Chombezo: Chachandu za Beka wa Tanga

Chombezo: Chachandu za Beka wa Tanga

CHACHANDU ZA BEKA WA TANGA
-26
Mpenzi msomaji, wiki iliyopita
niliishia pale Rey na Beka waliokuwa
wameelezana hisia zao za mapenzi
walipochepuka na kupita njia ya
uchochoroni. Hawakutembea muda
mrefu, Beka aliyevutiwa sana na Rey
alimvamia msichana huyo na kuanza
kumshika hapa na pale. Je, kilifuatia
nini? Tuwe pamoja…
eka akiwa anakiletea fujo kifua
kibichi cha Rey huku akijisemea
moyoni kwamba ‘sikuachi kimbe
wewe’, mtoto huyo alijisikia raha
iliyopitiliza lakini hakujua kama
kinjia hicho cha uchochoro
walichokuwepo kilikuwa kinapendwa
sana kutumiwa na baba yake mzee
Kibandiko.
Kufuatia Rey damu kumwenda mbio,
akaona halikuwa jambo la busara
kutorudisha mashambulizi si naye
akaanza kukichezea kifua cha Beka!
Wakati vijana hao waliyoyaanza
mambo ya mapenzi mapema
wakiletea fujo, mzee Kibandiko
aliyekuwa amekwenda kumuona
rafiki yake mzee wa Shamba akawa
anarejea nyumbani.
Kama nilivyokuambia kwamba
alikuwa anapenda sana kupita ile njia
ya uchochoroni, akiwa ametembea
mita kadhaa mbele yake akaona
kama kulikuwa na watu waliokuwa
wamegandana.
Kwa kuwa alikuwa mtu mzima alijua
watu aliowaona walikuwa wa jinsia
tofauti waliokuwa wakipashana joto
la yale mambo yetu.
Kutokana na mzee huyo kuwa mnazi
mzuri wa mambo ya malovee,
akapunguza mwendo na kuanza
kusonga mbele kwa kunyata kama
paka aliyemuona panya mbele yake.
Lengo lake alitaka kuwapiga chabo
vizuri na kuona mwisho wa yote
ungekuwaje, kila aliposogea mbele
alikuwa akijibanza kwenye nyumba.
Wakati huo Beka na Rey waliokuwa
wanaamini walikuwa eneo salama,
waliendelea na yao bila kumuona
mzee Kibandiko aliyekuwa amevaa
shati nyeusi iliyomfanya asionekane
vizuri.
Mzee Kibandiko alipokuwa mita
chache japo kigiza kilianza
kuchanganya aliweza kubaini
aliyekuwa kamtaiti ‘mtu’ alikuwa ni
Beka akajikuta akijisemea moyoni
‘shabashi’.
Msemo huo alikuwa akipenda sana
kuutamka alipofurahisha na jambo
kwani hakutegemea kabisa kama
Beka angeweza kumtaiti mtu kwa
jinsi alivyokuwa akimfahamu.
Kutokana na mzee huyo kuwa na
akili zilizomtosha mwenyewe,
akasema moyoni kwamba lazima
aufuatilie mpambano wa Beka na
msichana aliyekuwa naye hadi
mwisho.
“Haya ndiyo mambo ninayoyataka,
mtoto wa kiume lazima uoneshe
urijali wako, sasa sijui huyu ndiye
aliyemla kuku wake na kumtoa
wekundu wa msimbazi?” mzee
Kibandiko aliwaza.
Wakati mzee huyo kabana pale
chocho na Beka na Rey wakiwa
wanashikana hapa na pale,
wakatokea vijana wawili.
Mzee Kibandiko alipowaona
alijifanya anajisaidia haja ndogo,
wale vijana waliposogea mbele Beka
na Rey waliwaona wakatimua mbio
kila mtu na njia yake.
Kitendo hicho kilimkera sana mzee
Kibandiko akaishia kutoa msonyo
mkubwa na kuwalaumu wale vijana
kusababisha Beka na Rey kutimka.
“Hawa vijana wa hili jiji wamepinda
kweli, si umewaona walivyoachiana
fasta na kutimua mbio?” mmoja wa
wale vijana alimwambia mwenzake.
“Yaani ni balaa, sema hatukujua
tungewashtukia mapema
tungejibanza ili tuone mchezo hadi
mwisho…yule jamaa lazima
angemchinja mtoto, wewe si umeona
uchochoro ulivyotulia?” kijana
mwingine alimwambia mwenzake
wakacheka.
Hata hivyo, kijana mwingine machale
yalimcheza kwamba hata mzee
Kibandiko alikuwa akiwachabo wale
vijana.
“Kwa nini unasema hivyo?” kijana
mwingine alimwuliza mwenzake.
“Wewe elewa hivyo kwani wakati
tunakaribia lile eneo nilimuona akiwa
ametulia anawaangalia lakini
alipotuona akajifanya anajisaidia na
tulipotoka katoa msonyo wa nguvu,”
yule kijana akamwambia rafiki yake,
wakacheka.
“Ila kweli maana kuna baadhi ya
wazee wa huu mji wamepinda na
wanapenda sana mambo hayo,”
kijana wa pili alimwambia
mwenzake.
Baada ya wale vijana kuendelea na
safari huku maongezi yao yakiwa juu
ya Beka na Rey waliokuwa
wametimua mbio, mzee Kibandiko
aliendelea kuwalaani kwa
kumuharibia picha yake.
“Hata hivyo, Beka anazidi kunipa
raha maana mtoto wa kiume
anafuata nyao zangu… mwaka huu
utakuwa ni wa zawadi kemkem
kwake,” mzee huyo alijisemea
moyoni.
Wakati mzee huyo ameshika njia
kuelekea nyumbani kwake, Beka na
Rey waliotoka nduki hawakuweza
kuonana tena kwani kila mmoja
alikwenda kwao.
Beka alipofika nyumbani mtu wa
kwanza kukutana naye alikuwa
mama yake aliyemkuta anaandaa
chakula jikoni.
“Mama za wakati huu!” Beka
alimsabahi mama yake.
“Nzuri mwanangu, mbona hivyo?”
mama alimwuliza.
“Vipi mama?” Beka alimwuliza mzazi
wake.
Mama yake akamwuliza mbona
alikuwa amechelewa kurudi
nyumbani alikuwa wapi, Beka
alimdanganya kwamba alikuwa kwa
rafiki yake Zuberi kujisomea.
Kwa kuwa mama huyo alikuwa
akifurahishwa sana na tabia ya
mwanaye kupenda kujisomea,
alimfagilia sana kisha akamwambia
aende akaoge ili ale.
Beka alimshukuru mama yake
akaenda kuoga, akiwa bafuni baba
yake alirejea akiwa mwenye furaha
kwani alikuwa akiimba.
Mkewe aliyekuwa anamfahamu vizuri
mumewe anavyokuwa akifurahi,
alijua alikotoka alifurahishwa na
jambo flani, akamuuliza:
“Haya mwenzangu umefurahishwa
na nini na kama umepata pesa nami
nigaie,” mama huyo alimwuliza
mumewe akiwa kanyoosha mkono
kusubiri apewe ‘mpunga’.
“Yaani mke wangu, kadiri siku
zinavyokwenda mwanao Beka
anazidi kunipa raha na kuniongezea
siku za kuishi hapa duniani!” mzee
huyo alimwambia mkewe.
“Kwani kafanyaje na unaposema
anakuongezea siku za kuishi yeye
kawa Mungu?” mkewe alimwuliza.
Kufuatia kuulizwa hivyo, mzee
Kibandiko alicheka sana na
kumwambia aliposema
anamuongezea siku anamaanisha
mtu anapokuwa na furaha siku zake
za kuishi zinaongezeka.
“Kweli baba Beka una mambo, haya
niambie mtoto kafanyaje
kilichokufurahisha nami niungane
nawe kufurahi!” mama huyo
alimwambia mumewe.
Je, baada ya kuulizwa hivyo na
mkewe atafunguka kuhusu Beka
kuanza kuwashughulikia ‘viumbe’?
 
Mabwaku!!!
"Mwaka huu utakuwa ni wa zawadi kemkem kwake"
Yaaniiiii. ....

Halafu sijui kama akigundua beka anamtarget msichana mwingine si ndo atamnunulia pikipiki kabisa!!!
 
Mabwaku!!!
"Mwaka huu utakuwa ni wa zawadi kemkem kwake"
Yaaniiiii. ....

Halafu sijui kama akigundua beka anamtarget msichana mwingine si ndo atamnunulia pikipiki kabisa!!!

kwi kwi kwi...hapo pikipiki inamuhusu
 
Jamani story ndiyo imeisha au mbona hakuna tena mwendelezo!!?
 
Back
Top Bottom