Burkinabe
JF-Expert Member
- Feb 12, 2023
- 1,892
- 3,196
Habari wana JF,
Kwa wale wazee wenzangu, watakubaliana na mimi kwamba wanachuo wa siku hizi wa Chuo Kikuu Cha Dar es Salaam wamepoa sana na wengi wao hawajiamini kulinganisha na wale wa miaka ya 2005 kurudi nyuma!
Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM) al-maarufu kama Mlimani, ilikuwa ni kitovu na chachu ya Mabadiliko kwa Tanzania na hata Afrika kwa ujumla.
Kwa wale ambao tumepita pale, kuna sehemu inaitwa "Nyerere Square". Hii ndiyo ground ambayo tulizoea kushuhudia umahili wa wanachuo katika kujenga hoja ambazo baadaye zilileta mabadiliko makubwa kabisa hapa nchini.
Inasemekana hata mabadiliko kwa nchi nyingi za kusini mwa jangwa la Sahara, yaliletwa na viongozi wao baada ya uzoefu ambao waliupata hapa Mlimani specifically "NYERERE SQUARE". Mfano John Garang wa Sudan (leo South Sudan), Yowel Kaguta Museven wa Uganda, Mwai Kibaki wa Kenya, n.k.
Wanachuo wa Mlimani ya Kipindi hicho, wasingekubali kabisa mijadala mikubwa ya Kitaifa kupita hivi hivi bila kuweka neno!
Anyway, naomba kwa leo niishie tu hapo kwamba wanachuo wa UDSM wa siku hizi wako very "DILUTE".
Hivyo, ninawaasa wahadhili na Maprofesa wa Mlimani kusaidia kurudisha HADHI ya UDSM kwa kuwajengea vijana ujasiri wa kujenga hoja kwa maslahi mapana ya Taifa lao.
Maana Taifa haliwezi kujengwa na vijana waoga waoga, wasio na uwezo wa kujenga hoja na ile type ya Yes Sir/Madam!
Amkeni,
Nawatakia tafakari njema.