Kama majengo umeshindwa kutuonesha. Tuoneshe basi japo High Speed Railway kutoka USA
Hizi hapa data za 2020
View attachment 2770359
High Speed Railway ndani ya USA ipo lakini kutokana na sababu za kijiografia na kiuchumi (sanjari na demographics), hakuna haja ya kuongeza network kupita kiasi. Kumbuka, hapa tunazungumzia nyanja zinazogusa wananchi moja kwa moja. Au umeshasahau?
Kabla ya kuanzisha mradi mkubwa wowote ule, serikali makini lazima izingatie costs and benefits. Hii issue ya HSR imekwisha jadiliwa katika bunge la Marekani (Congress) mara kadhaa.
Marekani ukizingatia population yake tayari ina large network ya usafiri wa ndege (domestic airline) ambayo inakidhi mahitaji ya wananchi kwa kiasi kikubwa. Kuongeza network ya HSR kupita kiasi kwa kipindi cha sasa ni matumizi mabovu ya rasilimali.
Kuhusu suala la geography na demographics: High Speed Railway inaleta manufaa zaidi ya kiuchumi kama population density ni kubwa na miji yenye wakazi wengi inakaribiana zaidi. Population kubwa ya Wachina iko katika miji ya mashariki zaidi mwa China kijiografia na ndiko ambako network yao ya HSR imejikita zaidi.
Population density ya Marekani ni ndogo kuliko China, isitoshe population imetawanyika zaidi (scattered) katika states mbalimbali tofauti na China, hivyo kupanua zaidi network ya HSR ni changamoto bila benefits kwenye uendeshaji wa mradi. Ni Wamarekani wangapi wenye safari za haraka watapanda treni ya mwendo kasi kutoka Los Angeles mpaka New York waache ndege ambayo ni nafuu na yenye kasi zaidi?
Sijui kama unafahamu kuwa Marekani ndiyo nchi yenye largest road network duniani. Pia Marekani hiyohiyo ni nchi yenye largest railroad network in the world kwa ajili ya usafirishaji wa mizigo (freights), usafiri wa umma n.k. Kuongeza network mpya ya HSR pia kunaleta athari kwa network kubwa ya reli ambayo tayari ipo na inaendesha uchumi.
Naomba nirudie:
Hapa tunazungumzia nyanja zenye manufaa na zinazogusa wananchi moja kwa moja kama ambavyo umesema wewe mwenyewe. Ndio maana hapo awali nilisema, ulinganisho wako wa miundombinu kati ya hizo nchi mbili una makosa mengi ya kisomi.