Venus Star
JF-Expert Member
- Dec 6, 2018
- 19,707
- 59,863
Hakuna marefu yasiyo na ncha. Huu ni msemo wetu waswahili ukiwa na maana ya kwamba hakuna kitu kikubwa kisichokuwa na mwisho wake.
Dunia yetu hii imekuwa na wababe wengi sana, waliweza kuleta mabadiliko makubwa sana hapa duniani. Walikuwepo akina Gilgamesh watawala ambao waliweza kujiita kuwa wao ni Mungu. Lakini walipita na kubakia kuwa Historia tu.
Staki niongelee historia sana. Lengo la uzi huu ni kutaka kupambanisha China na USA katika nyanja ambazo zinagusa wananchi moja kwa moja. Nyaja hizo ni:-
1. Miundombinu
2. Teknolojia
3. Maaendeleo ya Vitu na watu
UHALISIA WA USA
Hakuna mtu yeyote atakayebisha kuhusu Marekani kupata nguvu kubwa baada ya kuanguka kwa Ulaya. Kuanguka kwa ulaya kulitokana na Kupiganwa kwa vita mara kwa mara. Kuanzia kwenye vita vya kwanza vya dunia mpaka kwenye vita vya pili. Marekani ilipata nguvu kubwa sana.
Lakini mambo yanazidi kubadilika.
Baada ya marekani kushiriki katika vita mbalimbali uchumi wake unazidi kuyumba. Vita ya Afghanistan ilitikisa sana uchumi wa Marekani. Marekani kwa sasa Demokrasia imebadilika na kuwa vioja. Wanasiasa hawasikilizani kila mmoja anatafuta Kick tu. Hakuna anayetafuta maendeleo ya nchi kama hapo nyuma. Kila mwanasiasa anatafuta manufaa yake na familia yake tu.
KUIBUKA KWA CHINA
Kwa upande wa china Taifa hili limekuwa na historia kubwa sana. Hususani kwenye upande wa Biashara. Lakini miaka ya 1800s na 1900s china ilipotea. Lakini mwishoni mwa miaka ya 1980s China ilianza kujitafuta. Ndio maana leo sasa tunaanza kuilinganisha China na Marekani.
SIZE
USA: 9,833,517 sq km
China: 9,596,960 sq km