chizi mtikila adai fidia ITV

Pdidy

JF-Expert Member
Nov 22, 2007
50,956
22,149
Mkuchika aisubiri Polisi suala la Mtikila
Mwandishi Wetu
Daily News; Tuesday,October 28, 2008 @00:02

ZA chichiemu hazikumtosha

Waziri wa Habari, Utamaduni na Michezo, George Mkuchika, amesema anaiachia Polisi kuchunguza suala la Mchungaji Christopher Mtikila, la kumwomba akifungie Kituo cha Televisheni cha ITV cha Dar es Salaam, baada ya kupata taarifa kwamba wameanza kulishughulikia suala hilo.

Akizungumza na gazeti hili, Msemaji wa wizara hiyo, Jacob Tesha alisema amezungumza na Waziri kwa simu jana mchana akiwa safarini kwenda Dodoma kwenye kikao cha Bunge kinachoanza leo, ili kufahamu hatima ya suala hilo na kumueleza hayo.

Alisema Waziri Mkuchika amekiri kupata barua ya Mtikila ambaye pia ni Mwenyekiti wa chama cha DP akimwomba aifungie ITV kwa kile alichodai wametangaza habari ya uongo aliyokwisha itolea taarifa katika mkutano wake na waandishi wa habari siku moja kabla kuwa ni ya kughushi.

Kwa mujibu wa barua hiyo ambayo nakala tunayo, Mtikila anadai kuwa Oktoba 6, mwaka huu mjini Tarime, alipata taarifa kwamba Chadema ilikuwa ikisambaza taarifa iliyoonyesha imeandikwa naye inayokisafisha chama hicho na tuhuma ya mauaji ya aliyekuwa Mbunge wa Tarime, Chacha Wangwe.

“Oktoba saba, Polisi walichukua maelezo yangu kuwa taarifa hiyo ni ya kughushi na siku iliyofuata niliitisha mkutano maalumu wa waandishi wa habari katika Sky Lodge ambao ulihudhuriwa pia na waandishi wa IPP inayomiliki ITV…nikasisitiza kuwa taarifa inayosambazwa na Chadema ikionyesha nimeandika mimi si ya kweli ni ya kughushi,” ilieleza sehemu ya barua ya Mtikila.

Katika barua hiyo ya Oktoba 20, mwaka huu, Mtikila alidai siku moja baada ya mkutano huo, katika kipindi maalumu baada ya taarifa ya habari ya ITV, ilisomwa taarifa hiyo yote huku wakijua kuwa ni ya uongo. Hata hivyo, Mkurugenzi wa Makosa ya Jinai, Robert Manumba, juzi alikiri kupokea malalamiko ya Mtikila kuhusu tukio hilo na kwamba uchunguzi unaendelea ili kubaini hasa ukweli kuhusu suala hilo.

Uongozi wa ITV ulisita kuzungumzia suala hilo baada ya kila siku walipotakiwa kuzungumza, kudai wasemaji wakuu wapo vikaoni na waliokuwapo walisema hawana taarifa kuhusu suala hilo. Jana, Mtikila alipoulizwa kuhusu uamuzi huo wa Waziri Mkuchika, alisema anasubiri majibu yake kwa maandishi kwani anafahamu kuwa waziri ana nafasi yake kama uongozi kushughulikia hilo na endapo atachelewa, atamfuata Dodoma katika kikao cha Bunge aliko ili kumshinikiza kushughulikia suala lake.
 
Mbona sijaona sehemu inayosema anadai fidia?, au ndiyo "GOTCHA" presentation of threads. badilisha heading yako iendane na habari ndugu "Predeshe". Au ni tatizo la kiufundi - translation maana naona sorce yako ni "Daily News"
 
rekebisha hiyo title, hata kama hukubaliani nae lakini kumwita chizi si muzuri.
 
Mbona sijaona sehemu inayosema anadai fidia?, au ndiyo "GOTCHA" presentation of threads. badilisha heading yako iendane na habari ndugu "Predeshe". Au ni tatizo la kiufundi - translation maana naona sorce yako ni "Daily News

TEEEH TEEEH!!!!!!!!!!!!!! MKUU SWALA LA FIDIA ALIKUWA AKIROPOKA JANA POSTA MPYA PALE KWENYE CANTEEN YA POSTA ,,HATUKUJUA KUNA HABARI KAMA HII INATOKKA NKASEMA NIMTAAHADHARISHE MCHAGA MWENZANGU MENGI ASIJE KUUMIA HUYU JAMAA ANA LENGO GANI BWASHEE!!!!NI HILO TU

TRANSALATION KWA KWELI!!!!!!!!!!!!!MEKU SIO TATI TATIZOOO KWELI!!!!!!!!
 
Mbona sijaona sehemu inayosema anadai fidia?, au ndiyo "GOTCHA" presentation of threads. badilisha heading yako iendane na habari ndugu "Predeshe". Au ni tatizo la kiufundi - translation maana naona sorce yako ni "Daily News

TEEEH TEEEH!!!!!!!!!!!!!! MKUU SWALA LA FIDIA ALIKUWA AKIROPOKA JANA POSTA MPYA PALE KWENYE CANTEEN YA POSTA ,,HATUKUJUA KUNA HABARI KAMA HII INATOKKA NKASEMA NIMTAAHADHARISHE MCHAGA MWENZANGU MENGI ASIJE KUUMIA HUYU JAMAA ANA LENGO GANI BWASHEE!!!!NI HILO TU

TRANSALATION KWA KWELI!!!!!!!!!!!!!MEKU SIO TATI TATIZOOO KWELI!!!!!!!!

Ina maana mmiliki wa ITV asingekuwa Mchaga usinge mtahadharisha?:eek:
Jaman ndugu WaTanzania, tujitahidi kuacha Ukabila na Udini.
 
Back
Top Bottom