana,na umetoa mwanya wa watu kujenga hoja na kutetea,lakini ukweli unabakia kwamba bado hakuna hoja imeyotetea vizuri.Kila mmoja anarusha mpira na wengine wakiona chuo fulani cha Kikristo kimekufa baso wanaonyeshea mfano huko wakati sio lengo.
Lengo ni nia nzuri na njema,sasa kamaa chuo fulani cha kikristo kimekufa basi mleta mada licha kwamba ni mkristo ila kwa ubinaadam wake ameona atoe hadhari kwa sie waislam kwamba chuo chetu kinakufa ili kisije kufikia kama hivyo walivyovitolea mfano watu wengine,Naweza kusema Waliochangia kwa nia Njema Mungu awabariki.
Unajua sie Waislam tumekuwa tukilalamika muda mrefu saana suala la elim,na tulipoteleza tunapajua,unajua kuna Wanafiki ndani ya Uislam na kuna Waislam wenye kujitambua.Sasa kama chuo chenyewe kimoja tena cha kisasa kinatushinda,sasa tumlalamkie nani.Maana kwenye nyumba zetu za ibada tu vurugu kila siku.Watu hata BAKWATA wanakuambia hawaitambui na kusema BAKWATA ni Tawi la Kanisa,hivi hii akili kweli?
Narejea kusema,adui wa Muislam yumo ndani ya Uislam na sivinginevyo
Mfano mdogo tu,unakuta mtoto wakati anaenda madrasa anavaa nguo ile chafuuu,na kanzu chafuu tena mbayaa,ila huyohuyo mtoto akienda Shuleni basi unakuta smart kweli,kiatu safii,soksi,shati safii yaani amependeza kweli na pesa ya kula juu.Sasa geukia upande wa pili wa Madrsa,huwezi kuamini ndugu zangu wakristo,ni kwamba Madrassa nyingi za kiislam mchango au ada ya mwezi haizidi Elfu 5,mie wanangu anasoma madrassa kwa mwezi elfu tatu tu,lakini cha kushangaza hakna hata anaetoa,yaani waalim wa madrass wana struggle kweli,wengo omba omba,na hawawezi kumfukuza mtoto kwa ada ya madrasa,ila wakati huo huko Mtoto huyo analipa karibia milioni shule ya kawaida.
Sasa hapo mtapata picha kwamba haya mambo yana background yake,na muislam mwenye kujitambua hapati shida kujua vyanzo.Kuna unafiki mwingi sana ndani ya Dini yetu,lazim tuliseme hili.Shule ngapi zinatushinda kusimamia Vizuri ikiwemo Ubungo Islamic na nyinginezo.
Naomba uongozi wa Chuo na BAKWATA na taasisi husika lazima walishughulikie hili.Chuo kinauwezo wa kuomba Wataalam Nchi nyingi sana za Kiislam zenye maendeleo makubwa ya ELIM kama Iran nk na wakasaidia pale,ila kuna tatizo ndani kwa ndani kwa maslahi ya wachache.