Choo cha kulipia Tegeta sokoni kimeniharibia siku

Kiashiria kimojawapo kikubwa kwa ustaarabu wa binadamu ni matumizi sahihi na usafi wa choo.
 
Niende moja kwa moja.

Nimeingia sokoni, nikaona siwezi kufika kwangu na mizigo, acha leo nijistri vyoo vya kulipia Tegeta loop salaleee!

Ni Muda huu nahisi Leo sitakula, nimekata tamaa kabisa. Ndani ya vyoo hivi unatoka na ugonjwa. Jamaniee sikushauri ukaangalie, panatia huruma. Nzi, kinyesi juu sijui, Jaman MTU kamaliza kupata huduma anashindwaje kusafisha.

Siku yangu imeharibika mapema Sana Kwa hali hii safari ni ndefu ndefu Sana ikiwa usafi wa choo uko vile.

Kinondoni mnapokea malipo ya huduma kwa vyoo vile, jiangalieni
Hao unaowalipa hawafanyi usafi?
 
Niende moja kwa moja.

Nimeingia sokoni, nikaona siwezi kufika kwangu na mizigo, acha leo nijistri vyoo vya kulipia Tegeta loop salaleee!

Ni Muda huu nahisi leo sitakula, nimekata tamaa kabisa. Ndani ya vyoo hivi unatoka na ugonjwa. Jamaniee sikushauri ukaangalie, panatia huruma. Nzi, kinyesi juu sijui, Jaman MTU kamaliza kupata huduma anashindwaje kusafisha.

Siku yangu imeharibika mapema Sana Kwa hali hii safari ni ndefu ndefu Sana ikiwa usafi wa choo uko vile.

Kinondoni mnapokea malipo ya huduma kwa vyoo vile, jiangalieni
Fanya ukapime UTI kabisa aiseeh usijekumpelekea mwenzio nyumbani
 
Vyoo vya sokon vipo hivyo vyote mkuu labda utakuwa mgeni kwenye masoko ya nchi hii
 
Kuna watu nahisi wana ugonjwa wa kujisaidia pembeni au kujisaidia na kuacha alichotoa...sidhani kama ni akili ya kawaida
 
system za kukatia nyengo maeneo ya sokoni hazijawahi kuwa safi kabisaa sio hapo tu lakini maeneo mengi.

Hapo sehem ingekua salama n kwenye lodge ya karibu, sema.sasa nako n mtihani.

Mmama wa watu umetoka zako kushusha kimba na vimfuko vyako vya nyanya na njegere ile unatoka nje unakutana na yule jirani yako mmbeya. Ghafla mtaa mzima.unajua ulienda kukandamizwa asubuh na mapema gesti za sokoni.
 
Swali la msingi ni kwa nini tuna vyoo vya kulipia kwanza? Katika jamii iliyostaarabika, sehemu za umma huduma ya vyoo haitakiwi kuwa ya kulipia maana hiyo ni huduma ya msingi ya jamii na kuna makusanyo mengi ya ushuru yanafanyika pale. Halafu unaweza kulipia ukakuta vyoo vya hovyo vilevile.

Bado tupo nyuma saaana.
 
Back
Top Bottom