Ukitoka kwenye utamaduni zinaoamini uchawi uchawi, unakuwa na kasumba ya kufikiri lolote linawezekana.
Na Africa tuna kasumba hizi za kupenda nguvu za kichawi, hususan kwa sababu tumechelewa sana kupata maendeleo ya kisayansi, lakini kiukweli dunia nzima ndiyo kwanza tunaamka kutoka dunia ya uchawi na kuanza dunia ya sayansi proper. Proper science is barely 500 years old. Kwa hiyo hili tatizo pengine lipo sana kwetu, lakini lipo dunia nzima.
Kufanya suala liwe gumu zaidi, kufikiria hivyo (inavyoonekana kichawichawi) ni sehemu ya scientific development, ni sehemu ya "Hegelian dialectic" za kisayansi za thesis, antithesis, synthesis.
Lakini swali muhimu ni, je, tunajuaje hapa tuna aspirations za kufanya vitu kisayansi, vitu vitakavyowezekana, na hapa ni kufikiri kichawichawi tu haya mambo hayawezekani kwa sababu yanapingana na kanuni za msingi kabisa za sayansi?
Yani kufikiri na kutenganisha kwamba kuna mambo yanawezekana ila hatujayajua vizuri tu kuweza kuyafanya, na kuna mambo hayawezekani kabisa kwa sababu kanuni za msingi za ulimwengu haziyakubali, inakuwa kazi ngumu sana.
Utamaduni wa kuamini uchawi unatufanya tusiweze kutenganisha sayansi na fantasy za kichawi.
Na hili jambo kulielewa na kulikubali ni vigumu sana. Watu tuna ubishi fulani hivi wa "anything is possible" katika dunia ambaho some things are impossible.
Ndiyo maana muandishi wa Science Fiction Arthur C. Clarke alisema "Any sufficiently advanced technology is indistinguishable from magic".
Sasa hawa wanaosema hili litawezekana wanajuaje kuwa wanasema hivyo kwa kukaa katika misingi ya kisayansi na kuongelea vitu ambavyo vitawezekana kweli, na hawasemi kwa misingi ya fantasy za kichawi mambo ambayo yanapingana na kanuni za msingi za kisayansi ambayo hayatawezekana kabisa?
If you are pursuing a theory or technology, how do you know it is possible at all, and it is not a dead end of impossible farcical fantasies?