Chini ya Uongozi wa Rais Samia, Vikundi 52 vyanufaika Arusha

kalacha mateo

Senior Member
Sep 27, 2021
118
237
Msisitizo wa Rais Samia Suluhu ni 10% za mapato ya Halmashauri zitolewe kama mkopo kwa Vijana, wananawake na walemavu. Pesa hizo zinasaidia makundi hayo kujiajiri na kuendesha maisha yao ya kila siku. Mkoani Arusha milioni 404.5 zimetolewa kwa vikundi 52 vya ujasiriamali.

Katika vikundi hivyo 28 ni vya wanawake ambavyo vimepata Sh. milioni 198.6, vikundi 14 vya vijana vimepata Sh. milioni 143. Wanufaika wengine ni vikundi 10 vya walemavu waliopata Sh. milioni 62.9. Vikundi hivyo vinajihusisha na shughuli mbalimbali ikiwemo ufugaji, biashara ndogo ndogo na vyombo vya moto.

Awali Halmashauri ya Arusha ilitoa milioni 873.6 kwa vikundi 116 ikiwemo 108 vya wanawake. Ikumbukwe moja ya kipaumbele katika mpango wa maendeleo ya serikali ya awamu ya sita ni kukuza uchumi wa watu, Hivyo uwezeshaji huu unasaidia kundi kubwa la watanzania kukua kiuchumi na kukuza uchumi wa nchi yao.
 
Back
Top Bottom