Chozi la Kabwe kwa Makonda limekoma

Chozi la Kabwe kwa Makonda limekoma

Haifahamiki vizuri kuhusu ufisadi wa Kabwe. Kadhalika haifahamiki vizuri kama kweli kulikuwa na bifu na hivyo Makonda alichongea tu. Lakini kitu kimoja ambacho binadamu ni lazima wafahamu ni kwamba ni vyema kufanya kila jambo kwa nia njema na kwa ukweli.

Tufahamu kwamba sisi si mali yetu wenyewe. hatukujiumba au kujitengeneza. Hakika tutajibu siku isiyo na jina juu ya yote mabaya tuliyotenda au kumtendea binadamu mwenzetu pasipo hatia au kosa.
 
Nasikia marehem alioa nyumba moja na mkulu mmoja... ya kweli hii?... kama ni kweli labda ni nepotism na sio utendaj ilio muweka pale... ila mimi simjui vizuri mkuu am just thinking louder....
Je utendaji wake ulikuaje alistahili kufanyiwa aliyofanyiwa?
Mkuu kama nilivo sema utendaji wake siujui vizuri ila watu wanasmea sbb alikuwa na kaka mkulu ndo maana ali panda kirahisi....lakini all in all, kilicho fanyika hasa kwa sbb alikuwa anaumwa halikiwa sawa.....
 
alijiuzulu uwaziri mkuu kwa sababu ya ufisadi wa richmond...huo ni ushahidi tosha
Huo sio ushahidi. Alijiuzuru kama walivyowahi kufanya Mzee Mwinyi akiwa Waziri wa Mambo ya Ndani 1974. Kuwajibika.
Lakini Ndugu yangu, kama Wewe unao ushahidi vinginevyo, utoe na uutumie kumpeleka kwenye vyombo vya dola ili ashitakiwe.
 
Mbona Lowasa ni fisadi toka enzi za Nyerere lakini aliaminiwa na Mkapa na Kikwete akapewa mpaka uwaziri mkuu? Teuzi nyingi zinaangalia urafiki..sio maadili
Kama ni ufisadi basi wangempeleka mahakamani na sio kulalamika nje tu wakat sheria ipo
 
Nasikia marehem alioa nyumba moja na mkulu mmoja... ya kweli hii?... kama ni kweli labda ni nepotism na sio utendaj ilio muweka pale... ila mimi simjui vizuri mkuu am just thinking louder....

Mkuu kama nilivo sema utendaji wake siujui vizuri ila watu wanasmea sbb alikuwa na kaka mkulu ndo maana ali panda kirahisi....lakini all in all, kilicho fanyika hasa kwa sbb alikuwa anaumwa halikiwa sawa.....
Hapa tunaangalia pia sheria ya kazi ya kuajiri kusimamisha na kufukuza haya mambo ya kukurupuka na kusimamisha au kufukuza kwa kigezo cha kutumbua siyo chakuungwa mkono maana kutaingia mambo mengi sana mf. Chuki, kuonekana na mengine mengi tufuate sheria tulizojiwekea wenyewe
 
Naona mnataka kutotoa nje ya mada kwa faida ya mizuka wenzako ngoja nikujibu tu.. mnajua ccm mliaminisha umma wa Watanzania Lowassa ni fisadi bila kuwa na ushaidi kisa kikiwa ni uwaziri mkuu? Mbaya zaidi Watanzania wameshajua chuya na mchele ni upi usani na ukweli ni upi 2020 siyo mbali
Chadema wakiongozwa na tundu lisu na dr.slaa ndio waliomtaja lowasa ni fisadi
 
Vijana wa ccm, wanaishi kwa kujipendekeza. Nahilo ndo tatizo, kutafuta tonge kwa majungu.
 
Chadema wakiongozwa na tundu lisu na dr.slaa ndio waliomtaja lowasa ni fisadi
Nimeshawajibu pale juu wazee wa mizuka kua ccm iliaminisha Watanzania kua Lowassa ni fisadi tatizo likiwa ni uwaziri mkuu lakini watanzania wameshawashtukia kua ccm ni mizuka mingi 2020 siyo mbali
 
Mkataba wa bilioni 3 ukasababisha huyu mzee kusimamishwa kazi ktk mazingira ya kufedhehesha wakati kuna mikataba ya kifisadi ya kutisha ya mabilioni inayohusisha watumishi wa umma pia mtumbua maji kanywea kawa mdogo km piritoni ;

1. Lugumi 39bn watu wake wanapeta hadi leo

2. Tegeta/Escrow account over 300bn

3. EPA over 130bn

4. Meremeta,

5. Kagoda

6. Nyumba za serikali

7. Kivuko cha magogoni/Bagamoyo

8. Fedha za Radar na mengine kibao tu!!

Jibu ni moja tu.

Hakuna dhamira ya dhati bali ni usanii uleule kutoka kwa watu walewale. Yaani jamaa wanajifanya kupambana na uchafu lakini ukweli ni kuwa wanapumbaza watu na kusafisha njia za wao kuiba na kuitafuna nchi hii zaidi na zaidi!!

Zaidi sana ni visasi tu.

Na kwa mtindo huu Tanzania hii kamwe haiwezi kwenda mbele kwa viongozi wasanii na wanafiki kama hawa wanaotenda kwa visasi kama hawa kwa kivuli cha dhamira ya kuwaletea watanzania maendeleo!!
umesahau richmond mkuu
 
Umesahau kuwa tatizo lilikua ni uwaziri mkuu ile report mbona ilisomwa nusu iliachwa kwa maslai ya nani? Je ni wapi ilisema Lowassa kachukua hela? Wacha mizuka
Ile report ilionyesha wazi kabisa jinsi lowasa kama waziri mkuu akishinikiza kuvunjwa kwa taratibu za upatikanaji wa mzabuni na kuonyesha upendeleo kabisa kwa kampuni ya richmond,hakuna namna mnayoweza kukwepesha uhusiano wa lowasa na richmond.
 
alijiuzulu uwaziri mkuu kwa sababu ya ufisadi wa richmond...huo ni ushahidi tosha


acha kuwa na akili fupi kama mkia wa NGURUWE
kujiuzuru kwa Muhonga kwa kashifa ya escrow mbona hakujamuondolea sifa ya kuteuliwa tena na kuongoza wizara ileile?
tatzo watu ccm imewageuza misukule hamna tena uelekeo
 
Hili la kabwe kuwa fisadi mkubwa si lakubishania. Nenda mwanza uambiwe nini ufisadi wa Kabwe. Luchelele jirani kabisa na Saint Augustine University alifanya nini juu ya viwanja vile, uwekezaji mkubwa alioufanya Luchelele mabilioni hayo aliyatoa wapi? Zawadi aloitoa kwa kiongozi mmoja mkubwa wa Taifa hili, zawadi ilitoka pembezoni mwa ziwa Victoria kifisadi kabisa watu wa mwanza wanajua, aliitoa wapi pesa hiyo? Sio hapo tu, iliyokua clinic ya makongoro ambayo ilikua ikitoa Huduma kwa akina mama na watoto takribani mwanza yote, iko wapi sasa kama sio jitihada zakifisadi za kabwe, tusiwe wanafiki, tuongee ukweli.Kabwe alikua fisadi mkubwa tens mwenye kiburi. Kama kuna mwana JF mwenye mchango was Wenje unaohusu ufisadi wakabwe atuwekee hapa tafadhari.

Hivi huyu Kabwe hilo jiji la Mwanza alikuwa analiongoza peke yake kiasi ambacho kwenye clinic yupo, viwanja yupo, ferry za samaki yupo....yaani kila mahali yupo....yupo....yupo...eeeh!!?

What is this nonsense aisee?

Hakuwa na wasaidizi? Hakuwa na wanasheria? Hakuwa na Baraza la madiwani? Hakukuwa na RC? haukuwa na maafisa ardhi?

Hivi ni kwa nini tusiseme na kukubaliana kuwa matatizo haya ni zaidi ya kumshambulia mtu mmoja mmoja tu?

Haiwezekani kamwe na milele haya mambo yafanywe na mtu mmoja kama siyo special organized system!!

Kabwe ni muhanga tu.....tusipumbazane hapa. Ni sawa na Richmond vs Lowassa mwaka 2008, huyu mzee alikuwa ni muhanga tu!

The problem is bigger than we think and it goes beyond one person!!
 
Ile report ilionyesha wazi kabisa jinsi lowasa kama waziri mkuu akishinikiza kuvunjwa kwa taratibu za upatikanaji wa mzabuni na kuonyesha upendeleo kabisa kwa kampuni ya richmond,hakuna namna mnayoweza kukwepesha uhusiano wa lowasa na richmond.
Kwenye report hakuna sehemu yoyote inaonyesha Lowassa alichukua hela pili takokuru haikuwepo mlimpeleka Mahakamani? Tatizo lilikua uwaziri mkuu
 
Back
Top Bottom