Chuo Kikuu cha Dar es salaam, Ndaki ya Sayansi ya Jamii
Kitivo kikongwe cha chuo kikuu cha UDSM chajadili kwa pamoja na jamii nzima mkataba wa bandari
Mwenyekiti wa mjadala wa leo Dr. Ng'wanza Soko Kamata wa kitivo cha CoSS UDSM aliwakaribisha wote waliojumuika ukumbini na wale walioshiriki kwa njia ya Zoom mtandaoni.
Ndaki ya Sayansi ya Jamii UDSM pia hujikita katika kuchambua tafakuri zilizopo katika jamii na hili jambo la sakata la mkataba wa bandari linaloifikirisha jamii ya kiTanzania linaangaziwa kwa upana.
Video ndefu hapa juu inawakilisha tafakuri inayotuletea yote ya mjadala mpana na mkubwa uliowaleta washikadau wakiwemo wanazuoni waalimu wahadhiri waandamizi 9 wa chuo kikuu wakiwemo Dr. Ng'wanza Soko Kamata, Dr. Richard Bruno Mbunda, Prof. Issa Shivji, wanafunzi wa UDSM na wananchi wanajamii kupitia mtandao
Uchambuzi wa Profesa Shivji mazito yabainika mkataba wa bandari
Chini ya ndaki ya sayansi ya jamii CoSS College of Social Sciences leo wahadhari na wanafunzi wajadili kwa kina mkataba wa bandari na unaleta madhara gani kwa taifa.
Mchokoza mada Dr. Richard Bruno Mbunda pamoja na wahadhiri na wanafunzi wa chuo kikuu cha UDSM na mgeni mwalika profesa Issa Shivji wamejadili kwa kina mada ya mkataba wa bandari ambao imekuwa habari kuu isiyozimika katika vijiwe na mitandao ya kijamii.
Dr. Richard Mbunda anasema kuwa pamoja na Ofisi ya Katibu wa Bunge kuwa ni mshauri mkuu wa bunge lakini pia secretariat ya bunge kuonesha kwa mapendekezo mapungufu ya mkataba lakini kamati ya bunge husika, waziri na bunge zima liliamua kutoyatilia maanani maangalizo muhimu ya secretariat ya Bunge kuhusu mkataba huu usioupa haki ya sovereignty Tanzania
Ila leo ndaki hiyo ya chuo kikuu cha Dar es Salaam imeamua kurudia enzi ambazo chuo kikuu hicho kongwe kilikuwa hakiko nyuma kuandaa mihadhara ya kuchambua mambo mazito yanayoendelea katika jamii .
Profesa Issa Shivji ameamua kujikita zaidi katika mguso huo wa mkataba una maana gani hasa pia unatuletea nini mezani na kumuachi Dr. Richard Bruno Mbunda akijikita kisheria zaidi una mazuri na mapungufu gani.
Profesa Issa Shivji anasema mkataba huu ni treaty yaani mkataba baina ya nchi na nchi na nchi hiyo ni Tanzania na nchi nyingine ambayo ni ngumu kusema kama ni nchi au la.
Ila kuna jambo ambalo limejitokeza katika hilo maana katika treaty lazima kuwepo nipe na nikupe baina ya wawili katika mkataba. Hilo halipo bali haki zote amepewa Dubai huku wajibu wote amepewa Tanzania bila haki. Yaani mkataba umekuwa uwekezaji ingawa unaitwa ni mashirikiano.
Ila ushirikiano huo si wa kijumla bali ni wa bandari na mwekezaji ametajwa ni DP World siyo wawekezaji wa kijumla wa kuhesabika kwa namba makampuni au wafanyabiashara kutoka Dubai.
Jingine ni kuwa DP World inamilikiwa na serikali yaani ni state company. Maana yake kampuni ya serikali inaweza kuleta mgongano wa kidiplomasia tofauti kama ingekuwa kampuni ya binafsi kwani kampuni binafsi huwa haiwezi kuleta mgogoro wa kidiplomasia maana mambo yote yangeishia mahakamani ila kwa kampuni inayomilikiwa na serikali ni tofauti.
Hii ina maana 80% matayarisho shughuli na mapendekezo ya mradi (early project activities) huu mradi wa serikali ya Dubai kupitia DP World na serikali ya Tanzania yalikuwa yameshaandaliwa hata kabla ya mkataba uliopitishwa na azimio la Bunge la Jamhuri ya Muungano tarehe 10 June 2023 mjini Dodoma.
Hii ina maana mikono ilishafungwa na mkataba hata kabla ya IGA ya Dodoma na hiyo mikataba mingine midogo midogo imeshamalizwa kabla ya HGA . Host Government Government Agreements inayotajwa kuwa itafuatia.
Mfano suala la ardhi kwa sheria za Tanzania rais wa jamhuri ya Muungano wa Tanzania katiba yetu inasema ni mdhamini / mwangalizi wa ardhi yote ili ndani ya mipaka ya nchi na kuwa mtanzania au mwekezaji akipewa umiliki wa miaka 33 au 66 au 99 Rais ana mamlaka ya kuichukua akiona inafaa kutumika kwa manufaa mapana ya jamii na nchi.
Lakini kwa mkataba wetu na DP World, hili la rais wa Tanzania ni mdhamini / mmiliki wa ardhi yote ya Tanzania amevuliwa mamlaka hayo na ameshanganganywa mamlaka hayo na mkataba huu wa aina yake wa bandari. Maana mkataba na Dubai unasema kuhusu ardhi upo bayana neno la kiingereza incumbrace (in property law) kuwa hakutakuwa na kikwazo chochote ...
Bandari ya Dar es Salaam haijathaminisha ili ijulikane serikali yetu imeshawekeza trilioni ngapi kabla DP World haijaingia mkataba. Hakuna mpango maalum wa kuelezea mapato yatagawanywa vipi baina ya Tanzania na DP World kutokana na mradi huu wa bandari.
Ajira za upande wetu zitakuwa za kada ya makuli ndiyo wataajiriwa pengine na wachache kwenye HR yaani utumishi lakini wataalamu wote watatoka nje. Kuhusu kazi za ndogo ndogo za kandarasi ku supply vitu kwa DP World itatolewa kuna masharti, vigezo na kanuni kibao ambazo wafanyabiashara wa Tanzania watashindwa kutimiza mfano standards, competitive market prices za kimataifa n.k Nani atakuwa mdhibiti kuhakikisha tenda ndogo kampuni za kitanzania zitawe kushinda kuuzia DP World vifaa, vipuri n.k mhadhara huu wa ndaki ya sayansi ya jamii CoSS unakuna vichwa wakiangalia mbele.
Muhadhara huu wa CoSS ndaki ya Sayansi ya Jamii ya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam unaenda mbali na kuona nini kifanyike maana mkataba huu ni mgumu kunufaisha taifa hata ukifanyiwa marekebisho kupitia hatua za HGA host government agreement.
Muhadhara wa huu CoSS pia uliunganisha jamii nje ya chuo wachangiaji mada na maswali kupitia mtandaoni live na kuona yafuatayo yafanyike .
Bunge liamue kukataa azimio lake lenyewe la tarehe 10 June 2023 kuhusu mkataba huu. Bunge lina mamlaka hayo na haliwezi kuhojiwa na DP World wala jumuiya ya kimataifa. Maana Bunge linachanguliwa na wananchi wa Tanzania na pale wananchi wanapokataa mkataba huu baada ya kusikilizwa, wabunge ni wajibu wao kuandaa azimio lingine linalozingatia maoni ya wananchi kuwa wameukataa mkataba / makubaliano haya.
Muhadhara unafahamishwa kuwa nchi kadhaa zimeweza kuvunja mikataba ya aina hii na haikuonekana ni ajabu na kutolea mifano Ecuador ilifuta mikataba 26, nchi ya Bolivia ikaondoa mikataba 17 huku South Africa nayo mikataba 20 iliondolewa wakati India nayo ilifuata mikataba 58.
Hivyo serikali na kikao cha bunge lake baada ya Azimio la Bunge kupitisha mkataba wa bandari kutoa kauli ya unyenyekevu ipo sikivu na kuahidi kusikiliza kelele pia maoni ya wananchi wake pamoja na maoni ya washikadau kama wataalamu wa sheria, wahadhiri wa vyuo vikuu, vyama vya siasa n.k
Mhadhara wa watu-huru kupitia tafakuri ya kina unafikiri ni wakati sahihi wa Bunge kuitisha kikao cha dharura kukaa na kufuta azimio lake la tarehe 10 Juni 2023 na bunge kuishauri serikali kuanza mchakato mpya kumpata mwekezaji mwenye masharti ya manufaa hata kama katika mchakato huo mpya wa wazi shindani atakuwemo DP World na wengine ambao watashindanishwa ...