China na Xi Jinping vipi tena?

China na Xi Jinping vipi tena?

Sijui.

Ila kwa jinsi Wachina walivyo walaghai, si ajabu jeshi lao si bora kivile.

Kwanza hata uzoefu wa vita halina.
Sasa kama hujui unabisha nini sasa.

Hao wachina wamekulaghai nini wewe ?
 
Kiwango cha kodi za bidhaa zitokazo China kwenda Marekani sasa ni 145%.

Kiwango cha kodi za bidhaa zitokazo Marekani kwenda China ni 84%.

Naona Mchina kashindwa kwenda sambamba Mnyamwezi 🤣.

Nyie Wachina wa Kiuruwi na Tabata Sanene kujeni hapa mtoe maelezo [visingizio] yenu ni kwa nini mmeshindwa kula sahani moja na Trump.

145% dhidi ya 84% hakuna kabisa uwiano wala ukaribu wowote ule.

Mnazidi kuthibitisha kuwa ngoma nzito nzito hamziwezi. Mnachoweza ni ujanja ujanja na ulaghai tu.

Hata bidhaa zinazouzwa Temu, kwa mfano, ubora wake ni wa mashaka sana.

Nunua nguo toka Temu halafu ifue uone itavyobadilika 🤣.

Sijui kwa nini tu Wachina wako hivyo.

Ndo maana mimi siwawmini kabisa watu wanavyodai kuwa jeshi la China sasa hivi ndo jeshi la pili kwa ubora duniani.
WACHINA wamepandisha tariff yao imefika 125% ! For all American imports.
 
wewe ni mjinga mchina soko alilonalo marekani na pesa anayoingza kuliko ampoteze marekan bora awapoteze hao asia na afrika fatilia utajua unadhan marekan ni fala yan ww unaona mbali kuliko marekani na trump
Ww hunq akili %60 ya bidhaa zote za china zinauzwa barani Asia alafu unaongea utopolo.
Labda ungesema Afrika ningekuelewa.
 
Hii ni kweli.
Hata hapa JF tunaongeleaga maswala ya kimataifa kiushabiki. Watu hawaleti evidence wanaleta story za vijiweni.
Naungana na nadharia inayosema Jamiiforums ilikua na wachangiaji wa maana miaka ya 2005 mpaka 10 huko, sasa hivi hata hamu ya kuchangia unakosa, kwasababu watu hawajengi hoja, wanaleta ushabiki wa kitoto, si unaona hapo juu, jitu zima badala ya kujenga hoja objectively kivipi China haiwezi kujibu tariffs za Marekani katika namna ambayo watu ambao hawafaham kinachoendelea wangenufaika na hoja yake, badala yake bandiko zima ni ushabiki na emoji juu.

Kuna mjinga mwenzake pia atakuja na hoja ya kishabiki kwanini Marekani hamuwezi Mchina

Uzi mzima unakua wa watoto.
 
Kabisa mkuu.
Ilitakiwa watu wasiojua chochote kuhusu tarrifs war kati ya USA na China wajichotee hayo maarifa kupitia huu uzi na waweze kuelewa vizuri.
 
Yani nyie waafrica mnaonunua mabeseni na yeboyebo kutoka china ndio mnaweza Ku replace soko la Marekani Kwa mchina.

Soko la Marekani Kwa mwaka linampa mchina Dola bilion 500 sawa na 3% ya GDP ya China..

Wakati soko Zima la Africa linampa mchina Dola bilion 160 tu.

Mpaka hapo utajua nani Yuko kwenye stress Sasa hivi
Hujasema YUS ana anapata kiasi gani toka China. Kwa taarifa hutaona China ikirudi nyuma.
 
Atakayeathirika hapa ni USA pakubwa, China analo soko la bidhaa zake Afrika na Asia, wakati USA anaarithiri watu wake mwenyewe. Juzi nimesikiliza BBC raia mmoja wa USA fundi magari anasema walikiwa wanategenea spare part from China na sasa havipo japo alisema ana amini vitakuja japo kwa ongezeka la dola 70.
Acha coment ya kipumbavu mkuu, africa ni nchi maskini hazina potential ya maana kwa china. Potential market ya china ni USA
 
Ndio kaz mnayoiweza watanzania ushabiki wa kijinga. Nataman mngepata hata muda wa kuja china muda huu kuja kwenye maonyesho ya canton fair kuna kitu mtatoka nacho.
Mkuu kwahiyo wote tuje china? Duh we tuwakilishe tu
 
Yani nyie waafrica mnaonunua mabeseni na yeboyebo kutoka china ndio mnaweza Ku replace soko la Marekani Kwa mchina.

Soko la Marekani Kwa mwaka linampa mchina Dola bilion 500 sawa na 3% ya GDP ya China..

Wakati soko Zima la Africa linampa mchina Dola bilion 160 tu.

Mpaka hapo utajua nani Yuko kwenye stress Sasa hivi
Duh humu watu wanatuaminisha china ana soko sehemu kubwa Africa,us hawezi mbabaisha😂
 
Back
Top Bottom