Chozi la Kabwe kwa Makonda limekoma

Chozi la Kabwe kwa Makonda limekoma

Red=Kuendeleza mema tu (siyo yote)
Blue= hiyo haitoshi kuwa ushahidi kuwa hakuwa mlaji.

Ukiingia ktk utumishi wa umma kwa sasa uwe tayari kuwajibika ikiwa ni pamoja na kuridhika na hatua ya kusimamishwa kazi kupisha uchunguzi, unakuwa umeisaidia serikali, tunasema Tanzania kwanza mtu baadae.
Unapofanya kazi na wanasiasa hasa kazi zenye maslahi makubwa km ukurugenzi there's a price to pay, tuwe wavumilivu jamani pia tufqnyeni kazi za watu tuache umimi.
Sor far hakuna aliye na uhakika iwapo Kabwe alikuwa mlaji au la, ingawa malalamiko yalikuwapo, ndio hivyo amefariki uchunguzi ukiendelea.
Tulisema lazima
viongozi wetu waoneshe wanachukia rushwa mbona wakionesha tunawageuka tena?
Nijibu pia kwa hoja sheria za kazi za kuajiri kufukuza na kusimamisha zinasemaje kwenye utumishi wa umma
 
Hafai kabisa huko Luchelele, kuacha matatizo kwa jamii. Ni Kosa la kujifunza kuwa na wakurgenzi wageni wasio na utu.
Yeye ni Kumiliki mashamba tu na Beach zetu.
Mlimwajibisha kufuata kanuni na sheria?
 
PAMOJA na kuelezwa kuwa umauti hauna adui, lakini kwa msiba huu wa Wilson Mbonea Kabwe umekuwa tofauti. Una maadui, tena maadui wasiofahamu maisha yake, utendaji na uadilifu wake katika kazi, anaandika Henerico Mayanja.

Hawa ni maadui waliojipambanua kuwa liwalo na liwe, lazima Kabwe aingie katika kitabu cha kumbukumbu za aibu, tena aibu ya tuhuma za wizi na ufisadi, licha ya kuwa na rekodi iliyotukuka katika maeneo mengi aliyofanya kazi.

Walioamua kuwa maadui wake, wanaongozwa na Paul Makonda, mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam, anayedaiwa kujiapiza kumng’oa Kabwe katika nafasi yake ya ukurugenzi wa jiji alilokuwa akiliongoza, akimwakilisha Rais John Pombe Magufuli.

Uadui wa Makonda kwa Kabwe unaelezwa na watu waliokuwa karibu na Kabwe na hata yeye mwenyewe kabla ya kukutwa na umauti Mei 20, mwaka huu.

Ieleweke kuwa utendaji uliotukuka wa Kabwe ndiyo umemfanya kuwa mkurugenzi wa majiji matatu kwa nyakati tofauti; Mbeya, Mwanza na baadaye Dar es Salaam, akiteuliwa na marais wawili; Benjamin Mkapa na Jakaya Kikwete kuongoza na kusimamia kasma, fedha na utendaji wa majiji hayo kwa mafanikio makubwa.

Watu wanajuliza, endapo Kabwe angekuwa mwizi na fisadi ni namna gani angeweza kuaminiwa na marais wote hawa, tena akiwamo Mkapa ambaye umakini wake unasifika, siyo Tanzania tu, bali dunia yote.

Ukiacha sifa hizo za utendaji kutoka kwa marais hao, hata katika salamu za serikali wakati wa msiba wa Kabwe nyumbani kwake, Msasani, Dar es Salaam, George Simbachawene, waziri wa nchi, ofisi ya rais, tawala za mikoa na serikali za mitaa (Tamisemi), alisema Tanzania imepoteza kiongozi mahiri na mwaminifu aliyeitumikia nafasi yake kwa umakini na weledi mkubwa kwa manufaa ya wananchi.

Kauli ya Simbachawene inaaminika na wengi waliokuwepo kwenye msiba huo kuwa inatoka kinywani kwake kwa dhati kabisa kwani alimfahamu Kabwe kwa muda mrefu na haina chembe ya unafiki uliozoeleka misibani.

Waziri huyo alisema- “kwa ngazi aliyokuwa amefikia Kabwe ni sawa na katibu mkuu wa wizara, leo hii ukiizungumzia Mwanza inayosifika kwa usafi na miundombinu, huwezi kuacha kumtaja Kabwe..

Alifanya mengi sana kwa ajili ya maendeleo ya Mwanza na maeneo mengine alikokuwa akifanya kazi za wananchi kwa niaba ya serikali, hakika serikali imepoteza mtumishi hodari na sisi tutaenzi mchango wake kwa kuendeleza mema aliyofanya Kabwe,” alisema Simbachawene.

Kauli hiyo ya Simbachawene na uteuzi wa kuaminiwa wa Mkapa na Kikwete ni ushahidi mwingine wa kutosha kuwa Kabwe hakuwa “mlaji,” alijitoa kufanya kazi za umma kwa uaminifu mkubwa na kupata fursa ya kutoa mchango wake katika kuendeleza majiji ya Mwanza, Mbeya na Dar es Salaam.

Lakini pamoja na mchango mkubwa wa Kabwe, anajitokeza Makonda, kijana mdogo katika utendaji wa kazi za serikali na utumishi wa umma akiwaeleza Watanzania kuwa Kabwe ni mtuhumiwa wa ufisadi.

Bila aibu, mbele ya wakazi wa Dar es Salaam na Watanzania kwa ujumla wao, Makonda wakati wa ufunguzi wa Daraja la Mwalimu Nyerere, linalounganisha Dar es Salaam na Kigamboni, alimchongea Kabwe na kumuonesha kuwa ni mtu asiyefaa.

Kwa staili ya Rais John Magufuli, bila kufanya utafiti alikubaliana na Makonda na kuamua kumsimamisha kazi Kabwe kwa tuhuma za kumdhalilisha, tena mbele ya umma.

Makonda alimchongea Kabwe Aprili 19 na baada ya siku 30, Kabwe mwenye miaka 60 alifariki dunia kwa ugonjwa ambao, pamoja na maelezo tofauti kuhusu chanzo cha kifo chake, upo uwezekano kuchangiwa na msongo wa mawazo kwa kudhalilishwa na kijana mdogo aliyeshindwa kuitambua vyema historia yake ya utendaji, hata kumwaminisha Rais Magufuli uongo.

Katika kutetea utu wake, Kabwe alisononeka mno kwa uamuzi wa Rais Magufuli na uchonganishi wa Makonda kwa kiongozi wa nchi.

Kabwe alisema; “mimi sihusiki na mikataba inayosemwa na Makonda, huu ni uongo mtupu, Makonda ametoa taarifa za uongo kwa Rais Magufuli akiwa na lengo la kunichafua na kunionesha mimi ni mtu wa hovyo ninayeendekeza ufisadi, hakika nimesikitika mno na kuumizwa.”

Aliongeza kueleza; “tuhuma zinazoelekezwa kwangu ni za uongo na zimelenga kunichafua mbele ya rais, nasisitiza tena hakuna mkataba wowote ambao ofisi yangu iliingia kwa nia ya kupoteza mapato ya serikali.”

Kabwe akaendelea kulalamika kwa uchungu; “hiki kinachodaiwa kupotea na Makonda kimepotea kutoka wapi?… huu ni upotoshaji wa wazi, hizo Sh. 3 bilioni zilichukuliwa na nani.”

Hadi mauti yanamkuta, Kabwe ndiye mkurugenzi pekee hadi sasa aliyewahi kuongoza majiji matatu Tanzania kwa nyakati tofauti na amekuwa na uzoefu wa miaka 19 katika uongozi wa serikali za mitaa.

Mbali na uzoefu huo, Kabwe ni mwanasheria, akiwa wakili wa Mahakama Kuu ya Tanzania na pia mmoja ya wanabodi wa benki ya jamii Dar Es Salaam (DCB).

Wakati sifa zote hizo zikilazimishwa kufutwa na Makonda kwa kumchongea, na hatimaye kusimamishwa kazi na baadaye kukutwa na umauti, Makonda ameguswa, kusutwa na nafsi yake na kuukata mshipa wa aibu. Akajitokeza kwenda kuhani msiba.

Ni haki yake kwenda kuhani msiba wa Kabwe, lakini kwa jitihada zake binafsi kumchafua Kabwe kwa rais na mbele ya umma, imedhihirika kuwa mshipa wake wa aibu umekatika.

Kabwe amefariki dunia akilia. Akitoa chozi na sononeko la nafsi kwa namna alivyotendwa na kiongozi aliyeamua kumchongea tu kwa sababu anazojua yeye.

Sasa chozi la Wilson Mbonea Kabwe limekoma. Hatalia tena juu ya uso wa dunia, kwani limekatizwa na umauti. Alale salama.

Makala hii imeandikwa katika Gazeti la Mseto la tarehe 26 Mei mpaka tarehe 1 Juni mwaka huu katika ukurasa wa 5.
Mbona Makonda ni wa juzi? Ni CHADEMA ndiyo waliomtoboa Kabwe, Mbunge Highness Kiwia wa Mjini Mwanza alisnika madhambi yake yooooote.

Anza na Mbunge Kiwia, jiulize mbona hskuja msibani?

Kabla hatujasahau, ni CHADEMA haohao waliomlipua LOWASSA kwa miaka 10 wakimwita Fisadi kila mahali. Baadaye akawa rais wao.

Na Marehemu Kabwe sasa mnataka kumtumia kisiasa kama Lowassa?
 
Serikali hii itajaa vijana sababu wambea,wanafiki na wanajua kujipendekeza sana
Hili nalo neno

Kikubwa zaidi ni kwamba hawana base ya kuhoji vitu vingi kutokana na lack of experience... a very risky venture kwa kiasi fulani, but maybe its worth taking kwa jinsi nchi ilivyokua imeoza

Magufuli inabidi achunge sana wanaojipendekeza kwake, atapoteza watu wa maana kwa ajili ya tabia ya ajabu ya siku hizi ya kuchongeana
 
Huu ukawa sasa unatetea wezi toka Lowasa aingie huko
 
Undumi la kuwili unatuvuruga sana wabongo...
Hii nchi! Ni double standards kila uchao.Kwa tabia hizi tutaendelea kuwa maskini kwa karne nyingi.

Kabla.ya kufariki ilionekana ni sawa alivyosimamishwa ili uchunguzi ufanyike.Sasa mauti yamemkuta midomo ileile inagaeuka na kuleta sympathy zisizo na kichwa wala miguu.

Hatuwezi kuendelea kwa mienendo hii,tuziache mamlaka zitende wajibu.Pia suala la tuhuma ni variable moja na afya ya mtu ni ingine.

Binafsi sipati shida na muandishi wa hiyo habari kwakuwa namna alivyoiandika ina reflect uwezo wake wa kuunganisha matukio.
 
Mbona Makonda ni wa juzi? Ni CHADEMA ndiyo waliomtoboa Kabwe, Mbunge Highness Kiwia wa Mjini Mwanza alisnika madhambi yake yooooote.

Anza na Mbunge Kiwia, jiulize mbona hskuja msibani?

Kabla hatujasahau, ni CHADEMA haohao waliomlipua LOWASSA kwa miaka 10 wakimwita Fisadi kila mahali. Baadaye akawa rais wao.

Na Marehemu Kabwe sasa mnataka kumtumia kisiasa kama Lowassa?
Juzi kwenye daraja ilikua ni chadema?
 
Hii nchi! Ni double standards kila uchao.Kwa tabia hizi tutaendelea kuwa maskini kwa karne nyingi.

Kabla.ya kufariki ilionekana ni sawa alivyosimamishwa ili uchunguzi ufanyike.Sasa mauti yamemkuta midomo ileile inagaeuka na kuleta sympathy zisizo na kichwa wala miguu.

Hatuwezi kuendelea kwa mienendo hii,tuziache mamlaka zitende wajibu.Pia suala la tuhuma ni variable moja na afya ya mtu ni ingine.

Binafsi sipati shida na muandishi wa hiyo habari kwakuwa namna alivyoiandika ina reflect uwezo wake wa kuunganisha matukio.
Bila kusahau na ukweli utatuweka Huru
 
tatizo halikuwa uwaziri mkuu..tatizo lilikuwa ni richmond...lowasa alishiriki mkataba wa richmond 100%
Kulikuwa na Shida Kubwa ya Umeme, Lowassa akiwa kama Waziri mkuu aliwasukuma waharakishe Mkataba wa Kuleta Umeme wa Dharura, Lakini Waziri Mkuu hasaini Mkataba. Hata hivyo Mkataba ulivyoleta Matatizo Lowassa alitaka kuuvunja JK akamkataza akamwambia ni Upepo Uvumao. JK asingeweza Kupenda kuwa na Lowassa kwani Lowassa angemfunika. Na hakuna Rais anayependa awe second in Voice and popularity, Na sii Tanzania tu Hata marekani watu ni makini sana kuchagua, 1) mgombea mwenza, 2) Secretary of State. Kwa hisia zangu JK ukiachilia Richmond hakumtaka tena Lowassa kwenye Administration yake kwa Kile Kinachoitwa "Mafahali wawili hawakai zizi moja" Ndio maana hakumtetea sana, na Lowassa atakuwa labda alimwonesha dharau bila kujua katika mikutano yao ya cabinet. Habari ndio hiyo. Ila wapo waliomkomalia Lowassa kwa maslahi yao mengine. Kama Mwakyembe a) Alikuwa anataka mkataba wa Kuzalisha Umeme (b) Aliutaka Uwaziri Mkuu (c) Alikuwa na Nia ya Kummaliza Lowassa ili ajisafishie njia yeye ya kugombea Urais kama alivyofanya 2015.
 
Makonda hajaongopa..!! Huyu kabwe si wenje kipindi ni mbunge wa nyamagana mara ngapi Kalia nae kuhusu ufisadi wake.. Kama dar alionewa, basi aliyofanya mwanza na mbeya kuna elements za ufisadi. Makonda yupo sahihi.
 
alijiuzulu uwaziri mkuu kwa sababu ya ufisadi wa richmond...huo ni ushahidi tosha
Serikali ilipoteza sh ngapi kwenye Richmond?Ukinithibitishia kama serikali ilipoteza hata thumni,leo najiondoa JF..mnakaa kukariri kama kasuku nyimbo za mabwana zenu bila kutumia bongo zenu zilizojaa tope kufikiri japo kidogo
 
PAMOJA na kuelezwa kuwa umauti hauna adui, lakini kwa msiba huu wa Wilson Mbonea Kabwe umekuwa tofauti. Una maadui, tena maadui wasiofahamu maisha yake, utendaji na uadilifu wake katika kazi, anaandika Henerico Mayanja.

Hawa ni maadui waliojipambanua kuwa liwalo na liwe, lazima Kabwe aingie katika kitabu cha kumbukumbu za aibu, tena aibu ya tuhuma za wizi na ufisadi, licha ya kuwa na rekodi iliyotukuka katika maeneo mengi aliyofanya kazi.

Walioamua kuwa maadui wake, wanaongozwa na Paul Makonda, mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam, anayedaiwa kujiapiza kumng’oa Kabwe katika nafasi yake ya ukurugenzi wa jiji alilokuwa akiliongoza, akimwakilisha Rais John Pombe Magufuli.

Uadui wa Makonda kwa Kabwe unaelezwa na watu waliokuwa karibu na Kabwe na hata yeye mwenyewe kabla ya kukutwa na umauti Mei 20, mwaka huu.

Ieleweke kuwa utendaji uliotukuka wa Kabwe ndiyo umemfanya kuwa mkurugenzi wa majiji matatu kwa nyakati tofauti; Mbeya, Mwanza na baadaye Dar es Salaam, akiteuliwa na marais wawili; Benjamin Mkapa na Jakaya Kikwete kuongoza na kusimamia kasma, fedha na utendaji wa majiji hayo kwa mafanikio makubwa.

Watu wanajuliza, endapo Kabwe angekuwa mwizi na fisadi ni namna gani angeweza kuaminiwa na marais wote hawa, tena akiwamo Mkapa ambaye umakini wake unasifika, siyo Tanzania tu, bali dunia yote.

Ukiacha sifa hizo za utendaji kutoka kwa marais hao, hata katika salamu za serikali wakati wa msiba wa Kabwe nyumbani kwake, Msasani, Dar es Salaam, George Simbachawene, waziri wa nchi, ofisi ya rais, tawala za mikoa na serikali za mitaa (Tamisemi), alisema Tanzania imepoteza kiongozi mahiri na mwaminifu aliyeitumikia nafasi yake kwa umakini na weledi mkubwa kwa manufaa ya wananchi.

Kauli ya Simbachawene inaaminika na wengi waliokuwepo kwenye msiba huo kuwa inatoka kinywani kwake kwa dhati kabisa kwani alimfahamu Kabwe kwa muda mrefu na haina chembe ya unafiki uliozoeleka misibani.

Waziri huyo alisema- “kwa ngazi aliyokuwa amefikia Kabwe ni sawa na katibu mkuu wa wizara, leo hii ukiizungumzia Mwanza inayosifika kwa usafi na miundombinu, huwezi kuacha kumtaja Kabwe..

Alifanya mengi sana kwa ajili ya maendeleo ya Mwanza na maeneo mengine alikokuwa akifanya kazi za wananchi kwa niaba ya serikali, hakika serikali imepoteza mtumishi hodari na sisi tutaenzi mchango wake kwa kuendeleza mema aliyofanya Kabwe,” alisema Simbachawene.

Kauli hiyo ya Simbachawene na uteuzi wa kuaminiwa wa Mkapa na Kikwete ni ushahidi mwingine wa kutosha kuwa Kabwe hakuwa “mlaji,” alijitoa kufanya kazi za umma kwa uaminifu mkubwa na kupata fursa ya kutoa mchango wake katika kuendeleza majiji ya Mwanza, Mbeya na Dar es Salaam.

Lakini pamoja na mchango mkubwa wa Kabwe, anajitokeza Makonda, kijana mdogo katika utendaji wa kazi za serikali na utumishi wa umma akiwaeleza Watanzania kuwa Kabwe ni mtuhumiwa wa ufisadi.

Bila aibu, mbele ya wakazi wa Dar es Salaam na Watanzania kwa ujumla wao, Makonda wakati wa ufunguzi wa Daraja la Mwalimu Nyerere, linalounganisha Dar es Salaam na Kigamboni, alimchongea Kabwe na kumuonesha kuwa ni mtu asiyefaa.

Kwa staili ya Rais John Magufuli, bila kufanya utafiti alikubaliana na Makonda na kuamua kumsimamisha kazi Kabwe kwa tuhuma za kumdhalilisha, tena mbele ya umma.

Makonda alimchongea Kabwe Aprili 19 na baada ya siku 30, Kabwe mwenye miaka 60 alifariki dunia kwa ugonjwa ambao, pamoja na maelezo tofauti kuhusu chanzo cha kifo chake, upo uwezekano kuchangiwa na msongo wa mawazo kwa kudhalilishwa na kijana mdogo aliyeshindwa kuitambua vyema historia yake ya utendaji, hata kumwaminisha Rais Magufuli uongo.

Katika kutetea utu wake, Kabwe alisononeka mno kwa uamuzi wa Rais Magufuli na uchonganishi wa Makonda kwa kiongozi wa nchi.

Kabwe alisema; “mimi sihusiki na mikataba inayosemwa na Makonda, huu ni uongo mtupu, Makonda ametoa taarifa za uongo kwa Rais Magufuli akiwa na lengo la kunichafua na kunionesha mimi ni mtu wa hovyo ninayeendekeza ufisadi, hakika nimesikitika mno na kuumizwa.”

Aliongeza kueleza; “tuhuma zinazoelekezwa kwangu ni za uongo na zimelenga kunichafua mbele ya rais, nasisitiza tena hakuna mkataba wowote ambao ofisi yangu iliingia kwa nia ya kupoteza mapato ya serikali.”

Kabwe akaendelea kulalamika kwa uchungu; “hiki kinachodaiwa kupotea na Makonda kimepotea kutoka wapi?… huu ni upotoshaji wa wazi, hizo Sh. 3 bilioni zilichukuliwa na nani.”

Hadi mauti yanamkuta, Kabwe ndiye mkurugenzi pekee hadi sasa aliyewahi kuongoza majiji matatu Tanzania kwa nyakati tofauti na amekuwa na uzoefu wa miaka 19 katika uongozi wa serikali za mitaa.

Mbali na uzoefu huo, Kabwe ni mwanasheria, akiwa wakili wa Mahakama Kuu ya Tanzania na pia mmoja ya wanabodi wa benki ya jamii Dar Es Salaam (DCB).

Wakati sifa zote hizo zikilazimishwa kufutwa na Makonda kwa kumchongea, na hatimaye kusimamishwa kazi na baadaye kukutwa na umauti, Makonda ameguswa, kusutwa na nafsi yake na kuukata mshipa wa aibu. Akajitokeza kwenda kuhani msiba.

Ni haki yake kwenda kuhani msiba wa Kabwe, lakini kwa jitihada zake binafsi kumchafua Kabwe kwa rais na mbele ya umma, imedhihirika kuwa mshipa wake wa aibu umekatika.

Kabwe amefariki dunia akilia. Akitoa chozi na sononeko la nafsi kwa namna alivyotendwa na kiongozi aliyeamua kumchongea tu kwa sababu anazojua yeye.

Sasa chozi la Wilson Mbonea Kabwe limekoma. Hatalia tena juu ya uso wa dunia, kwani limekatizwa na umauti. Alale salama.

Makala hii imeandikwa katika Gazeti la Mseto la tarehe 26 Mei mpaka tarehe 1 Juni mwaka huu katika ukurasa wa 5.
Mkuu usifukue makaburi, Kabwe kafanya kazi yake amemaliza kazi yake duniani.
Hata hivyo conveniently huongelei sakata lililomtoa kafara mzee huyu.
Ni Ubungo.
Mbona huongele suala la tozo kwa basi moja linalolipiwa shs 8,000 lakini Jiji linalipwa nusu yake yaani shs 4,000, suala lililoibuliwa na Makonda.
Mnaweza kumlaumu Makonda kwa kutokuwa na uzoefu, lakini wizi wa wazi namna hiyo usio na maelezo ,kuuelezea kivingine ni unafiki.
Kwa hili Makonda si mnafiki.
 
Huo umakini wa Mkapa ni Upi??!!!!!!....Umakini wa kuuza NBC au kujiuzia Kiwira???

EPA, Meremeta n.k zote hizi zilifanyika wakati wa Mkapa..... Teuzi za Tanzania hazizingatii Uchapakazi bali Urafiki..

Kebwe Tumuombee huko aliko... Ila alikuwa fisadi aliyekubuhu.
 
Mimi naungana na Makonda.... Swala lilimtoa Kebwe ni wizi wa Tozo Za Magari Ubungo..... Yeye akiwa Bosi wa Jiji hakuliona hilo???
 
Makonda hajaongopa..!! Huyu kabwe si wenje kipindi ni mbunge wa nyamagana mara ngapi Kalia nae kuhusu ufisadi wake.. Kama dar alionewa, basi aliyofanya mwanza na mbeya kuna elements za ufisadi. Makonda yupo sahihi.
Jibu swali chadema walimsimamisha kazi
 
Sasa naanza kujua kwa nini , kama chama hamkujiushisha kuhakikisha Wenje anarudi bungeni! Mwanzisha mada hamkuridhishwa na maelezo ya Wenje juu ya Kabwe na ufisadi. Mmenishangaza sana!!!
 
Mimi naungana na Makonda.... Swala lilimtoa Kebwe ni wizi wa Tozo Za Magari Ubungo..... Yeye akiwa Bosi wa Jiji hakuliona hilo???
Je kwenye kumsimamisha mlifuata sheria za kazi?
 
Huo umakini wa Mkapa ni Upi??!!!!!!....Umakini wa kuuza NBC au kujiuzia Kiwira???

EPA, Meremeta n.k zote hizi zilifanyika wakati wa Mkapa..... Teuzi za Tanzania hazizingatii Uchapakazi bali Urafiki..

Kebwe Tumuombee huko aliko... Ila alikuwa fisadi aliyekubuhu.
Mimi siangali ufisadi wake wala simtetei penye kosa lazima sheria zifuatwe lakini kwenye kumsimamisha sheria ilifuatwa?
 
Back
Top Bottom